Let assumes Diamond angemuacha kipindi kile ambacho washika dau wamemkataa,BSS imemkataa .Hivi hizo hela za kulipa angezipata wapi?
Hao watu wa sasa wanaye muona wa maana wangemwona wapi?
Hata kama wangemwona wange mvumilia na kumbeba kama Diamond? Kuna kipindi cha nyuma Mondi wakati akimzunguzia Harmonize,alisema ilifika kipindi alitamani kuachana na Harmonize sababu ya maneno ya watu ya kumkatisha tamaa eti "Harmo anafanana na Yy,atapoteza mda na hela yake".Ila yy aliziba sikio akapiga moyo konde akambeba mpaka leo.
Issues sio kulipa alichomfanyia Diamond,Harmonize ni zaidi ya hela aliyomlipa na hata Diamond alichofanyiwa na Papa Misifa ni zaidi ya hela aliyo mlipa.
Kwa hiyo si shangai Mondi kuposti sababu hawa wa historia ambayo HAITAKUJA KUFUTIKA never.
Alafu Mondi kawa fair sana kwa Harmonize pamoja na kumlipa hiyo million 600,kamwachia Youtube acc,Kamwachia brand yake ya Harmonize,Kamruhusu kuimba nyimbo ambazo zilisimamiwa na WCB.
Hivi unamjua Kizz Daniel?Yule kabla ya kutoka ktk label ya G Worldwide iliyomtoa alikuwa anaitwa Kiss Daniel,lkn baada ya kutoka wakamwambia kwanza haruhusiwi kutumia jina la Kiss Daniel ,Youtube acc na hata kuperform nyimbo alizoziimba chini ya G worldwide.
Hivi unajua Davido chini ya Label yake ya DMV wasanii wake wote nyimbo zao na video zao Youtube zipo kwenye acc ya Davido,hamna hata mmoja mwenye account yake binafsi.Mayorkun pamoja na ukubwa wake hana account yake binafsi ya Youtube.
Hivi unamjua Joeboy ambaye mwaka jana ametikisa Nigeria kwa vibao vyake viwili baby na beginning,kama hujui nyimbo zake zote zipo kwenye acc ya empower,hana account binafsi ya Youtube.
Barakha Da Prince wakati anaondoka Rockstar yy mwenyewe alikili ana nyimbo mbili moja kafanya na Casper Nyvest nyingine na Sarkodie,RockStar wamezizuia na account ya Youtube aliyofunguliwa chini ya RockStar wamemzuia kutumia.
Sasa ukitafakari utagundua WCB walikuwa fair sana kwa Harmonize.Kama wangesema wampigie mahesabu basi kuanzia brand ya jina lake,acc Youtube na vinginevyo angelipa hela ndefu sana.
WCB wao walizuia hizi nyimbo ambazo zipo kwenye Afrobongo sababu nyingi walizisimami wao,ndio wakadai hela yao.