Diamond Platnumz ahoji kwanini Ali Kiba (mkongwe) hana media yake? Atoa onyo kushindanishwa na wasanii wa Tanzania 'ni wadogo sana kwake'

Diamond Platnumz ahoji kwanini Ali Kiba (mkongwe) hana media yake? Atoa onyo kushindanishwa na wasanii wa Tanzania 'ni wadogo sana kwake'

Watu hawana shukran ndo maana watu wanaona kila mmoja apambane mwenyeeewe.angalia wanaijeria wengi walivyoughaibun wanabebana na wanaitana. Kibongo bongo ni ngumu watu hatuaminiani.
Sawa ndiyo ameshatoboa kwa East Africa, lakin awape support watz wenzake nao watoke mbona Nigeria wanabebana sana!!
 
Naona yeye na media yake wanatumia nguvu kupush iyo EP yake iende, wenzie wamefanya listening party wakaacha mzingo uende wenyewe ila yeye ni kulazimisha mixer kutumia mpaka mahusiano yake
Asikudanganye mtu mkuu.

Hakuna msanii ambae hapendi kufanya promotion ya kazi zake, sema tu inahitaji budget ya maana kufanya hivyo kitu ambacho kimekuwa rahisi kwa Mond kwasababu ana platform nyingi za kufanya hivyo.
 
Mondi hana wakumshindanisha huyo Kiba ni makelele tu yupo kwenye game miaka 18 hana kampuni wala lolote la maana yani yupo yupo tu

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Hapa duniani tunatofautiana akili na nyota, Alikiba ana watu wengi ila amekosa akili za kuwageuza kuwa chanzo cha mapato zaidi ya kukomaa na mziki tu. Siku akiacha kuimba sijui tu.
 
Asikudanganye mtu mkuu.

Hakuna msanii ambae hapendi kufanya promotion ya kazi zake, sema tu inahitaji budget ya maana kufanya hivyo kitu ambacho kimekuwa rahisi kwa Mond kwasababu ana platform nyingi za kufanya hivyo.
Anachokifanya sio promotioni ila ni stunts/kiki tu
 
Hii inanipa picha pia kuhusu lile tukio jingine la bondia namba moja nchini kama anavojinasibu yeye, bwana Mwakinyo kukataa mpambano na twaha kiduku sabab ya kulinda brand yake isishuke. Hili naliona kwa mondi nae kukataa tuzo za ndani anataka kulinda brand yake sababu ikitokea akakosa tuzo kama ya msanii bora wa mwaka kwa Tanzania, hii inaweza kumuharibia kiasi fulani kwa tuzo za nje.
Kwamba Diamond amezuia kuanzishwa kwa tuzo za ndani?

Kama kuna msanii wa ndani ambae atafanya vizuri kuliko Mond endapo zikianzishwa hizo tuzo, kwanini asionekane hata kwenye tuzo za nje??

Yani Mond akubalike tuzo za nje kisha aje kufeli kwenye hizi za makopo mtakazoanzisha?

Basi watakuwa wanatumia vigezo tofauti na vile vya kule nje, na kama wanatumia vigezo tofauti unashauri tukubali vigezo vipi, vya ndani au nje?
 
Leo hii nashangaa sana Diamond hataki tena kuwekwa kwenye tuzo za nchini kwao na amesahau kwamba tuzo hizo zilimtangaza kwa namna moja au nyingine.

Naona Domo amekuwa mshamba sana na amejisahau sana.

Kuwazidi wasanii wenzio mafanikio sio kwamba ndo umewazidi kuimba, hutaki kushindanishwa na wasanii wa ndani kwamba unawakandamiza, mbona wasanii wa Wanigeria, Marekani wanashiriki kwenye tuzo za nchi zao tena na wasanii wachanga waliowazidi kila kitu.

Domo acha maneno, wakina Wizkid, Burnaboy ni wakubwa lakini hawanaga ushamba kama huo.
 
Namuunga mkono, kwa alipofika asishindane tena tz sababu watu wanatumia vibaya nafasi yake na effort aliyoweka ktk mziki wake wanataka shortcut kupanda kwa kumdhihaki na kujifananisha naye!

Kitu ambacho kinamshusha morali,wacha ashindane kwa watu wanapthamini mziki wake!
 
Ficha ujinga wako hapa. Tanzania tunaendeshwa na wivu na majungu. Sasa unategemea nini kama kwenye mirabaha hakupata kitu.

Diamond yuko sahihi, amevuka zamani sana hiyo level.

Unaandaa tuzo majaji ni watangazaji wa clouds, eatv na efm utegemee watafanya haki.
 
Unashupaza shingo kumtetea ambaye wengine tunamwona kama upuuzi tu, huo ujasiri wa kusikiliza nyimbo zenye matusi matusi unaupata wapi ukiwa na Wazazi wako hata na Watoto wako, au ndiyo kile kizazi cha digital.com?
Kwanini usisikikize kwaya au Qasida? Unataka ukasikilize Bongoflava na wazazi wako ili iwe nini yani??

Watu mna hoja za kitoto sana, huo mziki wa marekani wenyewe unaweza kuusikiliza ma wazazi wako kwakua tu hamuelewi kinachoimbwa, ila ikitafasiriwa hapatakalika kabisa. Kuna mziki wenye ujumbe sikuizi??

Hii ni karne ya 21th acheni kulazimisha maisha ya zama za mawe?
 
Me nnachoamini 'Jembe halichagui Shamba' sasa jembe likisema silimi kwenye kibustani sababu sio hadhi yangu.. hapo napata mashaka kidogo na ubora wa hilo jembe[emoji57]
 
Back
Top Bottom