Program Manager
JF-Expert Member
- Aug 6, 2018
- 2,763
- 3,955
Mtandao maarufu wa kupanga charts za muziki duniani wa Billboard umeachia makala wakielezea namna ya kupata mafanikio kimataifa kwa kutumia mtandao wa Youtube huku wakimtolea mfano star wa muziki wa Tanzania @Diamondplatnumz
Makala hiyo imeandikwa "Wanamuziki wa Marekani wanatafuta njia za kutoboa kwenye Youtube, Wanapaswa kusoma mikakati ya kufanya na kuachia video kutoka kwa wasanii wa Kiafrika."
Wasanii wa Magharibi wanaweza kujifunza kutoka kwa kile wanachokifanya wasanii wa Kiafrika , haswa wale ambao wamefanikiwa kimataifa," Amezungumza meneja wa 'Youtube Music Trends' Kevin Meenan, ambaye anasimamia ukusanyaji na uchambuzi wa data za chati za Muziki za YouTube. Ameelezea kuwa alivutiwa sana na mbinu pamoja na ubunifu ambao anautumia msanii wa bongo flava wa Tanzania Diamond Platnumz kwenye chaneli yake ya YouTube - sehemu moja tu ya mikakati ya ujasiriamali ambayo inajumuisha kituo cha redio ya FM na TV pamoja na usimamizi kamili wa huduma, kurekodi, kuchapisha na kampuni ya burudani, @WCB_Wasafi.
Kwenye Makala hiyo Kevin Meenan amesema Ukubwa wa diamond kwenye Youtube ni wakustaajabisha akiwa na Subscribers Millioni 3.6 na zaidi ya jumla ya views Millioni 980 huku 80% ya watamazaji wakiwa wanatokea nje ya Tanzania. Kwa kipimo cha kipindi cha kutoka Mei 1, 2019 hadi Mei 1, 2020 Meenan anasema kwamba, kimataifa Diamond alitazamwa zaidi na watu wa Nchini ya Kenya ikifuatiwa na Tanzania na Marekani.
Billboard wameeleza kuwa Msimamizi huyo wa Youtube Trending alishangazwa kukuta Diamond ameweka zaidi ya video 600 kwenye mtandao wa Youtube "Kwa kweli ilibidi nichunguze mara tatu ili kuhakikisha kuwa ilikuwa sawa," Alielezea. Wamesifia kuwa Diamond anaweza kuweka hadi video 20 akitangaza Official video moja tu huku wakitolea mfano wa wimbo wa Jeje ambapo ukiachana na Official video, kuna dance video, cartoon video, lyrics video pamoja na official audio.
Kwenye Makala hiyo Billboard wameelezea kuwa uchunguzi wao umegundua kuwa wasanii wengi ambao wamefanikiwa kufikisha subscribers zaidi ya Million 1 basi huwa wanatazamwa zaidi na watu wa nje ya nchi zao.
Sent using Jamii Forums mobile app