Diamond Platnumz hili la kumfananisha demu (msichana) wako na Yesu (Mungu) utuombe radhi wakristo na utubu au wimbo wake ufungiwe na BASATA

Diamond Platnumz hili la kumfananisha demu (msichana) wako na Yesu (Mungu) utuombe radhi wakristo na utubu au wimbo wake ufungiwe na BASATA

Maishà n magumu jaman,mpaka wakina gwajima wanataka kwenda bungeni,huo muda wakupgania dini za wazungu mnautoa wap
Sasa hayo maisha magumu si yako...sisi hayatuhusu na wala Hatufanani maisha bro wewe endelea kupambana na hali yako
 
Yesu alikuwa mwizi wa mbao tu, au wewe haujapata hiyo stori?
Mathayo 12
31 Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.
 
Lakini pia si watu wameona alipoishia. Kanye West aliwahi kujifananisha na Messiah sikuhizi akili zake hazijamkaa sawa. Sasa kama watu wanadhani Mungu anataniwa waendelee na mavuno tutayashuhudia hapahapa.
Unaongea kishabiki, kangi alikemewa kwa maneno yake embu uwe mtu wa kuchunguza ndio unaongea sio unaropoka tu
 
Wakristo bana.
Eti 'Yesu' ni 'Mungu' 😂 😂 😂😂😂
 
Mtoa mada kaingiza Ukristo na Uislamu wachangiaji nao wanaingiza Ukristo na Uislamu

Mada ingebaki tu kuwa diamond kakufuru tu basi lakini siyo kusema je mwingine angefanya... kisha amtaje Muhammad au Allah; yaani kana kwamba diamond kafanya hivyo kwakuwa yeye mwislamu (kwahiyo ameamua kuutweza Ukristo)

Sivyo hivyo; Diamond huyo mnaemchukulia kama Mwislamu hajaanza leo kufuru zake hizo tena siyo kwa kuegemea upande mmoja/fulani wa dini tu bali kwa yeyote anayeamini kuna Mola angekubali tu kuwa Diamond ni kafiri

Tukirudi kwenye Ukristo na Uislamu; ni haramu kumfananisha Mola na mtu au Kiumbe mwingine kwa namna yoyote ile (iwe tashibiha, sitiari, lakabu, mubalagha au mbinu nyingine yoyote ya kisanaa)

Kwahiyo hata mleta mada unapotuambia Diamond kakufuru kwa kumfananisha Demu wake na Yesu tena unarefusha kwa kusema yesu ndo Mungu bado hujatutetea sisi Wa-Kristo tunaoamini Yesu siye Mungu

Tanbihi;
Haya mambo ya burudani yana mipaka yake na ndomaana watu wa dini wanazuia baadhi ya burudani kwakuwa zote hizo ndo zinapelekea watu kukufuru kama sio kukufurishwa mfano mziki na vyenye kuambatana nao
 
Wakristo bana.
Eti 'Yesu' ni 'Mungu' [emoji23] [emoji23] [emoji23][emoji23][emoji23]
Yesu ni zaidi ya mtu wa kawaida na ni zaidi pia ya malaika hata kama alifanya kazi za kitume na kinabii kwa kuwa katika Qur'an anaelezwa kuwa ni roho ya Mungu na ni neno la Mungu. Na alikuja ili kufanyika ishara kwa binadamu.
 
Yesu ni zaidi ya mtu wa kawaida na ni zaidi pia ya malaika hata kama alifanya kazi za kitume na kinabii kwa kuwa katika Qur'an anaelezwa kuwa ni roho ya Mungu na ni neno la Mungu. Na alikuja ili kufanyika ishara kwa binadamu.

Kwahiyo 'Yesu' ni 'Mungu'?
 
Sasa hayo maisha magumu si yako...sisi hayatuhusu na wala Hatufanani maisha bro wewe endelea kupambana na hali yako
Acheni ushamba kupigania mambo ambayo hamjui yalianzia wap,acha kuwaibia waafrika wenzio sadaka
 
Hapa mnapiga kelele lakin unamkuta mtu huyo huyo anaimba "Malaika nakupenda Malaika...Malaika ningekuoa Malaika"...pumbqvu unamfananisha Mwanamke na Malaika!...hapo mpo kimya!wacheni unafiki nakujifanya wajauaji Sana...wewe jua hukuelewa kilichoimbwa na usitake kupotosha watu!
 
Yesu (Nabii Issa) sio Mungu

Kama ni kweli kakosea ila na wewe umekosea kumpa yesu cheo cha Mungu
 
Nimeusikiliza wimbo mpya wa Diamond Platnumz uitwao ongeza kiukweli anatakiwa atafute mhariri wa mashairi na mistari yake. Kwenye ngoma ya ongeza anasema "we ndo wangu yesu mkombozi sa mbona unaniacha mwenyewe" anamuongelea mwanamke/ msichana/demu wake.

Kwa hili Diamond hapana umeenda mbali mno na umetukosea Wakristo. Hivi mkristo aimbe wimbo amljnganishe demu wake na Mtume Mohammad au Allah atakuwa sawa?

Kwetu Wakristo Yesu ni Mungu kweli, mtu kweli Yohana Mtakatifu 1:1-10. Yesu ni Mungu mwana katika nafsi tatu za Mungu zinazofanya Utatu Mtakatifu.

Yesu aliacha kiti chake cha nzi kule mbinguni akauvaa mwili akashuka duniani ili atufie na kutukomboa sisi na dhambi zetu. Alisulubiwa akafa, akazikwa siku ya tatu akafufuka na sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba na hapa tulipo tunasubiri arudi aje awahukumu walio hai na wafu. Maana ameahidi anakwenda kwa Baba kutuandalia makao na atakuja kutuchukua ili alipo nasi tuwepo. Je ni Yesu huyu wa kumlinganisha na demu wake kweli Diamond Platnumz?

Yesu huyu ambaye alikuwepo kabla ya ulimwengu kuumbwa ambaye maandiko yanasema vitu vyote viliumbwa kwa jina lake na pasipo yeye hakuna kilichoumbwa? Huyu ndiyo wa kumlinganisha na demu.


Ni kweli sanaa inahitaji ubunifu lakini siyo kwa kiwango hiki Diamond aombe radhi kwa kweli au wimbo wake ufungiwe na BASATA.
Hata kwa dini ya kiislamu ni kufuru kubwa kumlinganisha yesu na mpenzi wa mtu
 
Back
Top Bottom