Nadhani hata wewe ukisoma hoja yako huielewi, maana yake uko kwenye ubishani siyo mjadala, kwa sababu kila nikikusoma unahama kwenye hoja yako ya msingi.
Kufanya show kubwa au ndogo, maana yake ni nini? Hii ni tofauti na hoja yako. Kwamba kutumbuiza kwa saa nyingi jukwaani ndiyo uliona ndiyo dalili ya kutotumia dawa za kulevya.
Kwa msingi wa hoja yako, show hata iwe kubwa namna gani, lakini kama itafanywa kwa dakika ishirini tu jukwaani sio kitu kwa mujibu wa hoja yako ndugu yangu.
Umeshawahi kumwona Chid Benz au TID wakitumbuiza jukwaani? Marehemu Banza Stone alikuwa anakaa jukwaani na Twanga Pepeta kwa saa ngapi?
Hivi ndugu yangu unaona kusafiri na commercial flights unaona kama vile kusafiri na roli la mizigo? Kwa sababu sikuelewi unavyohusisha shida na kusafiri kwenda Marekani.
Unamaanisha nini?
Ova