Diamond Platnumz badili mwenendo before it’s too late!

We jamaa yeye ana exposure kumzidi Justin Bieber ?, uraibu hauna hayo , anamzidi whitney exposure ? Anamzid exposure Lamar Odom ? Mbona hawa wote wamemzidi hela na exposure ? Justin ni Tajiri kumzid diamond Mara mia ila alitumbukia huko ikawa kisanga, vip kuhusu wayne ? Anamweza kifedha ? Sasa yale ma seizure yalimkutaje ? Mzee akienda huko anakoenda anapotea mzee huo ndio ukweli….
 
Mzee unahisi kwanini wamesema Mondi wala sio wewe, Harmonize wala Marioo?
We haupo busy kwenye Shughuli zako?
Watu waliwahi kusema Unavuta Unga?
 
We jamaa ww mimi siku zote siwezi kuzifananisha nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea, ni vitu viwili tofauti.

Hao kina Justin wamekuwa hapo kutokana na mifumo wezeshi ya nchi sasa jiulize Diamond amekuwa hapo alipo kwa mifumo wezeshi ya nchi au mifumo yake?
 
Huyo diamond unamuona kwenye tv wenzako tunabang nae mpuuzi wewe!


Wenzako tunampa ushauri "Naseeb" wewe na kichwa chako kimejaa kamasi endelea kumpa ushauri "Diamond"


Nadhani Kwa kichwa chako kilichojaa uharo wa Bata hutaelewa nilichoandika!


Kahyaba wa buguruni wewe

Sent from my Pixel 5 using JamiiForums mobile app
 
Mzee unahisi kwanini wamesema Mondi wala sio wewe, Harmonize wala Marioo?
We haupo busy kwenye Shughuli zako?
Watu waliwahi kusema Unavuta Unga

Mzee unahisi kwanini wamesema Mondi wala sio wewe, Harmonize wala Marioo?
We haupo busy kwenye Shughuli zako?
Watu waliwahi kusema Unavuta Unga?
Na pia jiulize kwann kina Mwana fa na jide km sikosei walirudi clouds kuomba msamaha baada ya kufungiwa vioo alaf Daimond hakurudi ila siku hizi wanarejesha wenyewe kambi kwake.

Jibu ni rahisi tutachafua vp brand yake, msanii anaishi kutokana na brand yake ndio chanzo chake cha pesa. Sasa hapo jiulize ni kwann Harmonize hana ubalozi wowote ule wa maana na pia kwann nchi hii kwa wasanii Daimond ni balozi na nwengine ni ma influencer?

Au wewe pia unaamini Hamisa na Alikiba hawajawahi kuchafua hali ya hewa ila ni Zuchu na Diamond tu ndi huwa wanachafua
 
Ww hadi unaingia kaburini huwezi kubang na Diamond labda useme kingwendu ww unampa ushauri unashindwa kujipa ww mwenyewe ushauri wa mafanikio na ww ujue nitolee makamasi yako hapa
 
Ishue ni kama anakula madawa ni noma mkuu, I am not a hater , this dude inspires alot of young people sawa ? Using narcotics ni tatizo mkuu hata uwe kama Jay Z , unakwenda DMX alitembea kimasihara sana. Unakumbuka the other day siku Yanga anafanya parade ya trophy ? Alishuka kwenye gari and he was drunk as hell talking to random people, that was not cool unless otherwise uniambie it was staged. Mimi binafsi sikubaliani na swala la mtu kuwa mteja, kwa hapa tz kuna kipindi chidy alikuwa juu kuliko diamond lakin saivi mkuu unaonaje ?
Anyways kama hatumii its cool, kama anatumia there is no getting out mpaka aende rehab, wengi wanaaoanzaga madawa huwa wanadhani wanaweza wakaacha kabla watu hawajajua yan huwa wanadhani ni kama kunywa pombe kumbe ni balaa..Muda ni rafiki mzuri tuombe uzima mkuu
 
Naomba nikujibu kistaarabu maana unaonekana una upeo wa akili.

Hayo majukumu ndiyo yamemfanya adondokee kwenye unga, kazi na uwekezaji katika hizo biashara zake vimemzidia na suluhisho alilolichagua ndio hilo.

Sikutaka kusema mengi sababu hii haikuwa sehemu ya lawama bali a wake up call.

Kama kweli unamkubali sana jamaa tafuta namna za kumnusuru, mimi ambaye wala sio shabiki yake nimekuja hapa kumpa onyo na ombi la kubadilika, wewe tafuta njia yako.

Kila kitu kina matokeo, mazuri au mabaya yote ni matokeo. Lakini, tunaweza kuamua aina ya matokeo ya kuyapokea.

Hii thread ni serious, sio cheap stunt na sina ninachonufaika na hilo hadi nifanye hivyo.
 
Kwahiyo una amini mleta mada kaleta hii habari ili amchafue Diamond?
 
Wewe jamaa mbona unaonekana una akili zako tu?
Yani unataka kusema Diamond ana majukumu kuliko tajiri wa Dunia Elon Musk?
I rest my case!
 
Ile siku ya parade la Yanga ndipo niliposhtuka na mimi, ni kama alikuwa high.
Niliogopa sana
 
Stimu ya Heroin ni mara buku ya orgasm- Sasa unadhani inaachika kiurahisi tu.

Wengine utamu wa ngono tu umetuteka ,sembuse unga?
 
Mkuu,

Na mimi nilikuwa na mawazo kama yako.

Ila pia, nikaona hii ni nafasi ya kuzungumzia tatizo la uraibu wa madawa ya kulevya kama ugonjwa katika jamii yetu.

Yani hata ukiongelea hili tatizo in the abstract tu bila kuwa too personal kwa Diamond, hayo ni mazungumzo yanayohitajika, kwa sababu anayevuma ni Diamond na madawa ya kulevya, lakini kuna watu wengi wana uraibu wa hayo madawa mpaka pombe. Wanaotuhusu na wasiotuhusu.

Pia, ni nafasi ya kuzungumzia gharama halisi za kuwa msanii maarufu, mambo ya afya ya akili, na jinsi gani tunaweza kusaidia kuandaa wasanii wetu wawe na maamuzi bora baada ya kupata umaarufu.

Waingereza wana msemo "Be careful what you wish for, you might receive it".

Ni mtihani mmoja kuushinda umasikini, kupata utajiri na umaarufu.

Ni mtihani tofauti kabisa kuweza kuishi vizuri baada ya kupata utajiri na umaarufu.

Kuna actor mmoja Mmarekani amefariki jana, anaitwa Matthew Perry, alikuwa katika show moja maarufu inaitwa "Friends" kwa miaka 10 kabla ya ku act katika shows nyingine nyingi. Alisema kuwa alifurahia umaarufu kwa miezi nane tu, baada ya hapo aliona umaarufu kuwa ni kero tupu.
 
Asante.
 
Kama daima hukuwahi kuwa mhanga wa tatizo la dawa za kulevya unaweza usione uzito ama umuhimu wa thread hii ya kuonya.

Kwa nilivyoguswa na thread hii, leo naeleza familia yangu imetikiswa na tatizo hili baada ya dada yangu kujiingiza humo.

Dada yangu, nisimtaje, naye alikuwa maarufu. Aliingiza pesa nyingi ila baada kukosana na management yake tukashtukia akitumia.

Tulifanya kosa, tulichagua iwe siri kama alivyokuwa akitaka yeye. Kumbe Ilikuwa siri ya kujimaliza, tatizo lilikua badala ya kumalizika.

Hali ikawa mbaya, ofisi yangu ikajaribu kusaidia, lakini akaacha kwa muda na akarudia tena kwa ubaya zaidi hadi akawa kama kawehuka.

Kiukweli, hakuamua kuacha kwa dhati hadi tulipoamua suala lake kuliweka wazi, kila anayemfahamu akajua hali yake.

Hiyo ikasaidia akarudi nyumbani na akatuomba mwenyewe apelekwe sober. Tunashukuru kwa sasa ameondoka katika tatizo hilo.

Ila, hasara aliyopata ni kubwa. Alikua na maduka mawili ya nguo, yalifilisika. Alikuwa na gari mbili aliuza zote na alikuwa na nyumba aliuza.

Isitoshe, aliuza vitu vyake vya ndani vyote. Akawa sifuri. Alituomba aende nje akasomee uigizaji, tumefanya hivyo na sasa yuko nje.

Kwanini thread hii ni muhimu?

Ni kwa sababu, njia ya kumsema hadharani mtu anayetumia dawa za kulevya humfanya aone uzito wa kosa lake na kuchukua hatua.

Kwa uzoefu wa dada yetu, baada ya kutoroka nyumbani, tulipoamua kumsema hadharani alirudi nyumbani na kuomba apelekwe sober.

Aliona aibu kwani ile siri aliyoomba tumfichie ilifichuka. Na ilikuwa dawa kuu iliyomsaidia kubadilika, lakini tayari dawa zilishamfilisi.

Kumfichia siri hii Nassib hakuwezi kumsaidia kuondokana na tatizo hilo hadi azomewe kama hivi hadharani, ndivyo kumsaidia.

Kama hatutamuunga mkono Nifah na tukaona kama ana chuki na Nassib, muda utaongea na tutarudi na majuto kama sisi kwa dada yetu.

Ieleweke kuwa, hakuna mtumiaji wa dawa za kulevya anayefurahia utumiaji wa dawa hizo baada ya kuathirika, ila hulazimika.

Hili janga ni kubwa zaidi ya tunavyofikiri, ila huwezi kuuona ukubwa wake hadi liingie kwenye sebule ya familia yako.

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…