Diamond Platnumz: Niliibiwa Tsh. Bilioni 4 niliyotaka kununulia ndege

Diamond Platnumz: Niliibiwa Tsh. Bilioni 4 niliyotaka kununulia ndege

Sidhani. Mimi nililipa sh. 45m NMB adv ya kupata gari kutoka ughaibuni mwaka jana hadi leo sijapata. Mhusika alishahama Tanzania na kampuni yake haipo tena nchini. Anaishi lndia karibu na wachina huko. Bado nahangaika kurejesha hiyo pesa.
Matapeli wapo
Lakini issue ya ndege mi najua unaagizia oda moja kwa moja kiwandani ,. Au kuna ndege za mtumba?
 
Ali'clarify' kuhusu kupata verses za 2Pac ambazo mpaka sasa zinamilikiwa na InterScope, alisema kama una pesa unanunua zile verse ambazo hazikuwahi kuwa released na kama kuna audio zilizorekodiwa ambazo zina verses/chorus unazinunua and then that's a collaboration.
Bullshit.
 
Aweke izo document alizofanyia malipo. Tumechoka na uongo wa wasanii.
 
Kama hii stori Ina ukweli basi mjini ni kiboko.

Imagine Diamond anatapeliwa Hadi kwenda kulilia Polisi, wewe mwenzangu utasalimika?

Ongezeni nyama basi maana naona kama sioni hivi, inaweza kuwa kamba maana Ukisikia mtu anaitwa msanii hapa Bongo ujue ni mpiga kamba 😆😆

=======

Baada ya kutua Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga leo Oktoba 29, staa wa bongoflava Diamond Platnumz amefunguka kuhusu ishu ya ndege yake binafsi (private jet) aliyotaka kununua.

"Ishu ya ndege yangu ina mambo kidogo, nilinunua jet nimelipa fedha nimetapeliwa, nilimpigia Waziri Mbarawa (Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa) alinisaidia, kaka yangu Hamza ( Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari) alinisaidia na sasa serikali nzima inanisaidia kupata haki yangu, nililipa fedha nyingi, kianzio zaidi ya bilioni ila niliowawatumia wananiletea ujanja ujanja," amesema Diamond Platnumz

Diamond amekuwa akitumia ndege binafsi katika safari zake za ndani na nje ya nchi.

Chanzo: Mwanaspoti
View attachment 2797713
Alikua na madalali wa kinaijeria huyu bila shaka...
 
Well kwa exposure aliyonayo na connections za hawa mawaziri na TCAA basi katapeliwa kizembe
 
Sidhani. Mimi nililipa sh. 45m NMB adv ya kupata gari kutoka ughaibuni mwaka jana hadi leo sijapata. Mhusika alishahama Tanzania na kampuni yake haipo tena nchini. Anaishi lndia karibu na wachina huko. Bado nahangaika kurejesha hiyo pesa.
Matapeli wapo
Mpaka Sasa wamefika wangapi PM mwanangu?
 
Mkuu mtu ana utajiri wa zaidi ya B 20 yan hiyo B 4 imsumbue kununua jet yake?
Mkuu utajiri na pesa cash mkononi ni vitu viwili tofauti. Mtu anaweza kuwa na utajiri labda wa milioni 100 ila cash akawa nayo Laki 2 tu.... kuna watu wangapi mijengo yao inauzwa na benki kisa wameshindwa kulipa marejesho hata robo ya utajiri hayajafika?
 
Kwa sasa tukae kimya tusubiri wale waliojiajiri kufuatilia maisha binafsi ya watu maarufu watuletee habari kamili. Ninamshauri komredi Simba atulie na kusubiri show za kampeni apige hela.
 
Back
Top Bottom