Diamond umemkosea nini Majizo na E-FM mbona hawachezi nyimbo zenu?

Ngoja nikuulize bro,
Upo kwenye Media??
Upo kwenye kiwanda cha Muziki??
Upo karibu na watu maarufu wa Muziki na Media??

Kama jibu ni ndio basi lazima ungekua unajua whats going on,
Kama jibu ni hapana basi hujui whats going on na ni vema ungewauliza wahusika kabla hujaanza kulalamika na kuonesha Diamond anaonewa sana na kuchukiwa sana.

Hujawahi kukaa na Diamond hata masaa matatu utamjuaje tabia yake? hao wanaosema ana dharau na bla bla bla jua wanamfahamu fika nje ndani sio kwenye TV.

Be crazy, Be Weird, Be whatever coz life is too short to be anything but HAPPY.
 
Mkuu radio kamwe haiwezi poteza umuhimu wake ..

Hio unasema wewe kwa maono yako,na siwezi kukupinga

Hata unapoishi mtaani kwako kama kulikuwa na duka moja tu mtaa mzima linalouza vocha pekeake,basi ilo duka lilikuwa na umuhimu kwa 100%

lakini kama sasa hivi izo vocha watu wa mtaani kwako wana uwezo wa kuzipata kwa njia nyingine au kwenye maduka mengine hapo hapo mtaani kisha ukaendelea kusema kwamba lile duka la mwanzo umuhimu wake umebakia vilevile 100% basi itabidi tukupime mkojo mkuu!!
 
Teknolojia gani unayoizungumzia?..marekani na teknolojia waliyonayo watu bado wanasikiliza redio,sembuse bongo??

Mtu yupo simuyu ndani ndani uko anaachaje kusikiliza redio??

Sent using Jamii Forums mobile app

Mfano wako wa simiyu haupo relatively na suala nililoliongea

Halafu ukakosea njia zaidi pale unapofananisha Marekani na apa bongo..yaaan ni vitu viwili tofauti

Ukitaka nikupe hoja ya msingi,basi nijbu kwa hoja ya msingi mkuu
 
hearly [emoji23] [emoji23] [emoji23] umesahau kuniambia niagize mofaya utakuja kulipa!
 
Bongo kila kitu vice versa mbele msanii analipwa kwa nyimbo yake kupigwa kwenye redio, huku msanii halipwi na kwenye show lazima ufanye bure usipofanya nongwa mara utaambiwa unadharau, kiburi lkn hawaangalii msanii kawekeza kiasi gani ktk ile kazi.Alafu ile movement iliyo anzishwaga na wasanii, kulipwa baada kazi zao kupigwa redioni sijui imeishia wapi au sijui ndio uoga wao kwa hizi media mpaka wana sahau haki zao muhimu.

Mimi Diamond namsikilizaga sana, hana matatizo ila watu wanamuona ana matatizo sababu anataka win win yaani kila upande unufaike na hapo ndipo unapogombana na washika dau (media) .Wakati wenzetu wa ulaya wanaamini nyimbo ni kivutio kinachowavutia wasikilizaji wasikilize redio zao na ndio maana kwa kujua umuhimu wa wasanii wanawalipa.

Kwanza kwa dunia ya sasa hata ukisoma baadhi ya tafiti, social media zimepunguza namba za wasikilizaji redio na watizamaji TV na ndio maana kila redio sasa hivi nazo zinatumia hizi social media platform ili kutafuta wasilikilizaji (insta, fb, YouTube) , so nikimuona msanii analia eti apewi promo na mshangaa wakati Kuna platform kibao za kupromoti kazi yako na ukaingiza hela, wakati kwenye redio hela huingizi na kwenye show unapiga bure.

Hizi media zijifunze kuheshim kazi za watu na mziki sio kazi ya milele unapokuwa wa moto ndio mda wa kupiga hela, ukishapita muda wako ndio basi, unabaki kuwa mtu wa lawama na kulialia kama Q chief na TID na wengineo.

Mimi nina mwaka wa pili nikifungua redio na sikiliza mpira TBC basi, ila TV vipindi vyangu ni habari Star TV, ITV, BBC swahili , Kipindi cha mahojiano EATV saa moja jioni baada ya hapo Trace Muziki, MTV base , NGE W (documentary za wanyama).Habari nyingine nitazisoma kupitia kwenye simu na PC yangu.

Mziki wa bongo nikimtoa Jide, Fa, AY, Nature, Prof Jay na Sugu hawa kidogo wapo vizuri, lkn hao wengine wana maisha mabovu, ninaowafaham mm Inspector, PNC na Big black (solid ground family wazee wa Bush party, yupo Tbt karibia St Mary College kwa mama yake hali yake ni mbaya) , sijui Blue maana nyumba yake ya Tabata mvua ikinyesha mnatega kambale ndani.
 
Kwani habari za michezo huwezi zipata mtandaoni? Kumbe na wewe bado mtumwa wa kina Shaffii Dauda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani habari za michezo huwezi zipata mtandaoni? Kumbe na wewe bado mtumwa wa kina Shaffii Dauda

Sent using Jamii Forums mobile app

Umesoma wapi ukakuta nimeandika habari za michezo hazipatikani mtandaoni?

Mkuu acha kukurupuka kama umefumaniwa,halafu uyo mtu uliemtaja nimeanza kumfahamu juzi juzi tu kwasabau ya haji Manara

Ndo ujue kuwa sinaga time na hao unaowasema wewe,japo nakiri kipindi nipo chuo miaka iyo nilikuwaga mtumwa wa XXL tu!!
 

Tatizo haliko kwa wasanii, Tatizo liko kwa Mameneja
kuna Said Fella, Salam na Babu Tale
Hawa wawili hawa, Babu Tale na Salam... ni shida kubwa na ndio wanayaleta hayo, wanaweza kwa wanaona wako sawa kwa upande wao kwa wanayoyafanya, ila kwa upande wa wanaofanyiwa yakawa sio sawa
 
Ni kweli hawahitaji media kufanikiwa lakini lazima tujiulize wasio cheza nyimbo zao amewakosea nini? kufanilkiwa ni kosa?

Mkuu kwa nini unahusisha kufanikiwa kwa Diamond na Kufungiwa/kutopigwa kwa nyimbo zake?? Mbona Clouds wana historia ya kufungia/kutopiga nyimbo za wasanii ambao hawana mafanikio kabisaa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wengi wanasema msanii hatakiwi kudharau media.. Msanii katoa ngoma kali sana kaipeleka media, baada ya hapo heshima inapimwaje hili wimbo wake mkali uanze kuchezwa?
Na kwa nini heshima anakosa Diamond hila anafungiwa mpaka Mbosso?

Ali Kiba akikosa hiyo heshima atafungiwa mpaka Abdu Kiba? Au Barnaba akikosa heshima inafungiwa THT yote?

Nafikiri kuna ishu zaidi ya heshima au dharau. Waswahili ni mabingwa wa kuvutana mashati.
 
AISEEE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…