Diamond Platnumz ajibu shutuma ya kudaiwa Wasafi ni wanyonyaji

Diamond Platnumz ajibu shutuma ya kudaiwa Wasafi ni wanyonyaji

Msanii wa kimataifa Diamond Platnumz akifanyiwa mahojiano na kituo Cha habari cha DW Swahili nchini Germany amejibu baadhi ya maswali aliyoulizwa na mwanahabari Moja Kati ya swali ni kuhusu tuhuma ya baadhi ya watu kusema Wasafi ni wanyonyaji.

Diamond amejibu kama ifuatavyo

Nimekuwa nikiwachukua wasanii wachanga nakuwaleta Wasafi wakiwa hawana majina na kuwageuza kuwa biashara kwa kuwekeza hela nyingi unakuta natumia mpaka 500M Kwenye uwekezaji kwa msanii mmoja katika kubrand, kumtangaza na kufanya sanaa yake iwe kubwa ndio maana baada ya kumchukua msanii tunamfundisha vitu vingi Kwenye industry ya mziki ambayo alikuwa hajui tunamsaidia kwenye kuimba, kucheza na namna ya kumaintain status yake kwenye mziki ndio maana unakuta kabla ya kumtoa msanii inatuchukua miaka au miezi ili kumfanya awe full package kabla hatujamtambulisha kwenye industry.

Industry yetu inazidi kukua na baadhi ya mambo watu wanaanza kuyaelewa hasa yanahusu biashara ya mziki tunachofanya sisi Wasafi ndio hata industry ya mziki wa Marekani wanafanya kwenye label nyingi shida ni Moja msanii ukishamfanya kuwa mkubwa na akishaona hela nyingi zinaingia kwenye label anaingia tamaa anatamani hela yote angekuwa anapata yeye ndio maana anaona kama ananyonywa, anashindwa kujua hii ni biashara na tumewekeza hela nyingi kwake, hakuchangia chochote kipindi tunamkuuza.

So lazima kuwe na return ya kile tulichowekeza mfano mimi sio kwamba hela zote napata peke yangu, lazima niwalipe wakina Sallam, Babu tale na Mkubwa fella ndio biashara ilivyo hauwezi kuondoka kirahisi tu njoo hapa tumalizane wakati pia hii label inalipa kodi na ipo kisheria na inatambulika na mamlaka ya mapato mfano last year tumelipa kodi 100M hivi tukikuachia kirahisi tu nani atalipa kodi? Hivi kuhusu kipaji kingine tutachokileta kwenye label nani atagharamia?

Nini Maoni yako kwenye majibu haya ya Mondi
 
Anasema amewekeza 500m kwa msanii kama vile ilikuwa ni fadhila na sio biashara lakini hasemi jumla ya mapato ambayo huyo msanii ameiingizia kampuni kwa kipindi chote anafanya kazi chini yao kupitia makato ya 60/40... ni mentality ile ile ya unyonyaji tu.
 
Anasema amewekeza 500m kwa msanii kama vile ilikuwa ni fadhila na sio biashara lakini hasemi jumla ya mapato ambayo huyo msanii ameiingizia kampuni kwa kipindi chote anafanya kazi chini yao kupitia makato ya 60/40... ni mentality ile ile ya unyonyaji tu.
Kama unahisi Ni unyonyaji na wewe fungua company uwe unamlipa mfanyakazi wako sawa na unachoingiza
 
kwenye ulimwengu wa kibiashara, ni sahihi mwenye hisa nyingi kupata faida kubwa. hapo mwamba yuko sawa kabisa, anavuna alichopanda. yani sauti yako tu na una mashairi ya kuunga unga! tena nakusaidia kutunga, eti tugawane pasu kwa pasu? hata mm siwezi kukubali huo upumbavu.. kama mtu anaona ananyonywa alipe gharama za uwekezaji wangu, kisha aende zake. no free lunch in B0NG0!
 
Back
Top Bottom