Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto na Nandy wahojiwa na Polisi kwa kusambaza video za faragha, wapewa dhamana...

Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto na Nandy wahojiwa na Polisi kwa kusambaza video za faragha, wapewa dhamana...

Safi sana. Anayesema serekali isifuatile haya mambo, nende twitter ujione wakenya walivyo choka ambapo serekali haikufuatilia maneno kama haya. Wiki iliyopita, Wakenya online wamezindua kampeni ya kuwaaibisha vijana wadogo ambao wanatoa picha na video chafu kwenye mitandao. Lengo ni kuzisambaza picha hizo sana mitandaoni hadi ziwafikie wazazi, walezi au jamaa ya vijana hao. Hash tag yenyewe ni [HASHTAG]#ifikiewazazi[/HASHTAG]
 
Wakuuu nimesikia kuwa diamond na nandy watapelekwa mahakani Kwa kosa la maadili OK nandy najua ni kufanya ngono kinyume na maumbile tena hadharani Lakini hiii Ya diamond sijainyaka naomba kujulishwa huyu Kijana diamond kafanyaje tena?
Hahah kinyume na maumbile? Uliona wapi mkuu?
 
Mawaziri hizi nguvu zihamishieni kwenye kuzisaka zile 1.5 Trillion maana aya mengine hata balozi wa Madale anaweza kukomaa nae,serikali inahamisha magoli.
 
unawezaje kumkamata mtu ambaye ana sauti kuliko wewe mwenye zamana... ana bishana na mawaziri kila leo... ana tokelezea ktk mikutano ya uzinduzi ya mh. yupo pamoja na DAB... una wezaje kumkamata huyo mtu kirahisi... kama sio kamchezo furani ni nini


Masikio hayazidi kichwa, Dogo asidanganyike na sifa za mitaani.
 
Haha Diamond na hao wengine hawana makosa... kwani video zilikuwa kwenye account zao?

Waliozisambaza ndio washughulikiwe...

Halafu kwa diamond ndio kabisa wanamaliza rasilimali za serikali maana hamna kosa pale
 
fact mkuu huwezi kulandana mama yako unamheshimu halafu kila siku upo na wanawake tu labda kama yule mama yake ni wa bandia ila kwa kimaadili mond anachofanya ni ujinga kama ni pesa karuhusu zimvue utu wake
mama yk.mwenyewe ana miliki kiben 10.. tena anaambatana nae na mond akiwemo..utawaambia nn...
 
Wasanii watatu Billinas, Nandy, Diamond na Mwanadada ambaye ni Mwanamitindo Hamisa Mobeto wameachiwa Kwa dhamana baada ya kushikiliwa na polisi Kwa kosa la kusambaza video zisiokuwa na maadili zikiwaonesha wako Faragha.

Pia wametakiwa kureport tena polisi siku ya ijumaa.....

Kuna habari pia kuwa Hamisa ana mpango wa kumfungulia case Diamond kwa kumdhalilisha na kuweka video kwenye mitandao na yeye haikuwa ridhaa yake bali ali lazimishwa kurekodiwa..

wasalaam
Mange anazidi kupotezwa na ile kitu uake ya 26/4 hahahaha muvi nyingine za kidwanzi sana
 
Mwakyembe amesema kuna baadhi ya wasanii ambao walianza kufanya uhuni ndani ya mitandao akiwemo mwanamuziki nyota wa muziki, Diamond ambae tayari amekamatwa na Jeshi la Polisi na anahojiwa kutokana na picha alizozungusha.

Pia Mwakyembe amesema pia imebidi binti Nandy naye akamatwe kisha kuhojiwa na wanaangalia namna ya kuwapeleka mahakamani.

Mwakyembe ametoa wito kwa vijana kuwa mitandao sio kokoro la kupeleka uchafu wote ambao umezuiwa na sheria zingine na nchi ina utamaduni wake ambapo inahitajika kulindwa kizazi cha sasa na cha kesho cha Taifa hili.

Akiuliza swali, mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga alitaka kujua kauli ya Serikali juu kukithiri kwa ushoga na kutukana matusi mithili ya bomu la nyuklia ambayo sio maadili ya mtanzania na team za matusi ikiwemo za Wema, Zari, Diamond na Shilole.

Mwakyembe amesema sheria ya EPOCA ilitungwa mwaka 2010 lakini zilikosekana kanuni za kubana maudhui hasa upande wa mitandao. Amesema kanuni zimeshatungwa na zimeanza kufanya kazi.


Aliyeandika hii Script nampa vyeo sana...
 
Back
Top Bottom