Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Mwanamuziki nguli anayetamba duniani kwa kazi zake na ukwasi mkubwa Naseeb Abdul Juma Issack almaarufu kama Diamond Platnumz anastahili kupewa tuzo ya heshima ya udaktari wa falsafa na vyuo maarufu duniani kwa jinsi ya mchango wake kwa mtu mmoja mmoja, jamii kwa upana wake, taifa/serikali (kupitia kodi anazolipa).
Ukimya wa taasisi za elimu ya juu duniani zikiwemo za ndani ya Tz unatia shaka kubwa kwasababu Bingwa huyu ame-reform wanamuziki wenzake na kutransform maisha ya vijana duniani kwamba alistahili hata nishani ya rais kama siyo tuzo ya Grammy. Uwezo wa Diamond haulingani na wa Khadija Kopa, Cpt. Komba na Mzee Nnauye ambao hawa wamefanywa/walifanywa Makada nguli wa chama tawala.
Matokeo ya kazi za Diamond katika tasnia ya muziki ni makubwa kuliko matokeo ya kazi za Maprofesa ambao hata wao wamestaafu bila hata single wakati ni wataalam wa muziki kwa ngazi ya uweledi wa uzamivu (PhD). Ziko wapi UDSM, OUT, SAUT, TUDARCO nk? Tunasubiri Mungu ampandishe cheo kwenda kwake ndiyo tumpe tuzo ambayo hatoiona kwa macho yake?
Tz tumpaishe Diamond wetu ili ulimwengu wa nje nao ujumuike nasi katika kumpaisha. Tuzo ya Muziki ya Grammy ndiyo inayoongoza dunia tangu karne ya 20 na ukiipata ile utakuwa na ela ya kuweza kufadhili bajeti ya serikali na kazi zako hazitakwama sokoni hata siku moja.
US ilimpaisha Jacko (Michael Jackson) hadi akaongoza dunia kwa kupata tuzo 100 hadi anafariki, katika hizo, ni Grammy Music Award ndiyo ilimpa kitita kilichomfanya billionaire. Sasa hapa kwetu CCM inamtumia Diamond kwa viwango vya chini mno ambavyo siyo hadhi yake. Siasa ni sumu.
Nadhani dunia imtendee Mondi haki anayostahili. Bila wivu kwa Diamond, Konde Boy hasingefanya bidii na kufanya vizuri kama anavyofanya hivyo Mondi amemtengeneza indirectly. Karibuni tujadili.
Taswira kwa hisani ya google.