Diamond Platnumz badili mwenendo before it’s too late!

Diamond Platnumz badili mwenendo before it’s too late!

Anastahali pongezi kwa alipofika ila ukitoa mafanikio yake kifedha kwenye muziki wake alifikia hatua ambayo angeweza kufanya makubwa zaidi ila ni kama akapotea kwa kufanya muziki wa nyumbani zaidi.

Mwaka 2014 Diamond anatoa Remix ya Number One na kushirikisha Davido kama msanii anayefanya vizuri East Africa na akaweza kupata collabo kutoka Nigeria. Burna Boy alikuwa anafanya collabo na wakina AKA kwenye All Eyes On Me.

Ukiangalia safari ya muziki kwa Burna Boy miaka ya 2016 anatoa Pree Me kama msanii wa kawaida tu pale Nigeria wakati huo Diamond ndiyo anatamba na kufanya collabo na AKA, Akothee. Mpaka 2017 anatoa wimbo na Ne-Yo.

Mpaka 2019 Harmonize akaweza kufanya kazi na Burna Boy, hapo ndiyo Burna akatoa Album ya African Giant iliyomtambulisha Duniani. Yani wakati Diamond anatoa A Boy from Tandale 2018, Burna Boy alikuwa bado anajitafuta.

Sasa hivi Burna Boy yupo kwenye level nyingine kabisa ambayo Diamond angeweza kuifikia ila sijui nini kilimkwamisha.
Bidhaa alizouza kwa wenyewe bei yake ndio inamfikisha hapo labda aongeze bidhaa zaidi kwa wenyewe ndio atatusua zaidi ya hapo,lakini pia washamwona hana Cha maana sana wamempimia level hiyo ndio kiasi chake na hata akiongeza mzigo kwa wenyewe watampimia kidogo tu hatoweza fika level za kina wizkidayo au burna boy.
Hapo ndio kwishne.
 
Huo ni ukweli mchungu, mwamba alianza kwenye upunda na sasa kaamua alambe kabisa, wanavyoanza wanasema wanapandisha energy wakishakua addicted ndio vile tena....
Wasi wasi wangu asije akamuharibu na kale kabinti
Maana ya Binti ni [bikra], Zuu kishafumuliwa mda sana toka Diamond alipoimba collabo na mama mkwe wake hapa ndipo Diamond alizawadiwa Katoto na akakata Utepe.
View: https://www.youtube.com/watch?v=k5BZiM1pggE
 
Naandika hii thread kwa machungu sana, hili limeniwia vigumu sana kulisema hapa, lakini imenibidi!

Siandiki nionekane nilisema, wala sipendi siku thread hii ije kufukuliwa kwamba yametimia, wala siandiki kama umbea. Hili ni suala serious juu ya kijana mwenzetu huyu maarufu pengine kuliko kijana yeyote kutokea katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

Ni nini kimekusibu Naseeb? Kwanini ulifikia uamuzi huo wa kutumbukia huko ulikotumbukia? Imeniumiza sana, kweli!
Mimi sio shabiki wako, ila siwezi kupinga wewe ni Icon, watu wanakutazama kama nembo ya upambanaji!
Na sidhani kama unajua wewe ni mtu mkubwa kiasi gani! Mambo mengi ambayo huwa unafanya yanathibitisha hilo, hili pia likiwemo.

Ndugu unayesoma haya, kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya wasanii na maisha yao hasa hapa kwetu Bongo lazima utakuwa umewahi kusikia tetesi za Diamond kutumia madawa ya kulevya, mengi yamesemwa… wengi wamesema.

Alianza Harmonize kipindi wapo kwenye ‘bifu’ kali baada ya kuachana na iliyokuwa label iliyomsimamia katika safari yake ya muziki ambayo mmiliki ni Diamond, kila mtu anajua jinsi mtifuano ulivyokuwa mkali baada ya Harmonize kuondoka.
Na katika mtifuano huo ndipo Harmonize alituhabarisha kuwa Diamond ni mteja wa madawa ya kulevya, binafsi sikuamini na niliomba isiwe kweli.
Sikuamini kwakuwa katika ugomvi kila mmoja atasema lolote la kumuumiza mgomvi wake, haikuwa na mashiko sana.

‘Dada wa Taifa’ Mange nae mwaka huu amehakikisha kwa kujiamini kabisa kuwa Diamond anatumia madawa ya kulevya, amesema hivyo mara nyingi… pia sikuamini.

Sasa baada ya maneno na tuhuma hizo juu yake mimi binafsi nikaingia ‘chimbo’
Kila mmoja ana chanzo chake kikuu cha habari, hasa kwa sisi wadau wa habari zote ngumu na nyepesi…
Nikauliza ili nijihakikishie je ni kweli yanayosemwa!
Nilichoambiwa ndicho kimenifanya niandike hii thread, nilijibiwa kiufupi kabisa, “NI KWELI ANATUMIA”

Siko hapa kubishana wala kumshawishi yeyote akubaliane na chanzo changu, mimi mwenyewe ndio naujua uzito wa chanzo changu hicho nyeti. Kiufupi ni kwamba chanzo changu hiki kikiniambia kesho nitafariki naanza kabisa kutubu!

Lengo kuu ni kuongea na muhusika mkuu, Jamii Forums ni platform kubwa pengine atafikishiwa haya.

Tafadhali Naseeb, badili mwenendo. Bado hujafikia hatua mbaya, unaweza kuacha kuanzia sasa ukarudi ktk hali yako ya kawaida.
Hukuona yaliyomkuta Whitney Houston? Wewe una ukubwa gani kumzidi malkia yule wa muziki wa muda wote?

Mifano ni mingi, kwa maslahi ya Taifa tusingependa siku ifike na wewe tukutolee mfano.
Wewe ndiye unayeujua ukweli zaidi kwanini umefikia hatua hiyo, ila tafakari nafasi yako ulipo na ubadilike.

Nifah
Muwe mnaelewa mambo nyie!si mnasema wanaume tafuteni hela!!? Sasa utafutaji una namna nyingi na hiyo namna ndio inayomtesa simba hadi atumie hayo makitu!!

Utajiri ni siri na siri ya utajiri ndio utajiri yenyewe!!

Anahesabu siku na masaaa,lazima arnde walau kwa style hiyo huko anapopaswa kwenda akatumike baada ya utajirisho!!!

Mtupende wanaume acheni kututia presha za utafutaji hadi tunauza nafsi!!
 
Uzi wako umenipa mixed feelings
Nimecheka hapo ulipoandika chanzo chako kikikuambia kesho unafariki unaanza kutubu

Nimeshuka para hapo ulipoanza kwa kumtaja kwa jina lake Naseeb kisha ujumbe wake nimejikuta napatwa na goosebumps...nimesikia uchungu

Hope ujumbe utamfikia,kama ni kweli aamue kuacha
Mwenyewe nilijizuia kucheka hapo kwenye chanzo changu, kwakuwa ni habari ya kusikitisha sana nikaacha.

Amen 🙏🏽
 
Akivuka umri alioushindwa ivan atakua na bahati sana. Chai jaba ua jeusi lilimchanganya sana hakutegemea kutoswa ndo maana hadi wa leo anamkana yule mtoto aliyesababisha valentine yake iwe ovyo.

Ustaa una gharama kubwa sana,wanaofaidi matunda yake ni watu wa pembeni ,yeye kutwa stress tupu kubuni mbinu za kubaki juu na kuongelewa daily
Aya yako ya kwanza haina ukweli bwana, halafu wala Diamond hana mpango na Zari kihivyo.
Aya ya pili ndio umetisha 👏🏽👏🏽
 
Mtu anapata wapi ujasiri wa kumfuatilia na kumpangia mtu maisha ya kuishi ?
Ikizingatiwa wewe sio Baba ake wala sio mama ake.?

Jiulize swali mmoja tu Kutumia kwake madawa kunaathir nin ktk maisha yako?

Ama akiwa sio mtumiaji wa madawa kunakunufaisha nin ktk maisha yako.?

Yaani mtu unaamka asubuh asubuh na kushusha kitabu kizima cha maneno kwa kumpangia mtu maisha ya kuishi.

Itoshe kusema kama hakuna lote unalofaidika nalo ungeacha kufatilia maisha ya watu.
Mtu anapata wapi ujasiri wa kumfatilia kiasi cha kujibu hoja za mtu anayefatilia maisha ya watu?
 
Kwani akifanya vizuri sisi huwa inatuhusu nini? It is not about that “Kufuatilia maisha yake” tunatoa maoni yetu kwa jinsi tunavyoona inafaa na si lazima ayafanyie kazi. Halafu hajashauriwa kitu kibaya brother, tatizo ninini?

Sisi wengine ni mashabiki zake humu, unless wewe ni mgeni JF, Nifah ni mtani wa Jadi wa timu yetu, maoni yake ya leo ni constructive sioni ubaya.
Asante darling.
 
Naandika hii thread kwa machungu sana, hili limeniwia vigumu sana kulisema hapa, lakini imenibidi!

Siandiki nionekane nilisema, wala sipendi siku thread hii ije kufukuliwa kwamba yametimia, wala siandiki kama umbea. Hili ni suala serious juu ya kijana mwenzetu huyu maarufu pengine kuliko kijana yeyote kutokea katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

Ni nini kimekusibu Naseeb? Kwanini ulifikia uamuzi huo wa kutumbukia huko ulikotumbukia? Imeniumiza sana, kweli!
Mimi sio shabiki wako, ila siwezi kupinga wewe ni Icon, watu wanakutazama kama nembo ya upambanaji!
Na sidhani kama unajua wewe ni mtu mkubwa kiasi gani! Mambo mengi ambayo huwa unafanya yanathibitisha hilo, hili pia likiwemo.

Ndugu unayesoma haya, kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya wasanii na maisha yao hasa hapa kwetu Bongo lazima utakuwa umewahi kusikia tetesi za Diamond kutumia madawa ya kulevya, mengi yamesemwa… wengi wamesema.

Alianza Harmonize kipindi wapo kwenye ‘bifu’ kali baada ya kuachana na iliyokuwa label iliyomsimamia katika safari yake ya muziki ambayo mmiliki ni Diamond, kila mtu anajua jinsi mtifuano ulivyokuwa mkali baada ya Harmonize kuondoka.
Na katika mtifuano huo ndipo Harmonize alituhabarisha kuwa Diamond ni mteja wa madawa ya kulevya, binafsi sikuamini na niliomba isiwe kweli.
Sikuamini kwakuwa katika ugomvi kila mmoja atasema lolote la kumuumiza mgomvi wake, haikuwa na mashiko sana.

‘Dada wa Taifa’ Mange nae mwaka huu amehakikisha kwa kujiamini kabisa kuwa Diamond anatumia madawa ya kulevya, amesema hivyo mara nyingi… pia sikuamini.

Sasa baada ya maneno na tuhuma hizo juu yake mimi binafsi nikaingia ‘chimbo’
Kila mmoja ana chanzo chake kikuu cha habari, hasa kwa sisi wadau wa habari zote ngumu na nyepesi…
Nikauliza ili nijihakikishie je ni kweli yanayosemwa!
Nilichoambiwa ndicho kimenifanya niandike hii thread, nilijibiwa kiufupi kabisa, “NI KWELI ANATUMIA”

Siko hapa kubishana wala kumshawishi yeyote akubaliane na chanzo changu, mimi mwenyewe ndio naujua uzito wa chanzo changu hicho nyeti. Kiufupi ni kwamba chanzo changu hiki kikiniambia kesho nitafariki naanza kabisa kutubu!

Lengo kuu ni kuongea na muhusika mkuu, Jamii Forums ni platform kubwa pengine atafikishiwa haya.

Tafadhali Naseeb, badili mwenendo. Bado hujafikia hatua mbaya, unaweza kuacha kuanzia sasa ukarudi ktk hali yako ya kawaida.
Hukuona yaliyomkuta Whitney Houston? Wewe una ukubwa gani kumzidi malkia yule wa muziki wa muda wote?

Mifano ni mingi, kwa maslahi ya Taifa tusingependa siku ifike na wewe tukutolee mfano.
Wewe ndiye unayeujua ukweli zaidi kwanini umefikia hatua hiyo, ila tafakari nafasi yako ulipo na ubadilike.

Nifah
Inaumiza sana huyu mwamba aki drop maana ana tu motivate wengi sana.
 
Back
Top Bottom