Diamond Platnumz hili la kumfananisha demu (msichana) wako na Yesu (Mungu) utuombe radhi wakristo na utubu au wimbo wake ufungiwe na BASATA

Sawaaaa...lakini

Hivi kweli Mungu anasifa ya kufa...tena siku tatu jamani jamani duuuh
 
Kwenye Ukristo hakuna binadami mwenye hadhi sawa na Yesu, mwambieni amfananishe demu wake na mtume wake.
 
Tumpende tu kwani wangekuwa wenzetu wangemkata kichwa.
Tujitofautishe na hao wanyama
 
Hoja umenielewa? Jikite kwenye hoja, achana na hayo marufuku ya mapepo
 
Anzisha mada mkuu, inaonekana unatumiwa vema na mapepo. Fungua thread tukuchomoe hayo majini
 
Kama hupendi usisikilize na usinunue muziki wake.

Kwa watu wengine Yesu ni Mwanafalsafa tu.
Hao ni wengine kama ulivyosema, hapa hoja haihusu watu wengine, vinginevyo Domo angehesabiwa kuwa yuko sawa. Ukiwa mtu mwingine usiingie kwenye huu uzi
 
Ingekuwa upande wa pili Fatwa ingemhusu.

Kama Mark Basseley Youseff wa Innocence of Muslims au kilichowapata akina Charlie Hebdo.
Sema ingekuwa upande wake "domo mwenyewe." Hii sio bahati mbaya, ni kusudi kabisa
 
Hao ni wengine kama ulivyosema, hapa hoja haihusu watu wengine, vinginevyo Domo angehesabiwa kuwa yuko sawa. Ukiwa mtu mwingine usiingie kwenye huu uzi
Unaingilia uhuru wa kikatiba wa watu kujieleza.

Ukishaweka uzi JF, mwanachama yeyote anaweza kuchangia.

Hivyo usiniwekee mipaka kwenye kuchangia.

Zaidi, mipaka yako ni ya kijinga.Kwa sababu huna uwezo wa kunizuia kuchangia. Unaweka sheria ya kijinga usiyoweza kui enforce.

Ujinga juu ya ujinga!

Kama unataka mazungumzo ya faragha, nisichangue, tuma PM kwa rafiki zako unaotaka kujadikiana nao.

Inaonekana huelewi hata maana ya Public Forum na Freedom of Speech.

Ndiyo maana huwezi kunielewa nikikwambia Domo ametumia haki yake ya kikatiba tu.

Kama hupendi alivyofanya unaruhusiwa kususia kusikiliza nyimbo zake.

Hiyo pia ni haki yako ya kikatiba.
 
Amtumumie Mwanafalsafa wa dini yake.
Inawezekana katika dini yake Yesu ni Mwanafalsafa.

Sasa usimzuie kumtumia mwanafalsafa wa dini yake.

Yesu ana maana tofauti kwa watu tofauti.

Wengine wanamuona Masiha mwana wa Mungu.

Wayahudi wenyewe waliomuona tangu anazaliwa wamemkataa, wamesema huyu si Masiha. Ni Rabbi tu, Mwalimu tu wa kawaida. Si mwana wa Mungu.

Wewe Mndengereko umemjua jana Yesu, kwa kuletewa dini na wakoloni, waliokuja kukunyanyasa na kukufanya mtumwa, unataka kujifanya unamjua Yesu kuliko wenyewe Wayahudi?

Wengine wanamuona mtume.

Wengine wanamuona mwanafalsafa.

Wengine wanamuona tapeli.

Wengine wanamuona kichaa.

Sasa, usilazimishe unavyomuona wewe, kika mtu amuone hivyo.

Na mimi sitaki kulazimisha ninavyomuona mimi umuone wewe.
 
Povu la nini? Imesema mwenyewe WATU WENGINE waanaamini hicho ukitakacho. Sasa huu uzi haujagusia watu wengine, umeongelea kuhusu wenye imani ya Mungu wa kweli. Kumbe kuja humu na hoja za watu wengine ni kudhihirisha ujinga wako, bali mimi sina uwezo wa kukuzuia usichangie mada. Waweza changia vyovyote vile utakavyo, lakini yatakuwa mawazo ya WATU WENGINE!!
 
Kwani Yesu Kristo alikuja kwa ajili ya kila mtu?
 
Kwann asingeimba mtume muhammad bu anawajua Muslims hawapend ujinga ila wakrsto wastaarabu maskini ya Mungu
 
Waweza kuta mleta mada ni babu tale kakaa pembini anaaNgalia mnavyohangaika na dini vs diamond...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…