Diamond Platnumz badili mwenendo before it’s too late!

Diamond Platnumz badili mwenendo before it’s too late!

Hata sie wa huku porini tunaomuona kwenye mitandao tu ukifatilia mahojiano yake hivi karibuni kwenye media mbalimbali unamuona kabisa kabadilika anaongea kama anasinzia anavuta vuta kamasi, haeleweki kabisa,, hata hivyo nimeumia sana hasa kama mama,, ukiisoma hii mada ukayakumbuka ya Whitney Houston unaweza kujikuta unalia tu madawa sio kitu cha kumuombea mtu ni mabaya mno
 
Naandika hii thread kwa machungu sana, hili limeniwia vigumu sana kulisema hapa, lakini imenibidi!

Siandiki nionekane nilisema, wala sipendi siku thread hii ije kufukuliwa kwamba yametimia, wala siandiki kama umbea. Hili ni suala serious juu ya kijana mwenzetu huyu maarufu pengine kuliko kijana yeyote kutokea katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

Ni nini kimekusibu Naseeb? Kwanini ulifikia uamuzi huo wa kutumbukia huko ulikotumbukia? Imeniumiza sana, kweli!
Mimi sio shabiki wako, ila siwezi kupinga wewe ni Icon, watu wanakutazama kama nembo ya upambanaji!
Na sidhani kama unajua wewe ni mtu mkubwa kiasi gani! Mambo mengi ambayo huwa unafanya yanathibitisha hilo, hili pia likiwemo.

Ndugu unayesoma haya, kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya wasanii na maisha yao hasa hapa kwetu Bongo lazima utakuwa umewahi kusikia tetesi za Diamond kutumia madawa ya kulevya, mengi yamesemwa… wengi wamesema.

Alianza Harmonize kipindi wapo kwenye ‘bifu’ kali baada ya kuachana na iliyokuwa label iliyomsimamia katika safari yake ya muziki ambayo mmiliki ni Diamond, kila mtu anajua jinsi mtifuano ulivyokuwa mkali baada ya Harmonize kuondoka.
Na katika mtifuano huo ndipo Harmonize alituhabarisha kuwa Diamond ni mteja wa madawa ya kulevya, binafsi sikuamini na niliomba isiwe kweli.
Sikuamini kwakuwa katika ugomvi kila mmoja atasema lolote la kumuumiza mgomvi wake, haikuwa na mashiko sana.

‘Dada wa Taifa’ Mange nae mwaka huu amehakikisha kwa kujiamini kabisa kuwa Diamond anatumia madawa ya kulevya, amesema hivyo mara nyingi… pia sikuamini.

Sasa baada ya maneno na tuhuma hizo juu yake mimi binafsi nikaingia ‘chimbo’
Kila mmoja ana chanzo chake kikuu cha habari, hasa kwa sisi wadau wa habari zote ngumu na nyepesi…
Nikauliza ili nijihakikishie je ni kweli yanayosemwa!
Nilichoambiwa ndicho kimenifanya niandike hii thread, nilijibiwa kiufupi kabisa, “NI KWELI ANATUMIA”

Siko hapa kubishana wala kumshawishi yeyote akubaliane na chanzo changu, mimi mwenyewe ndio naujua uzito wa chanzo changu hicho nyeti. Kiufupi ni kwamba chanzo changu hiki kikiniambia kesho nitafariki naanza kabisa kutubu!

Lengo kuu ni kuongea na muhusika mkuu, Jamii Forums ni platform kubwa pengine atafikishiwa haya.

Tafadhali Naseeb, badili mwenendo. Bado hujafikia hatua mbaya, unaweza kuacha kuanzia sasa ukarudi ktk hali yako ya kawaida.
Hukuona yaliyomkuta Whitney Houston? Wewe una ukubwa gani kumzidi malkia yule wa muziki wa muda wote?

Mifano ni mingi, kwa maslahi ya Taifa tusingependa siku ifike na wewe tukutolee mfano.
Wewe ndiye unayeujua ukweli zaidi kwanini umefikia hatua hiyo, ila tafakari nafasi yako ulipo na ubadilike.

Nifah
Its too late
 
hata afya yake imekongoroka, uwezo wa kutunga umeporomoka ana flow nyimbo za matusi tu.. he is loosing mentally and physically kila siku.. in 10 years anaweza kuwa vibaya maana balaa la madawa ni kwamba the more you take the more u need it.
wanaomzunguka waache uchawa na upambe wameambie ukweli, family na ma manager wamsaidie..
vita za madawa huwez ishinda mwenyewe , amuulize Lord Eyez katokaje huko.
Kwa ile afya aliyo nayo sasa kwenye hii nyimbo mpya aliyoimba na Kofii mwezi uliopita mimi Buskdokta kwa uzoefu wangu wa miti shamba ni ngumu kuamini kwamba jama Hali Sembe.
 
Vijana wa ki Tanzania mnao tafuta maisha, hivi ndivyo wa Tanzania walivyo mkizipata mtakuwa mnazungumziwa, na ukiona watu wanakuzungumza ujue kuna kitu kikubwa unakifanya ambapo huo uwezo wao kufanya hawawezi.

Ukiona huzungumziwi ujue hakuna ulichofanya, tafuta pesa hadi waseme umemtoa mzazi wako kafara au unauza madawa.

Maneno yasikurudishe nyuma, unapozidi kusemwa ndipo unazidi kupiga msumari pale pale hakuna kurudi nyuma, na ukiona wameanza maneno we unaongeza dozi hadi wakae kimya.

Her mom was dirt poor from Tandale, dogo ame make kufika hapo, maza anakula maisha, imagine from nothin leo ana rolls royce, utamshauri nini? au yeye ndiye akushauri wewe.. 🤣
 
Kwahiyo mkuu na wewe unaweza kutumia madawa ya kulevya ili kuupata utajiri?
Nimekosa kabisa cha kuongea!
Hujanielewa kumbe!
Huyo Simba atapotea kabisa coz nyakati zake za utajiri aliopewa zimeisha!

Nini kinatokea,kinachotokea ni retreat yaani ufanye Nini pale mambo yanapokua magumu kiasi kwamba your days are numbered!?

Ni displacement reaction hufuata,sasa Kila mtu hu retreat kivyake,hao Huwa wanapata pesa na umaarufu kw mkataba fulani toka kwa yule mwenye mwanga za wa ulimwengu!!!

Nimejitahidi labda umenielewa,nikiongeza zaidi ya hapa nitakosea!!!
 
Jipe moyo ukanya barabarani tukuseme then uamini ndio mafanikio yako.

Wema sepetu yuko wapi?
Wa Tanzania walio wengi wana roho za chuki,visasi na chuki binafsi, ndio maana umasikini na wao ni ndugu.

Usimseme Wema Sepetu, ipo hivi muziki ndivyo ulivyo utakutumia na kukuacha, umaarufu utakutumia na kukuacha, hii ni kwa dunia nzima, huwezi kung'aa siku zote.

Kila mtu ni bora katika wakati wake, hata timu za mpira kuna wakati zinang'aa kuna wakati zinapotea. Boxing walikuwepo kina Tyson siwezi sema ameishiwa lakini umri pia unaenda kuna vijana wenye uwezo zaidi wana ku replace, hio ni kanuni rahisi tu.
 
Unatwanga maji kwenye kinu ili upate unga, ukisikisikia kulewa sifa ni pamoja kulewa vilevi, ulevi ulevi wa vitu fulani fulani hivi, hata staili yake ya mahusiano yake ya kimapenzi nayo ni ya kilevi, kijana mdogo huwezi kuwa na wanawake lukuku tena warembo hasa unazaa nao kisha unawaacha. Huyu kijana ilitakiwa apewe ushauri nasaha mapema wakati ndiyo anaanza kupata mafanikio na sifa nyingi ili asijiingize kwenye uraibu wa dawa za kulevya. Kwa sasa ngumu kumtoa huko mpaka aharibikiwe akili. Imekuwa ni kawaida kwa wanamuziki kujiingiza kwenye uraibu ndio kiki kwao ila ni hatari kwa mentality yao na uchumi wao. Hawa wanamuziki totally ni walevi wa pombe, bangi, wanawake/wanaume na ulevi mwingine kama dawa za kulevya skendo za ulevi haziishi kwao. Wana hela za kulewa ushahidi ni nyimbo zao wanazoziimba kusifia ulevi
 
"machungu sana"

Diamond is doing very well, he is way better financial, humzidi hata ukijumlisha ukoo wako wote na ukoo kwa mkweo humzidi.

Kama hiyo ndo akili ya drugs, acha avute, maana yako timamu haijakufikisha popote zaidi ya kukusaidia kupata uchungu

Diamond was asked once kama anatumia madawa, alikataa, akasema hatumii, in that case nachagua kuamini maneno yake kwamba hatumii.
Bogus. Ulitegemea aseme ndio natumia?
 
Cocaine is a hell of a drug...

Asije tu akajichanganya akagusa Fentanyl. Na afya ile mgogoro asubuhi na mapema tu parapanda italia.

Na kuna chanjo ya Cocaine WaBrazil wanasema itakuwa tayari hivi karibuni. Labda itamuwahi....

Screenshot_20231028_164332_DuckDuckGo.jpg
 
Mbaya mbovu ya wasanii wengi kutumia vilevi ni vile wanataka ku maintain vibe wakiwa juu ya stage,pili watu maarufu wanakuwa na pirukushani nyingi kiasi kwamba hata muda wa kupumzika unakuwa finyu hivyo anajikuta anaingia kwenye vilevi kama sehemu ya kumpumzisha na kumuasha vibe ili pesa siku nyengine iingie!.

Refer msanii mkubwa kama Michael Jackson alishawahi sema kitu ambacho alikuwa hakipendi ni tour!!!, Na hizo ndizo zilikuwa zinamuingizia mshiko maana msanii bila show sawasawa na kazi bure!,Sasa kumaintain hiyo ili aendane na vibe la watu kama hatatumia midawa hapo itakuwaje!,mashabiki mtalalama mmetoa hela zenu halafu hamna kitu na mtu anatandika show ya masaa kadhaa..

Nafikiri ni muhimu wasanii wahaswe na wafatiliwe maana nje na kazi wanafamilia pia na watu wanaowategemea.
Umeongea point kubwa sanaa.. unaweza kuta ndani ya masaa 24 yy ana mawili tuu.
Mi naona ana fanya kazi kupitiliza inapelekea uchovu mkubwa...ukichoka sanaa usingizi hauji ndio anaamua kubust mara vinanoga.
 
Mtu anapata wapi ujasiri wa kumfuatilia na kumpangia mtu maisha ya kuishi ?
Ikizingatiwa wewe sio Baba ake wala sio mama ake.?

Jiulize swali mmoja tu Kutumia kwake madawa kunaathir nin ktk maisha yako?

Ama akiwa sio mtumiaji wa madawa kunakunufaisha nin ktk maisha yako.?

Yaani mtu unaamka asubuh asubuh na kushusha kitabu kizima cha maneno kwa kumpangia mtu maisha ya kuishi.

Itoshe kusema kama hakuna lote unalofaidika nalo ungeacha kufatilia maisha ya watu.
Wacha ujuaji na upuuzi dogo. Nyie ndio mashoga na hamtaki muanbiwe eti mku..... ni wako. Pumbavu kabisa wewe.
 
Back
Top Bottom