Diamond platnumz asipodhibitiwa ataleta maafa

Diamond platnumz asipodhibitiwa ataleta maafa

tarehe 25 jana siku ya xmas diamond alikuwa na show ya funga mwaka pale Darlive watu,
watu walijitokeza kwa wingi sana kiasi kwamba hakuna pa kutema mate, ukinyanyua mguu hakuna pa kuweka na bado wengine waliokuwa nje walishindwa kuingia
Imefika wakati sasa huyu jamaa show zake zipangwe kwenye viwanja vikubwa kama uwanja wa taifa au ule wa uhuru la si sivyo siku itakuja kutokea maafa makubwa kwa
watu kukosa hewa
kukanyagana na misongamano
mamlaka husika wanaweza kuchukua taadhari mapema kabla janga halijatokea na kuanza kusingizia freemason
jionee picha mwenyewe kilichojiri jana

Wala yakitokea sitakuwepo.
Mie napenda live band.
 
DUH BINADAMU TUPO TOFAUTI SANA MI NADHANI WAJARIBU KUANGALIA NA IDADI YA WATU NA MAENEO ZINAPOFANYIKA SHOO ZAO......
 
Haya tunasubiri na huyu kibakuli wao alete nyomi kama ana ubavu
ali kiba ana potential nzuri tu ya kufanya vizuri ila jamaa namuona kama vile anajihold kurudi nyumasijui kwanini...... mond saiv ni mkali kama umeme huwezi kumlinganisha na kiba kuna tofauti kubwa sana na wanaowalinganisha hua nawashangaa sana siongei kwa ushabiki bali ukweli ninao uona
 
Hapo dawa ni kuongeza bei ya viingilio ili kudhibiti idadi ya watu.
ANGALIZO: Kwa kiingilio cha chini ya 50000 msitarajie msongamano kwisha kwenye show zake.
hivi ulishawahi kujiuliza kwa nini Dar Live ilijengwa Mbagala na si Oysterbay??....
 
Tarehe 25 jana siku ya Christmas, Diamond alikuwa na show ya funga mwaka pale Darlive watu,watu walijitokeza kwa wingi sana kiasi kwamba hakuna pa kutema mate, ukinyanyua mguu hakuna pa kuweka na bado wengine waliokuwa nje walishindwa kuingia.

Imefika wakati sasa huyu jamaa show zake zipangwe kwenye viwanja vikubwa kama uwanja wa Taifa au ule wa Uhuru la si sivyo siku itakuja kutokea maafa makubwa kwa watu kukosa hewa,kukanyagana na misongamano.

Mamlaka husika wanaweza kuchukua taadhari mapema kabla janga halijatokea na kuanza kusingizia freemason
jionee picha mwenyewe kilichojiri jana.

Ninyi mnatakiwa mumpate Donald Trump kama nyampara wenu maana ujinga umezidi sana
 
And he is great at making his own. There will never be another DIAMOND PLATNUMZ
 
Back
Top Bottom