Diamond anafanikiwa kwa sababu anapenda anachofanya, ukipenda unachofanya hutoangalia umaarufu unaopata wala pesa unayoingiza, pesa na mafanikio haviwezi kukupumbaza ukaacha kufanya unachokipenda, ukifanya jambo kwa maslahi lazima utaridhika baada ya mafanikio kidogo kwa sababu hukipendi.
Siri ni moja vijana, penda unachofanya na fanya unachopenda, mafanikio huja kwa kile unachopenda kukifanya. Ni siri ya watu wote waliofanikiwa. Hakuna kazi inalipa kuliko nyingine, penda unachofanya.
hongera Diamond.