Diamond Platnumz hili la kumfananisha demu (msichana) wako na Yesu (Mungu) utuombe radhi wakristo na utubu au wimbo wake ufungiwe na BASATA

Diamond Platnumz hili la kumfananisha demu (msichana) wako na Yesu (Mungu) utuombe radhi wakristo na utubu au wimbo wake ufungiwe na BASATA

Mimi mbona wala sioni tatizo, anadhihirisha tu kwamba Ukristo ni dini ya amani upendo na uvumilivu, ndio maana pia utamsikia anaimba haleluya, au hata kuonekana amevaa msalaba n.k.

Ni wazi kuwa anatambua taabu au ghadhabu anazoweza kukumbana nazo iwapo atakuwa akiwataja hovyo MITUME, MANABII na VIONGOZI wa imani yake mwenyewe.

Dini ni kuelimisha na kuelekeza Mtu namna sahihi ya kufanya jambo ambalo unadhani amekosea na sio ghadhabu maana wa kuhukumu yupo.
 
Nimeusikiliza wimbo mpya wa Diamond Platnumz uitwao ongeza kiukweli anatakiwa atafute mhariri wa mashairi na mistari yake. Kwenye ngoma ya ongeza anasema "we ndo wangu yesu mkombozi sa mbona unaniacha mwenyewe" anamuongelea mwanamke/ msichana/demu wake.

Kwa hili Diamond hapana umeenda mbali mno na umetukosea Wakristo. Hivi mkristo aimbe wimbo amljnganishe demu wake na Mtume Mohammad au Allah atakuwa sawa?

Kwetu Wakristo Yesu ni Mungu kweli, mtu kweli Yohana Mtakatifu 1:1-10. Yesu ni Mungu mwana katika nafsi tatu za Mungu zinazofanya Utatu Mtakatifu.

Yesu aliacha kiti chake cha nzi kule mbinguni akauvaa mwili akashuka duniani ili atufie na kutukomboa sisi na dhambi zetu. Alisulubiwa akafa, akazikwa siku ya tatu akafufuka na sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba na hapa tulipo tunasubiri arudi aje awahukumu walio hai na wafu. Maana ameahidi anakwenda kwa Baba kutuandalia makao na atakuja kutuchukua ili alipo nasi tuwepo. Je ni Yesu huyu wa kumlinganisha na demu wake kweli Diamond Platnumz?

Yesu huyu ambaye alikuwepo kabla ya ulimwengu kuumbwa ambaye maandiko yanasema vitu vyote viliumbwa kwa jina lake na pasipo yeye hakuna kilichoumbwa? Huyu ndiyo wa kumlinganisha na demu.


Ni kweli sanaa inahitaji ubunifu lakini siyo kwa kiwango hiki Diamond aombe radhi kwa kweli au wimbo wake ufungiwe na BASATA.
Kama hupendi usisikilize na usinunue muziki wake.

Kwa watu wengine Yesu ni Mwanafalsafa tu.
 
Marko 16:19
Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kulia wa Mungu.

Kuhusu Yesu kuwa au kutokuwa Mungu....tujue tu ya kuwa Biblia ni mkusanyiko wa maandiko/vitabu vingi...hivyo inahitaji kukutana na aya kadha wa kadha kabla kujiridhisha na kile unachotaka kuamini.
 
Nimeonja Utamu Wa Yesu
Ya Rose Muhando imekubaliwa na Wakristo kisa ni msanii wa Injili
Ila hii ya Leo imekataliwa na wakristo kisa ni Diamond

Mungu yuko wapi ya Ney imekubaliwa sikuona aliyeibuka kuipinga wala kusema haitakiwi
Ma Niggas huwa wanaimba nyimbo za kukejeli kule Marekani na za kuhusisha Freemasons kuipinga Imani ya Kristo hamkuibuka kupinga.

Wakati fulani niliwahi kumtongoza msichana akaniambia sikati kuolewa mwanaume pekee na rafiki yangu ni Yesu tu

Acha Nikae Kimya[emoji850][emoji850]
 
Shida ya kuanzisha na kuchangia uzi kwa kukurupuka ndio hizi na wachangiaji wengi naona mmesapoti bila kufuatilia. Diamond amesema

" .... wewe ndio wangu yesu mkombozi sa mbona petro unaniacha mwenyewe..."

Naona umetoa neno petro ili kuhalalisha ulivyo elewa wewe. Hapo kalinganisha kitendo cha yeye kuachwa sawa na petro alivyo muacha yesu. Sijaona kosa mimi hapo zaidi tu niseme kwamba jamaa ni mbunifu.
 
Katika Uislam kuna nguzo za Imani ni sita ikiwemo kuamini Vitab na MItume yke......ambavo vitabu vya Mungu ikiwemo Injil na ktk mitume akiwemo Yesu (kwa kiarab ISSA) ukileta mambo ya dini kwenye suala la mziki itabidi lijibiwe kidini. Kwa muktadha huo hata yeye Diamond anamuhusu huyo Yesu otherwise iwe kuna jengine lipo kwa mleta mada.
 
Wakristo wenyewe wameshajidharau na kumfanya Yesu wao adharaulike. Ndio maana Diamond anaweza kutunga mashairi ya kumkejeli Yesu. Tena Diamond ameiga tu, aliyeanza kutoa hizo dharau ni Kangi Lugola alipomfananisha Magufuli na Yesu, na viongozi wakubwa wa dini ya kikristo wakakaa kimya huku wakimshangilia Magufuli na kumsifia ovyo ovyo. Sasa tuwaache wakristo wavune walichopanda. Yote haya ni mafanikio ya uongozi wa awamu ya tano!

Heshima ya Yesu italetwa na wale wanaomwamini, na itapotezwa na hao hao wanaomwamini.

CCM oyeee!
Magufuli oyeee!
Diamond oyeee!
 
Kuna kina Yesu/Jesus zaidi milioni duniani kote. Halafu sisi wakristo ni waelewa tofauti na wenzetu wa upande wa pili, labda Kama wewe NI msabato. By the way Yesu wetu sisi anajulikana Kama Yesu Mnazereti wa ukoo wa Daudi. Diamond kamtaja huyo?
 
Dini iheshimiwe diamond kakosea


Waafrika mna kwere na hizi dini zilizoletwa kuliko hao wazungu waliokudanganyeni. Ariana Grande kaimba God is a woman, yaani ingekuwa Afrika angekosewa radhi na babaake. Waafrika wenzangu mnanitia aibu sana nyinyi
 
Wakristo sie wapole sana ingekua waislamu muda huu kijana angekua keshaharibiwa sura na vitisho kibao vya kusomewa albadir.

Domo mpuuzi halafu mdini balaa hapo ndipo kaonyesha rangi yake halisi.
Sio mara ya Kwanza hata kwenye Ile video ya Nana ukiangalia vzr anaikashifu ukristo. Sema amekuta huku tu wa pole ndo. Maana wa nafanya watakalo.
 
Back
Top Bottom