Diamond Platnumz, Rayvanny na Zuchu wamependekezwa kuwania tuzo za Grammy 2021

Diamond Platnumz, Rayvanny na Zuchu wamependekezwa kuwania tuzo za Grammy 2021

Kigoma Independent hii habari Ni nzuri Sana na Ni kubwa Sana kwenye industry yetu ya mziki ukutakiwa uwasilishe kwa huo mtindo huo wa mipasho hakukua na sababu ya kufanya hivyo mzee next time jifunze kuandika Uzi bila mipasho au usingeandika kabisa watu wastaharabu wangeandika Hilo ndio uliokosea mzee
Habari ya uongo achana na huyu kima
 
Wakuu naomba mwenye uelewa wa jinsi ya ku vote kwenye grammy consideration anielekeze please,I want to vote down Zuchu for good.
 
Inakubidi ufahamu hakuna kitu kibaya kama itikadi. Siasa ni itikadi. Athari nyingi na maafa mengi binadamu kwa binadamu moja miongoni mwa kisababishi ni itikadi ya mlengo wowote ambao wao wanaouamini.

CCM na Upinzani ni vyama vyenye watu wenye itikadi zao. Itikadi inajikita kwenye mizizi ya moyo kabisa!

Msanii kwa sanaa yake anakuwa kiunganishi cha watu wenye itikadi tofauti kuwa wamoja na ni kwa burudani tu. Atakapoanza kuonyesha itikadi yake siyo kosa! Kosa ni pale unaporusha vijembe na kebehi kwa itikadi nyengine ambayo hiyo itikadi imekusanya miongoni mwa ujumla wa mashabiki wako.

Unachotegemea ni nini? Watakuasi tu! Umeitusi au kuikebehi itakadi yao ya Uchama ambayo imejikita kwenye moyo halafu unakuja kwa nembo ya Utaifa wakuunge mkono kwenye kazi yako?!

Wataungana na adui yako! Ndiyo kilichotokea kwa Zuchu na WCB. Kwa namna moja ama nyengine inaweza isiwaathiri ila kwa namna moja ama nyengine inaonyesha wapo mashabiki wapo serious kwenye mambo yao hususani masuala ya itikadi na wamewaonyesha kama wanaweza na wanaweza.

Inawabidi waelewe siasa ya Tanzania inabadilika kwa kasi ya hasira ambayo ni mbaya sana! Ana uhuru wa kuchagua chama! Ila afahamu siasa ni itikadi na yeye ni msanii achange karata zake vyema kama anatarajia kupata support ya jamii nzima yenye itikadi ya vyama tofauti.
Hivi hizo itikadi ni kwa mtu mmoja tu au? Mbona wasanii ni wengi walioimba nyimbo za hivyo kwamba hao hawaonekani au na pia hao wasanii zamani walikuwa hawatumiki kwenye kampeni au ndio leo hizo harakati ndio zinaonekana kama kugoma wamgomee na Mo Dewj mbona alionekana kuunga mkono upande mmoja basi waache kushabikia Simba sc na kugomea bidhaa zake. Likiwezekana hilo itakuwa sio unafki.
 
Back
Top Bottom