Diamond Platnumz ashinda tuzo tatu AFRIMA

Hivi kuna watu bado wanamcompare diamond na ali kiba kimuziki na katika mafanikio ndani ya muziki??au ndo ubishi tu wa asili watu wanao hawataki kukubali kuwa mondi ni noma
Hivi nani huwa anawacompare...ifike muda sikiliza muziki uburudike hayo mengine unajitesa bure!!
 
Tunzo 3 ni hat trick (kwenye soccer) mara ya 3 hii anashinda tunzo tatu kwa pamoja.

*2012 - Kili awards
*2014 - Channel O awards
*2016 - Afrimma Nig Awards

2018 - Diamond ongeza juhudi zaidi Inshallah utapata tunzo 3 nyingine, kupitia hesabu za sequence and series in mathematics.
---Hongera sana Diamond Platnumz
 
ahahaaa maajabu diaomond yupo overated na anguko lake litakuwa kubwa sana eti best male east africa toka lini diamond akawa juu ya eddy kenzo au camilion?

Hivi hii kesi imefikia wapi hadi sasa?! Ishatolewa hukumu au bado inaendelea?
Diamond kazindua wimbo wake mpya ni ule wimbo wa Saida Karoli wa Salome kaumix mix.

Mwanasheria wa Saida anapanga kwenda mahakamani. Itakuwa nafasi ya Saida Karoli kurudi kwenye muziki maana atalipwa mamilioni naona. Tusubiri tuone.
 
Kwa kweli tusha zoea, he is making Tz proud, jamani huwezi kumcompare na yoyote kwa sasa hapa bongo, nnacho shukuru ni kuwa akikosa tuzo mbili leo ana pata tano wiki inayo fuata.
*kumchukia diamond ni kujitafutia ugonjwa wa moyo na mshtuko maana kila siku utanuna na kulalamika.
 
Eddy kenzo? Diamond akienda uganda anajaza show huku eddy kenzo akija bongo labda afanye show maisha clabu kuhusu kenya ndo usiseme
hebu niwekee link diamond aliofanya show uganda? diamond kenya anajaza watu maana huwa anaenda show za bure sio kwamba watu wanalipia mashow ya promotion hata eddy kenzo angejaza usitufanye wajinga hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…