Diamond Platnumz ajaza uwanja unaoingiza watu 70,000 Sierra Leone

Diamond Platnumz ajaza uwanja unaoingiza watu 70,000 Sierra Leone

Nna mashaka na ufuatiliaji wako wa burudani za Afrika mashariki,unaendeshwa na chuki mkuu narudia Tena Chuki ni adui wa Haki,Hakuna mpigaji matasha bora kama Diamond hapa Bongo video zake zipo YouTube zimegaa kajionee mwenyewe halafu urudi na kauli za Diamond hata bure hajazi
Hatuzungumzii video za youtube mkuu,tunazungumzia ilo tamasha mnalosema amejaza watu elfu 70,hayo ya youtube hata akijaza watu milioni haituhusu,hatutaki mpotoshe watu hata kama mnanunuliwa tecno na kuwekewa bando na WCB...Halafu acheni hizo tabia mtu akitoa maoni ambayo WCB amyapendi mnasema ni chuki,mbona watu hawamchukii AY,FA,Prof Jay? Ambao nao kiuchumi wapo vizuri!!
 
sioni kitu cha ajabu, ishakuwa kawaida sasa, Chibu ni level nyingine na ni mjanja, kwa sasa unaona kabisa jamaa kajikita zaidi kwenye nyimbo za kurusha mashabiki hata kama hawajui kiswahili, kuna ngoma kama yope, babalao, kitorondo, Nana na nyingine ni silaha Kali sana kwenye show, hawa wanaoimba ngonjera wakienda nje show zinapoa maana hawaeleweki.

kiasi kingine cha comments za haters humu wanaokesha google ili kuna kumkosoa Chibu kwa sababu zisizo na mantiki ni ishara tosha kwamba diamond kafanikiwa mno, (mafanikio yanapozidi maadui na mashabiki huongezeka zaidi).

naona kwasu kwasu wameegamia point moja ambayo ni dhaifu, eti hakuwa peke yake🙂🙂 mshaambiwa Diamond ndio alichaguliwa kuwa mburudishaji mkuu kwenye hili tamasha na ndio maana ni yeye pekee aliyepewa interview ya radio siku ya tukio, wale wengine walikuwepo kupasha pasha tu tamasha huku attention yote ukiwa kumsubiri. Diamond kufanya unyama wa sina yake ambao hata YouTube tumeuona......Diamond ni level nyingine hana mpinzani kwa ukanda huu
 
Kweli kuwa hater kipaji,kuna MTU kakujibu si chini ya mara moja kuwa hakuna show ya MTU mmoja bado huelewi yaani ukianda show ya msanii Fulani lazima wawepo wasindikizaji huwa wanatangulia kabla ya Main Act
Umefatilia MSINGI WA JIBU LANGU au coz ulishachagua upande umeamua tu nawe kuja kua di
 
joseph1989,
Tunachokijadili hapa sio u mainact was mond,tunachokijadili hapa ni chibudenga na tale kutudanganya hiyo show ilikuwa yao na chibu ndiye aliyejaza uwanja wakati mwaka Jana ilifanyika na watu wakajaa hivo hivo,ni km fiesta hats manfongo akiwa main act watu bado watajaa tu
 
Kwa akili yako ushawai ona show ya mtu mmoja,muda mwingine akili mnaziachaga wap lkn,ukiambiwa kaja haimaanishi alikuwa pekee yake lazima wawepo wasanii wengine maana hana mapafu ya kuperform masaa sita pekee au wewe ungeweza au unazani kuna show ya masaa 2 kisha inaisha? Hizi chuki zinawashushia heshima kwa kuchangia thread pasipokufikiria
Tunaposema diamond peke yake tunamaanisha show ni ya kwake yeye ndo kaindaa then kaalika wasanii wengine sio kualikwa km alivyoalikwa huko Sierra Leone,wewe ni mbumbumbu
 
4by94,
Sijui unasomaje hizi post za watu wengine lakini kama ungekuwa unazisoma vizuri usingejijubu hivyo. Umejibu kama vile tunabishana jambo ambalo siyo kweli. Inawezekana waswahili tumezowea ubishi kiasi kuwa hata kama hakuna jambo la kubisha tutajaribu kutengeza mazingira ya kubishana.
 
4by94,
Unataka kusema asingekuepo chibu watu wasingekuja? Mbona mwaka Jana hakuwepo na watu walijaa hivo hivo?
 
Tunachokijadili hapa sio u mainact was mond,tunachokijadili hapa ni chibudenga na tale kutudanganya hiyo show ilikuwa yao na chibu ndiye aliyejaza uwanja wakati mwaka Jana ilifanyika na watu wakajaa hivo hivo,ni km fiesta hats manfongo akiwa main act watu bado watajaa tu
Kwa hiyo juzi hapa pambano la Mwakinyo aliyejaza mwakinyo au Dogo Mfaume.Au Burnaboy aliyejaza Burnaboy au Joh Makini.

Wewe najua Mondi humpendi nishabishana
na wewe sana,kama humpendi mtu acha kumfuatilia atakukera na utaumia.

Yashafanyika matamasha kibao akina Cabo snoop,Wizkid,Davido,Psquare,Koffi kama main act yaani wao ni kitavu na mvuto wa hiyo show.

So kuwa Main act maana yake walio ingia wengi wao wamefuata kumtizama main act.

Mwache ajisifu kuwa Main act ktk nchi ambayo hawaongei kiswahili,sio swala dogo sababu yy ndiye MAIN ACT na utaumia sana.

Next week Gunea Bisau,as MAIN ACT another day another show in Anglophone country.
77114229_2856984911026588_5620358901567972982_n.jpg
 
Back
Top Bottom