Al-shabaab
JF-Expert Member
- Aug 24, 2013
- 1,791
- 619
Get ready, on Friday dis week mkali wenu wa Afro pop anadondosha new hit song.
Chanzo: Diamond Platnumz Twiter A/C
...Updates...
Wimbo tayari umetoka.
Chanzo: Diamond Platnumz Twiter A/C
...Updates...
Wimbo tayari umetoka.
Mambo 10 kutoka kwenye wimbo UTANIPENDA
1. Ni simulizi iliyobeba hofu ya watu wengi. Nisipokuwa na mali, nisipokuwa na kazi, nikipigika mtaendelea kunipenda, kunisifia, na kuwa karibu yangu kama sasa?
2. Imejitosheleza kimaishari. Mashairi yameshiba na ya kina tofauti na nyimbo nyingi za aina hiyo zenye mashairi ya kujirudia sana
3. Video na wimbo vimechukua uhalisia zaidi wa maisha yake kwa kuwatumia watu wake muhimu maishani wakiwemo mama yake Sandra, mchumba wake Zari, mwanae Tiffah, mameneja wake na wengine
4. Ni Bongo Flava halisi (yenye vionjo vya pwani) ambayo kwa ukubwa wake inakuwa na maana zaidi kwa sasa kufanya nyimbo za aina hiyo ili kuitangaza kimataifa kutokana na ukubwa wake Afrika na duniani kwa ujumla.
5. Wimbo umetumia asilimia 100% Kiswahili. Hii inawafanya wengi wasioelewa Kiswahili kuhangaika kukijua walau kidogo na matokeo yake ni kuwa lugha inasambaa zaidi
6. Imeleta utamu wa kutumia mastaa wengine wa kibongo kwenye video kubwa (cameos). Ndani wameonekana mastaa kama Mwana FA, Shaa, Chege, Master Jay, Harmonize, Wolper
7. Kawakumbuka mashabiki wake waliokuwa wakijitokeza uwanja wa ndege kumpokea kutoka kwenye tuzo
8. Unaweza kuingia mkwanja kwenye video yako pia. Dr Mwaka na kliniki yake imepunguza gharama alizotumia kumlipa Godfather
9. Unaweza kumtumia ex wako pia kama video queen.. no hard feelings!! Vipi kuhusu Sepetunga lakini?
10. It?s a brilliant video and a masterpiece!!
Last edited by a moderator: