Naandika hii thread kwa machungu sana, hili limeniwia vigumu sana kulisema hapa, lakini imenibidi!
Siandiki nionekane nilisema, wala sipendi siku thread hii ije kufukuliwa kwamba yametimia, wala siandiki kama umbea. Hili ni suala serious juu ya kijana mwenzetu huyu maarufu pengine kuliko kijana yeyote kutokea katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.
Ni nini kimekusibu Naseeb? Kwanini ulifikia uamuzi huo wa kutumbukia huko ulikotumbukia? Imeniumiza sana, kweli!
Mimi sio shabiki wako, ila siwezi kupinga wewe ni Icon, watu wanakutazama kama nembo ya upambanaji!
Na sidhani kama unajua wewe ni mtu mkubwa kiasi gani! Mambo mengi ambayo huwa unafanya yanathibitisha hilo, hili pia likiwemo.
Ndugu unayesoma haya, kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya wasanii na maisha yao hasa hapa kwetu Bongo lazima utakuwa umewahi kusikia tetesi za Diamond kutumia madawa ya kulevya, mengi yamesemwa… wengi wamesema.
Alianza Harmonize kipindi wapo kwenye ‘bifu’ kali baada ya kuachana na iliyokuwa label iliyomsimamia katika safari yake ya muziki ambayo mmiliki ni Diamond, kila mtu anajua jinsi mtifuano ulivyokuwa mkali baada ya Harmonize kuondoka.
Na katika mtifuano huo ndipo Harmonize alituhabarisha kuwa Diamond ni mteja wa madawa ya kulevya, binafsi sikuamini na niliomba isiwe kweli.
Sikuamini kwakuwa katika ugomvi kila mmoja atasema lolote la kumuumiza mgomvi wake, haikuwa na mashiko sana.
‘Dada wa Taifa’ Mange nae mwaka huu amehakikisha kwa kujiamini kabisa kuwa Diamond anatumia madawa ya kulevya, amesema hivyo mara nyingi… pia sikuamini.
Sasa baada ya maneno na tuhuma hizo juu yake mimi binafsi nikaingia ‘chimbo’
Kila mmoja ana chanzo chake kikuu cha habari, hasa kwa sisi wadau wa habari zote ngumu na nyepesi…
Nikauliza ili nijihakikishie je ni kweli yanayosemwa!
Nilichoambiwa ndicho kimenifanya niandike hii thread, nilijibiwa kiufupi kabisa, “NI KWELI ANATUMIA”
Siko hapa kubishana wala kumshawishi yeyote akubaliane na chanzo changu, mimi mwenyewe ndio naujua uzito wa chanzo changu hicho nyeti. Kiufupi ni kwamba chanzo changu hiki kikiniambia kesho nitafariki naanza kabisa kutubu!
Lengo kuu ni kuongea na muhusika mkuu, Jamii Forums ni platform kubwa pengine atafikishiwa haya.
Tafadhali Naseeb, badili mwenendo. Bado hujafikia hatua mbaya, unaweza kuacha kuanzia sasa ukarudi ktk hali yako ya kawaida.
Hukuona yaliyomkuta Whitney Houston? Wewe una ukubwa gani kumzidi malkia yule wa muziki wa muda wote?
Mifano ni mingi, kwa maslahi ya Taifa tusingependa siku ifike na wewe tukutolee mfano.
Wewe ndiye unayeujua ukweli zaidi kwanini umefikia hatua hiyo, ila tafakari nafasi yako ulipo na ubadilike.
Nifah
Kama daima hukuwahi kuwa mhanga wa tatizo la dawa za kulevya unaweza usione uzito ama umuhimu wa thread hii ya kuonya.
Kwa nilivyoguswa na thread hii, leo naeleza familia yangu imetikiswa na tatizo hili baada ya dada yangu kujiingiza humo.
Dada yangu, nisimtaje, naye alikuwa maarufu. Aliingiza pesa nyingi ila baada kukosana na management yake tukashtukia akitumia.
Tulifanya kosa, tulichagua iwe siri kama alivyokuwa akitaka yeye. Kumbe Ilikuwa siri ya kujimaliza, tatizo lilikua badala ya kumalizika.
Hali ikawa mbaya, ofisi yangu ikajaribu kusaidia, lakini akaacha kwa muda na akarudia tena kwa ubaya zaidi hadi akawa kama kawehuka.
Kiukweli, hakuamua kuacha kwa dhati hadi tulipoamua suala lake kuliweka wazi, kila anayemfahamu akajua hali yake.
Hiyo ikasaidia akarudi nyumbani na akatuomba mwenyewe apelekwe sober. Tunashukuru kwa sasa ameondoka katika tatizo hilo.
Ila, hasara aliyopata ni kubwa. Alikua na maduka mawili ya nguo, yalifilisika. Alikuwa na gari mbili aliuza zote na alikuwa na nyumba aliuza.
Isitoshe, aliuza vitu vyake vya ndani vyote. Akawa sifuri. Alituomba aende nje akasomee uigizaji, tumefanya hivyo na sasa yuko nje.
Kwanini thread hii ni muhimu?
Ni kwa sababu, njia ya kumsema hadharani mtu anayetumia dawa za kulevya humfanya aone uzito wa kosa lake na kuchukua hatua.
Kwa uzoefu wa dada yetu, baada ya kutoroka nyumbani, tulipoamua kumsema hadharani alirudi nyumbani na kuomba apelekwe sober.
Aliona aibu kwani ile siri aliyoomba tumfichie ilifichuka. Na ilikuwa dawa kuu iliyomsaidia kubadilika, lakini tayari dawa zilishamfilisi.
Kumfichia siri hii Nassib hakuwezi kumsaidia kuondokana na tatizo hilo hadi azomewe kama hivi hadharani, ndivyo kumsaidia.
Kama hatutamuunga mkono Nifah na tukaona kama ana chuki na Nassib, muda utaongea na tutarudi na majuto kama sisi kwa dada yetu.
Ieleweke kuwa, hakuna mtumiaji wa dawa za kulevya anayefurahia utumiaji wa dawa hizo baada ya kuathirika, ila hulazimika.
Hili janga ni kubwa zaidi ya tunavyofikiri, ila huwezi kuuona ukubwa wake hadi liingie kwenye sebule ya familia yako.
Ova