Kuwa tajiri siyo kigezo cha kutoa pesa kirahisi kama unajiona wewe ukishika elfu 50 huoni ugumu kutoa elf 6 basi ujue we bado ni masikini usie na mipango yoyote
Tajiri mzoefu jinsi anavyozidi kupata pesa ndo jinsi anazidi kuwa mgumu maana mipango nayo inaongezeka kwahiyo usishangae kuona anaitisha press kwasababu ya million 200 hiyo ni pesa nyingi
Kuna tajiri mmoja miaka ya nyuma alikua anamiliki mabus flan hivi ila kila siku alikua anasoma mita ya maji ya nyumban kwake na kuandika sehemu baada ya kugundua anabambikiwa bill ya maji kisa tu wamemuona ni tajiri, kwahiyo usishangae jinsi unavyozidi kuwa na pesa ndo jinsi ugumu unaongezeka