Diamond platnumz, baba ni baba tu, rudi kwa baba yako

Diamond platnumz, baba ni baba tu, rudi kwa baba yako

Diamond; rudi kwa baba yako kijana kabla yupo hai, akija kuondoka duniani hatuombei ila ataondoka na kinyongo na wewe, Hivyo hutakua hapo ulipo. Watu wanakudanganya eti hata akikulaani haikupati sio kweli kabisa baba ni baba tu. Hata vitabu vinasema watii wazazi wako hao ndy mungu wa duniani. Pia mama Diamond hivi unajisikiaje kua na maisha mazuri wakati uliezaanae anapata taabu! wewe ndy ulie takiwa kumsema mwanao amtunze baba yake? Inamaana wewe hukuwahi kufanya kosa na ukasamehewa?
Au huyo baba asinge fanya jihudi za kukupata ungempata huyo mtt?
 
Diamond; rudi kwa baba yako kijana kabla yupo hai, akija kuondoka duniani hatuombei ila ataondoka na kinyongo na wewe, Hivyo hutakua hapo ulipo. Watu wanakudanganya eti hata akikulaani haikupati sio kweli kabisa baba ni baba tu. Hata vitabu vinasema watii wazazi wako hao ndy mungu wa duniani. Pia mama Diamond hivi unajisikiaje kua na maisha mazuri wakati uliezaanae anapata taabu! wewe ndy ulie takiwa kumsema mwanao amtunze baba yake? Inamaana wewe hukuwahi kufanya kosa na ukasamehewa?
Au huyo baba asinge fanya jihudi za kukupata ungempata huyo mtt?
Huwez jua ya moyoni ndugu, kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe
 
Mbona amesema kinachomuumiza ni maneno ya watu wanaosema kwamba mwanae(diamond) hamsaidii. Kwa kauli hii ina maana Mond anamsaidia baba akee,
Hajamtupa mzee wake anamsaidia
 
acha akipate cha moto,ubaba hauishii kumwaga sperms tu,ubaba ni malezi,kama baba hakuwepo pindi diamond anamuhitaji the most,why diamond awepo kwenye maisha ya baba yake now?Diamond hakuna kurudi nyuma na kumsamehe siyo lazima umsaidie
Well...a responsible father hawezi kuishia kwenye fertilisation yapaswa awe part ya process yote kuanzia mimba hadi mtoto akue.

Tunajua maisha ya kibongo yana lots of ups n down ila bado ukiwa kama mzazi whether baba au mama ni aibu ,dhambi na uuaji kutelekeza familia yako.
 
tatizo mizee ya hivi inakeraga sana,hasa wanapojitokeza baada ya kuona mtoto aliyemtelekeza kipindi ambacho mtoto anauhitaji hasa wa mapenzi ya baba(akiwa kinda),amekuwa na mafanikio!hii inanipa picha kwamba laiti huyu mtoto asingefanikiwa na kuendelea kuwa majalala kama enzi hizo maana yake ni kwamba utelekezaji ungeendelea tu,toka utoto mpk ukubwani.

hili ni somo zuri sana kwa wanaume/wanawake wanaotelekeza watoto pasi na kuanticipate potentiality ya iko kiumbe huko mbeleni...uzuri fundisho limekuja kupitia superstar ili hadhira kubwa ijifunze kupitia kinachoendelea kati ya chibu na mdingi wake. Yaani mtu wa hivi kumsamehe kiroho safi(kumsafia nia) ni ngumu sana maana utakuwa unafikiria kuwa hili limdingi limejirudi baada ya kuona now I am somebody in this world,vyenginevo asingejirudi huyu,so unahisi kabisa huyu hajaja kwa sababu eti amekuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanawe kwa sasa la hasha,bali mafanikio ndo yametengeneza mahaba kwa mwanawe!hatari sana hii.
 
Mleta mada na wadau wengine mliochangia hadi hapa,hivi baba yake Diamond anaitwa Mzee Platnumz?
 
Hata mm ilinichukua muda sana kumsamehe baba yangu ingawa bado mpaka leo anaishi na mama. Baba ambae hafanyi majukumu yake kwa mtoto wanaumiza sana watoto kisaikolojia. Naelewa jinsi diamond anavyojisikia kuhusu baba yake. Inahitaji neema kumsamehe irresponsible father.

Ni kweli kabisa hawa mababa wanawacha mama zetu kuteseka na watoto bila kuwajali kwa lolote. Mfano, leo huyo baba kwa kuwa amemuona Diamond fedha imekamata ndiyo anaomba msamaha. Utakuta mama alipata shida sana kumlea mwenyewe mtoto wakati baba anastarehe na mwanamke au wanawake wengine. Leo ameingia steji ya fainali uzeeni ndiyo anamkumbuka mtoto.

Loh loh looooooooooh! nina hasira.................................
 
Mzee platinum alikuwa chicha ila bg up ana kumbukumbu nzuri" nilipenda aliposema mm ni super star sihojiwi bila pesa haha ha ha ha.
 
Jamani kuna vitu mtu anapenda kusamehe ila vingine siyo kusamehe ni swala la moyo
Kwa hiyo na sisi tunamkosea Mungu asitusamehe km kuna makosa ya moyo tunafanya
Binadam hajakamilika ndugu kuna leo na kesho
 
Diamond; rudi kwa baba yako kijana kabla yupo hai, akija kuondoka duniani hatuombei ila ataondoka na kinyongo na wewe, Hivyo hutakua hapo ulipo. Watu wanakudanganya eti hata akikulaani haikupati sio kweli kabisa baba ni baba tu. Hata vitabu vinasema watii wazazi wako hao ndy mungu wa duniani. Pia mama Diamond hivi unajisikiaje kua na maisha mazuri wakati uliezaanae anapata taabu! wewe ndy ulie takiwa kumsema mwanao amtunze baba yake? Inamaana wewe hukuwahi kufanya kosa na ukasamehewa?
Au huyo baba asinge fanya jihudi za kukupata ungempata huyo mtt?
Kweli kabisa mkuu Umesema jambo la maana
Diamond kutomsamehe baba yake hapat faida wala hasara(ukitoa mambo ya imani) chukulia kiuibinadam tu hatapungukiwa kitu wala kuongezeka
Na kumsamehe pia hapat hasara
Ni vema tu amsamehe
 
itakuwa anapepo la kutokusamehe.....Mwanadamu gani asiyejua kusamehe!! baba kaomba msamaha inamaana kalitambua na kukiri kosa, kwanza mtu unapozidi kuweka hasira moyoni unazidi kujijaza sumu ambazo aghalabu kuja kuleta matokeo mazuri, Msamehe Baba maisha yazidi kuendelea. ukijijua wewe hupendi kusamehe watu basi ujihakikishie wewe ni Mkamilifu
 
Nimeona interview ya clouds tv na mzee platnumz, kweli jamaa kachoka. Huyu ni baba yake na mwanamuziki matata nchini Diamond Platnumz.
Kama alikukosea wewe na mama yako, mbona ameshasema mumsamehe? Bila ya yeye Diamond asingekuwa alivyo sasa. Hivyo inatakiwa Diamond awe na moyo mkubwa wa kusamehe mtu ambaye ameshaomba kusamehewa. Binadamu tuna mapungufu na ni ujasiri ulioje kukubali kuwa umekosa na kuomba kusamehewa. Diamond ni kioo cha jamii, awe na moyo wa kusamehe. Pia kwa Queen Darlin, baba yenu kawaomba msamaha wote. Msaidieni. Nadhani kwa kiasi fulani anaweza akawa mtu wa 'sembe'.

P.s: Sikujua kama Diamond na Queen Darlin ni mtu na dada yake. Wanashea baba, tena huyu aliyehojiwa na Clouds Tv Weekend chat.
Mpaka ukielewa what happened then u will change n be in a position to judge
 
Minamshauri kabla ya kumsamehe akapime DNA kwanza kama ni baba yake halisi, na kwa jinsi hali ya sa ivi ilivyo huku mitaani watu wanatelekeza sana watoto tena kwa makusudi tu. Hiyo iwe funzo kwa wale waliokataaa na kutelekeza watoto, huwa naamini mtoto akitelekezwa mungu huwa anamshushia baraka.
 
KILA ANAYESAMEHE NAE ATASASAMEHEWA DIAMOND INABIDI ALEGEZE KAMBA AWE NA MOYO WA KUSAMEHE.
 
Diamond mwisho wake mbaya sana atakuja juta amzarauye babaye maisha yake ni kama tone la maji huwezi kujua mapenzi ya baba yako na mama yako yaliingia dosari gani kwa mwanaume mwenye akili hayo mambo usiyaingilie unatakiwa uyakwepe usukubali kujumuishwa humo inahitaji akili sana sababu ni rahisi sana kwa mama kumwaminisha mtoto mabaya ya baba yake kuliko baba kumwaminisha mtoto
TATIZO La WATANZANIA Kupenda Kuweka Mbele Chuki Zetu BINAFSI Ktk Issue Sensitive!! KWANI Wkt Huyo Mzee Anakula Raha Na Kushindwa KUWAPATIA Msaada Walau Wa Yale Mahitaji Muhimu Kwa BINADAMU, Alizuiwa Na Nani!!?? HIVI Angekuwa Amekubali Kuwa Yeye Ndiye Baba Mzazi Wa Diamond Na KUKUBALI Kumtunza Mtt Wake, Hata Kama Walikosana Na Mzazi MWENZAKE, NANI Angemzuia Kutoa Matunzo Kwa Mtt Wake!!! LKN Yeye Alikwepa Majukumu Ya Kumtunza Mzazi Akiwa Mjamzito Na Hatimaye Mtt!! AKAENDELEA Kula Bata Tu, Na Nilivyomuona Na Kumsikia Ni MHUNI Wa Mjini Tu!! Maneno Ya KISELA Tu!!! So Ameleta USELA MAVI!!! PIA Kama Diamond Angekuwa Hana AKILI Za KUONA Na KUFAHAMU, Kuwa Babake Yupo Hai Na UWEZO Kiuchumi Tu!! MBAYA Zaidi Ni Pale Mtt Anaposhindwa Kupata Hata VIFAA Vya Shule Na Chakula!!! HUKU Ukiambiwa Babako Yuko Hai Tu Na Ana Kauwezo!! ILA Waliwakataa Tokea Mimba Hadi Leo Hii!! Mtt / Wtt Wanaona Mama Yao Anavyotaabika Kuwalea!! LEO Baada Ya Mtt KUPATA MAFANIKIO KWA UWEZO WAKE MUNGU, ETI Baba Ndio ANAJITOKEZA Na Kusema Mi Ndiye Babake!!! PUMBAVUU!!!! WKT Ule Life Taiti Ulikuwa Mbali, Ila Kipindi Cha Neema Unajitokeza!!!!! ALAFU Unataka Upatiwe Huduma, Ambazo Ww Ulizikimbia Kuzitoa!!! ALAFU WATANZANIA Kwa CHUKI BINAFSI Tu, Wanamuona Mtt Ndiye Mshenzi!!!! MTAKUWA Hamtendei Haki Diamond Na Wtt Wooote Waliokataliwa Na Baba Zao Tokea MIMBA, Hadi Walipopata Mafanikio!!!! UZURI Yule MSELA AMEKIRI Mwenyewe, Kuwa Ktk Issue Za Kuwasiliana Na Kumpatia PESA Halina Tatizo, Diamond Analifanya!!!! JE Ww Ulitaka Diamond Afanye Lipi Zaidi!!!!?? ACHENI CHUKI ZENU BINAFSI, KTK ISSUE SENSITIVE!! WATU Wengi Wanafanya Huo UJINGA Alafu Wanakuja KUOMBA MISAADA KWAO!!!!
 
Dili la Vodacom limewakuna wazee wa clouds sababu hawajapata cha kukatiwa. Na huyo Baba yake nae anajiendekeza kufata hao mbona hana tatizo na mwanae kutafuta kiki kusikiliza wenye wivu kama wa Clouds kutampeleka zaidi anapotaka kwenda...bila kujijua. Tamaa mbaya.. Bora hata Dee hambebi bebi kama pochi. Atulie huko huko alipo.
Vizuri mleta mada umejua sasa kuwa Darlene ni dada yake, mnaodai kamtupa baba yake amuoni alivyo na watoto wa baba yake? Mnachekesha. Mnavyojaribu kumchafua ndio anabarikiwa, endeleeni na hongera zenu.
 
Back
Top Bottom