Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vipi unamiliki biashara ya vyombo vya habari n entertainment?Leo CEO wa Wasafi Media Diamond Platnumz ametangaza kwa mara ya kwanza mkoa ambao utaanza kurushwa Wasafi FM, kumbuka Diamond alithibitisha mwezi wa 4 mwaka huu kuwa wamepata idhini ya kurusha nchi nzima. So rasmi wameanza na Mwanza ambapo tayari imepata frequency ya 104.1 lakini sababu aliyotoa Diamond kwanini wameamua leo eti ni kwasababu ya kushinda manager wake Babu Tale kura ya maoni CCM Morogoro Kijijini.
Hii ni sababu ya kijinga sana kwahiyo kama Babu Tale asingeshinda inamaana angesogeza muda?
Kingine zaidi waliwaambia wapenzi wao wapige kura za kuchagua mkoa gani waanze nayo kurusha Wasafi FM kura nyingi ikapata Mkoa wa Tanga. Sasa sijajua kwanini wameanza na Mwanza? Kama mlikuwa na mkoa wenu mfukoni kwanini mliwasumbua watu wapige kura?
Sababu za kibiashara!Ameshindwa kuanza na mkoa wake wa kigoma kama anavyojiita mwenyewe kuwa ni mzawa huo si utumwa