Diamond Platnumz Kufikishwa Mahakamani

Diamond Platnumz Kufikishwa Mahakamani

tamko lao lililenga kuonya jamii kuwa ni kinyume cha sheria kukutwa au kuvaa sare za jeshi. Ishu kama ni zenyewe au zinafanana ni suala la kisheria zaidi kama ulivyohoji, ila cha moto unakuwa umeishakipata tayari - usumbufu wa hapa na pale, psychological torture etc

Ndo ujue kuna kitu kinaitwa malicious prosecution, wrongful arrest etc etc kina deal na hizo psychological torture etc
 
Utakuta Amiri jeshi ndio katoa ruhusa ya jamaa kuvaa hizo sare.Si unajua amiri jeshi ndio rafiki yao hao wasanii.
 
Hii sasa ni double standard,mbona mh. Mwigullu Nchemba anavaa kofia ya jeshi la China na hajachukuliwa hatua yoyote?hili ni jeshi letu wananchi na huyo Diamond ana mchango wa kodi inayowapa hao wanajeshi mshahara.
 
Diamond alikuwa na kibali cha kutumia nguo za jeshi la wananchi kwenye show yake na alipewa toka alhamisi!
 
ha ha ha ha "mwana daresalama" umepanic.

We ndo umepanikishwa na kiba inaonyesha cna team ushuzi kama za kwenu zinazowanyima usingizi bosi wako domo kafulia ajipange na.mtajutra mwaka huyo kiba atawanyima sana usingizi
 
We ndo umepanikishwa na kiba inaonyesha cna team ushuzi kama za kwenu zinazowanyima usingizi bosi wako domo kafulia ajipange na.mtajutra mwaka huyo kiba atawanyima sana usingizi

Inaonyesha una akili za kitoto sana kila mada una kimbilia ubishani wa kiba na domo ha ha ha ha,too childish for me to discuss mada za kipuuzi kama hizo,nyie first year mna shida sana.
 
ww akili yako cio nzuri soma hiyo sheria hapo juu vizuri. vazi liwe au lisiwe la JWTZ ila lina mfanano wowote tayari ni kosa. we kawe wakili mirembe.

Ushaambiwa sio sheria ni tamko..mtu anahukumiwa kwa sheria sio tamko ila kwasababu ni layman inabidi nikuelewe tu
 
Inaonyesha una akili za kitoto sana kila mada una kimbilia ubishani wa kiba na domo ha ha ha ha,too childish for me to discuss mada za kipuuzi kama hizo,nyie first year mna shida sana.

We ndo mwenye akili za kitoto unaye bishana na mtoto mwenako upo hapo dume zima wivu na hyo team domo itakuua kumbe unafatilia comment zangu good for me it seems huna cha kufanya hadi unafatilia kiba na daimond eeh usilo lijua ni sawa na ucku wa giza na huo unjuka wako wako wa kufikiria first i feel sory for u unaye discus topic za kitoto kama sio juha nini naona fiesta ili kuumiza sana jinyonge basi mumeumbuka nyooooooooo shame on you and mind ua own fuc...business
 
We ndo mwenye akili za kitoto unaye bishana na mtoto mwenako upo hapo dume zima wivu na hyo team domo itakuua kumbe unafatilia comment zangu good for me it seems huna cha kufanya hadi unafatilia kiba na daimond eeh usilo lijua ni sawa na ucku wa giza na huo unjuka wako wako wa kufikiria first i feel sory for u unaye discus topic za kitoto kama sio juha nini naona fiesta ili kuumiza sana jinyonge basi mumeumbuka nyooooooooo shame on you and mind ua own fuc...business

Unaoneka ni fundi sana wa maneno ila kichwani ni box,fun enough ni jinsi unavyo komalia domo na kiba as if u r a f@kin street whor.e who is stressed na some kind of........afterall ni ustupi.d kubishana na mgonjwa kama wewe,una jiita beyonce kumbe ni kichaa wa vingunguti......soma mama wazazi wana kutegemea.HAYA UMESHINDA.jioni njema.
 
diamond3-300x171.jpg


MSANII nyota wa muziki wa Bongo Flava nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ huenda akaingia matatani baada ya juzi kupanda jukwaani kutumbuiza katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 akiwa amevaa sare ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kinyume cha sheria.

Tangu msanii huyo afanye hivyo, mjadala umeibuka kwa wengi wao kujiuliza nini maana yake na kama alifanya hivyo kwa kibali maalumu au la, hasa ikizingatiwa ni hivi karibuni Jeshi hilo lilitoa onyo kwa wasanii na wengineo kutotumia mavazi hayo.

Mbali ya Diamond, hata vijana wake nao walishambulia jukwaa wakiwa katika mavazi hayo, akiwemo msanii aliyemshirikisha katika moja ya nyimbo zake, Ney wa Mitego.

Wakati shoo hiyo ikiendelea, baadhi ya mashabiki walianza kumzomea kila alipoimba kabla ya video kubwa ambazo zilikuwa mbele ya jukwaa hilo kuanza kuonyesha picha za mnato na video za mwanamuziki huyo akiwa amevaa mavazi hayo huku akiwa kama askari ‘anayekoki’ risasi katika katika bastora na baadaye katika bunduki ya kivita.

Kitendo hicho, kilionekama kuwakera zaidi maelfu ya wapenzi na mashabiki wa muziki waliokuwa wamejazana katika viwanja vya Leaders Club, huku kila mmoja akiwa na tafsiri yake.

Baada ya tukio hilo la juzi usiku, kitendo cha nyota huyo kuvalia mavazi hayo ya JWTZ, kimeibua mjadala hadi katika mitandao ya kijamii kuanzia jana asubuhi, ambapo picha za msanii huyo zikitumika kujenga hoja ya uhalali wa kufanya hivyo, huku vijana kadhaa wanaokutwa nazo mitaani wakiteswa vibaya na jeshi hilo.

Kwa upande wake Diamond, alitoa taarifa ndefu katika ukurasa wake wa Facebook na Instagram, akiishia kuelezea ni kwa nini alizomewa katika shoo hiyo.

Tanzania Daima ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura juu ya kitendo cha msanii huyo, alisema alikuwa hajui chochote na kuahidi kulifanyia kazi kama atapelekewa taarifa na wasaidizi wake.

Alipotafutwa Kaimu Msemaji wa JWTZ, Meja Joseph Msanja, simu yake iliita bila kupokelewa na alipotafutwa msaidizi wake, alikiri kupata taarifa na kujionea kupitia shoo hiyo, huku akisisitiza bosi wake anaweza kulizungumzia hilo.

Tukio hilo limefanyika ikiwa ni siku chache tu tangu kijana mmoja aliyekuwa amevalia mavazi ya kijeshi maeneo ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam, kuvuliwa na kupewa adhabu ya kuogelea katika dimbwi la maji machafu yaliyotuama.

Aidha, msanii Gwamaka Kaihula ‘Crazy GK’ aliwahi kuhojiwa na Jeshi hilo kwa kutumia mavazi ya kijeshi katika kibao chake cha Simba wa Afrika, ambapo alijitetea pamoja na kuomba msamaha kwa kilichofanyika.

Kutokana na wimbi la watu mbalimbali hasa wasanii kuvalia mavazi yanayofanana na sare za jeshi hilo, hivi karibuni Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya JWTZ, ilionya kama ifuatavyo:

“Kumejitokeza kama fasheni kwa baadhi ya wasanii, hasa wanamuziki wa Bongo fleva, kurekodi video zao wakiwa wamevaa sare za jeshi kama vile suruali, viatu, fulana, kaptula, mabegi au kofia.

“Inawezekana kwa namna moja ama nyingine, baadhi ya watumiaji wa sare hizo hawafahamu ni kinyume cha sheria ya nchi kukutwa nazo, ingawa kutokujua sheria bado sio utetezi mbele ya mahakama.

“Mtu yeyote yule asiye na ruhusa ya kushona, kuuza au kuingiza nchini sare za jeshi, atakuwa ametenda kosa, kwa hiyo atafikishwa mahakamani na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.

“Katika uvaaji au uingizaji nguo, kama itatokea kwamba nguo hizo zinafanana kwa aina yoyote ile na zile za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, ikadhaniwa kuwa ni hizo, mtu huyo ana hatia na anastahili kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria zinazohusu sare za majeshi zilizopo,” ilifafanua taarifa hiyo.

Chanzo:Tanzania Daima


Mwandishi huyu n kanjanja,kwanza GK hakuvaaa mabaka kwenye video ya simba wa africa ilikuwa n wimbo wa Ama zangu Ama zao hlo mosi,pili hii habar imekaaa kimagendo magendo kumchafua icon wa tz tu bt hata angevaa nn Diamond atabak kuwa Diamond na ukitaka jua kama n Msanii nyota na icon wa nchi siku akupanda mahakaman na kuhukumiwa kwa kosa hilo njoo hapa nkupe salio la 50K...
TeamGoodmusic.....
Hatemajungu na wivu
 
Back
Top Bottom