Nashauri Basata wangeweka kitengo maalum kwa ajili ya kupitia mikataba ya kati ya wasanii na lebo au wasanii na kampuni nyingine,kabla ya kuingia kandarasi.
Ni sawa na hii tume ya ushindani(FCC)ambayo inadhibiti na kupitisha mikataba inayotumiwa na Microfinaces kutoa mikopo kwa wateja au kama ambavyo benki kuu inadhibiti sheria na mikataba ya mikopo baina ya benki za kibiashara na wateja wao.
Hii itaondoa haya malalamiko baada ya mtu kuingia kwenye mikataba ndio anaanza kelele,kwa mazingira yetu wasanii wengi hawana elimu ila wana vipaji kwahio mambo mengi haya ya taratibu na sheria hawajui hasa ikizingatiwa wengi wanapoanza usanii wanakuwa hawana exposure,hawana uelewa na wana shida ya pesa hivyo ni rahisi kukubali chochote kilichopo mezani.
Haya malalamiko hayajaanza leo,tangu bongo movie walikuwa wakilaamikia wahindi,Ikaja hawa bongofleva wakamlaumu sana Ruge na wengineo,Na sasa Diamond nae ameingia kwenye lawama lakini yote haya ukiangalia ni kukosa udhibiti na uelewa mdogo wa wasanii.
Mwaka jana kama sikosei kuna msanii wa kike sijui ni Nandy au nani alilalamikia kampuni fulani sijui ilikiwa benki ile kumtumia na kumlipa malipo kiduchu.
Sasa tunawauliza nyie wasanii mnapoingia mikataba mwanzoni huwa hamuoni?kama mnaona kwanini hamkatai?Kwa hili naona Diamond yupo sahihi,kama ulikubali mikataba basi kubaliana na madhara yake pia.
Kwahio lazima kuwe na udhibiti wa hii mikataba,kama hii ni biashara basi Basata kama chombo cha serikali lazima ijue nini kimeandikwa humo na je hakikiuki sheria na taratibu za nchi?
Inawezekana pia katika hili Diamond akawa anatumia Lebo yake kujinufaisha zaidi dhidi ya wasanini wadogo kwa kisingizio kwamba amewekeza kwao,kwahio udhibiti unahitajika hapa.