Tukubaliane kuwa yule mama yake naye ni tatizo kubwa, hivi halioni hilo kwa mwanae? Ameweza kucontrol mangapi ya Diamond hilo limshinde? Diamond ana access na wataalamu wa kila aina angetaka wamsaidie kuishinda addiction asingeshindwa.
Diamond wa kipindi cha wema alikuwa amekonda bado kapauka pauka kiasi, Diamond wa kipindi cha Zari alikuwa ana ka mwili, anavaa smart anapendeza, akivaa suti inakaa, huyu Diamondi wa Tanasha na wa Zuchu aisee pamoja na hela zote hatazamiki, kakondeana, ngozi imevutika, ana mirasta yaani haeleweki.
Anyways: It is never too late, kama ni addict kweli bado ana nafasi ya kupona, watu wake hawawezi kumwambia ukweli yamkini wanafaidia na yeye kuwa alivyo. Na pakisambaratika kila mtu atabeba mbao zake atasambaa!
Binafsi ntasikitika sana tukimpoteza huyu kijana wa Tandale aliyefanikiwa kufika mahali ambapo wasanii wetu hawakuweza kufika, “Super star”.