Diamond Platnumz ajibu shutuma ya kudaiwa Wasafi ni wanyonyaji

Diamond Platnumz ajibu shutuma ya kudaiwa Wasafi ni wanyonyaji

Uzuri ni kwamba wasanii wenyewe pesa wanazoambiwa watoe ili waondoke "wanazimudu"

Kabla ya kuingia WCB hizo pesa wangetajiwa hivi wangeweza hata jua zinakopatikania?

lakini sasa hivi wanatajiwa pesa na wanatoa,hata kama sio zao ila wameshatengenezewa njia

ya kupata pesa,kukopa popote wakapata hizopesa, Haina cha unyonyaji this is Business na uzuri zaidi

walalamikaji ni vipepe yasiowahusu sijawahi ona hata siku 1 wahusika wenyewe wakisema wanaonewa,maana wanajua walipotolewa.
 
Mkuu mbona kama unamsea mtu nafasi yake kwani kuna sehemu amesema wamemshikilia asijitegemee
Mataga wa wcb mnalia-lia sana mmebaki wapweke lebel imebaki na pisi ya boss na mbosso ambaye naye soon anasepa🤣🤣🤣
 
Tatizo kubwa mnoo la misukule wa NDOMO Ni kukosa kumbukumbu.

Utayasikia hii ni DUNIA ya KIBEPARI, haluna msaada pale Wasafi ni biashara. WCB siyo Charity.

Ukiyaambia, yes ilikuwa ni biashara na kila mtu wanalipana pesa.

Utayasikia tena hukubyakipanua MDOMO Kama CHAI JABA. Mtu kasaidiwa halafu Hana hata shukrani kabisa. Yaani unatakiwa uadhiviwe, ushughulikiwe, utoe pesa halafu uendelee kumwabudu Kibwengo Domo.

View attachment 2299063
Don't hate a nigga driving a cullinan
He effs better girls than you
Eats better than you
Knows people better than you
Has more cash than you
And I guess he is happier than you

Hata kama una mdomo mzuri whati is the worth of it kama vyote hvo kakupita
 
Msanii wa kimataifa Diamond Platnumz akifanyiwa mahojiano na kituo Cha habari cha DW Swahili nchini Germany amejibu baadhi ya maswali aliyoulizwa na mwanahabari Moja Kati ya swali ni kuhusu tuhuma ya baadhi ya watu kusema Wasafi ni wanyonyaji.

Diamond amejibu kama ifuatavyo

Nimekuwa nikiwachukua wasanii wachanga nakuwaleta Wasafi wakiwa hawana majina na kuwageuza kuwa biashara kwa kuwekeza hela nyingi unakuta natumia mpaka 500M Kwenye uwekezaji kwa msanii mmoja katika kubrand, kumtangaza na kufanya sanaa yake iwe kubwa ndio maana baada ya kumchukua msanii tunamfundisha vitu vingi Kwenye industry ya mziki ambayo alikuwa hajui tunamsaidia kwenye kuimba, kucheza na namna ya kumaintain status yake kwenye mziki ndio maana unakuta kabla ya kumtoa msanii inatuchukua miaka au miezi ili kumfanya awe full package kabla atujamtambulisha kwenye industry.

Industry yetu inazidi kukuwa na baadhi ya mambo watu wanaanza kuyaelewa hasa yanahusu biashara ya mziki tunachofanya sisi Wasafi ndio hata industry ya mziki wa Marekani wanafanya kwenye label nyingi shida ni Moja msanii ukishamfanya kuwa mkubwa na akishaona hela nyingi zinaingia kwenye label anaingia tamaa anatamani hela yote angekuwa anapata yeye ndio maana anaona kama ananyonywa anashindwa kujua hii ni biashara na tuwekeza hela nyingi kwake hakuchangia chochote kipindi tunamkuuza.

So lazima kuwe na return ya kile tulichowekeza mfano mimi sio kwamba hela zote napata pekee yangu lazima niwalipe wakina Sallam, Babu tale na Mkubwa fella ndio biashara ilivyo hauwezi kuondoka kirahisi tu njoo hapa tumalizane wakati pia hii label inalipa kodi na ipo kisheria na inatambulika na mamlaka ya mapato mfano last year tumelipa kodi 100M hivi tukikuachia kirahisi tu nani atalipa kodi? Hivi kuhusu kipaji kingine tutachokileta kwenye label nani atagharamia?

Nini Maoni yako kwenye majibu haya ya Mondi
Kwenye haya maelezo mbona unyonyaji upo

Hii ni kwa wanaojua kuchambua mstari mmoja baada ya mwingine kama biblia
 
Ni kweli, mtu anaenda pale mweupe kabisa ana kipaji ambacho pia kinahitaji kutengenezwa then after few years anaona cash flows kubwa anaingia tamaa anataka afanye yake! Its OK kufanya yako lakini kuna mikataba uli sign inaelekeza cha kufanya ukitaka kutoka kabla mkataba hauja expire. Kama umefikia huo ukubwa vunja mkataba na kuondoka kwa amani bila maneno mingi.
 
Kwenye haya maelezo mbona unyonyaji upo

Hii ni kwa wanaojua kuchambua mstari mmoja baada ya mwingine kama biblia
Ukiona mtu amefikia level za kunyonywa ujue anavyo vya kunyonywa ambavyo havikuja kimiujiza. Ngombe lazima umlishe vizuri ili atoe maziwa uyakamue, sasa ukianza kukamua unaambiwa maziwa ni ya Ngombe si yako! Ndio mtoa maziwa ni Ngombe lakini bila juhudi zangu kumlisha asingetoa maziwa!

Hivi jeuri ya fedha ya Ray Van au Harmonize unafikiri ni akili zao tu? WCB sio kituo cha misaada it's a business! Ukizidiwa akili kwenye biashara sababu ya njaa zako shauri yako! No free lunch! Ni sawa uanze biashara kinyonge sababu ya mtaji alafu utake huruma kwa washindani giants!

Ndivyo label kubwa duniani zinavyofanya ikiwemo Bad Boys record! Hao madogo waliotoka WCB wote wako vizuri financially baada ya "kunyonywa" kitu ambacho ilitosha kuwapa reasonable credits WCB badala ya kuwaponda, huko nyuma ukigombana na producer au meneja unarudi "mavumbini" completely! Wengine walidhurumiwa walipodai chao boss akanuna na kufunga mirija yote na ilibidi waende kuomba msamaha kwa magoti wakirekodiwa na media!

Panapostahili credit tuache unafiki! Mimi si shabiki wa Bongo Fleva wala sijawahi kuwa shabiki wa Diamond lakini Imagine hii Bongo Fleva zama hizi bila uwepo wa atmosphere ya WCB! Kuna thamani wameweka na waheshimiwe kwa hilo.
 
Umeongea point kubwa sana
 
Diamond yupo sahihi kabisa. Tena zama hizi za wcb ni afadhali, kijana anajitoa na anaweza kuanzisha label yake. Zaman ukijitoa mahali ndo umekwisha, unaishiaaa kabisa na kusahaulika. Bravo Sana to diamond
 
Back
Top Bottom