Diamond umemkosea nini Majizo na E-FM mbona hawachezi nyimbo zenu?

kwa East Africa media wao tofauti yao na wasafi imeanza mwishoni mwa mwaka 2016 wao waliandaa tuzo na walitangaza kila msanii alete nyimbo zake katika idara ya muziki ili waweze kupanga kategori lakini wasafi walipuuzia ilo na iyo ndo sababu ya EATV na EA radio hawapigi nyimbo za wasafi kwani wao hawakuonyesha ushirikiano walipoandaa tuzo iweje wao wasapoti nyimbo zao...
Hivi
Diamond Platnumz tusimtetee sana jamaa anadharau imagine alichowafanyia East Africa Media. East Africa media waliandaa tuzo wakawaomba wasanii wajitokeze kujaza fomu za ushiriki jamaa akachomoa. Na siyo kuchomoa tu akatoa maneno ya dharau eti ohoo siwezi kujaza fomu mimi ili niwekwe kwenye tuzo ni kama naapply. Hili ndilo lililofanya mpaka kesho EA media wasipige nyimbo za WCB.

Mashabiki wa Diamond mnalaumu bure tu lakini tambueni kuwa hakuna mtu kichaa ambaye anaweza akaacha kucheza nyimbo nzuri za WCB akacheza vinyimbo vya kina Mario bila sababu ya msingi, ukiona mtu amefikia hatua hiyo jua kuwa imemlazimu. Redio stations ni makampuni lakini zinaongozwa na watu ambao wanastahili heshima na kuwa recognized mchango wao na wakidharauliwa wanaumia siyo wamiliki tu staff wote wanajisikia vibaya maana ofisi ni kama familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Diamond amemkosea nini majizo?
Ni Diamond pekee hakujaza hizo fomu?
 
Huu ni uongo mwanzo mbona walikuwa wanapiga? na mbona kuna radio zinapiga na linatajwa? sema tuu wamiliki wana chuki sana

Nikweli zipo redio zinazopiga nyimbo zao, ni matakwa yao, nionachomimi hizo redio zilizotajwa zinatafsiri kama ni kupromoti Wasafi. Wakati huo walikuwa hawajaanzisha Vituo vya Redio na Televisheni. Kwa sasa hiyo ni Brand.
 
Kuna wimbo mmoja ametoa Dulla Makabila, unaitwa "Kisimu changu" sehemu ameimba ni mwendo wa Savanna, akarudia tena ......ni mwendo wa Safari. Wimbo huohuo kwa Clouds ikifikia hapo wanazuia yasisikike maneno lkn kwa EFM wao wanaachia maneno yasikike. Tafsiri fupi kwa Clouds ni Brand kwa EFM ni ujumbe.

Pia huku mikoani kuna wimbo mmoja katika mashairi ametajwa Joseph Kusaga, huo wamefuta isisikike.
 
Diamond Platnumz tusimtetee sana jamaa anadharau imagine alichowafanyia East Africa Media. East Africa media waliandaa tuzo wakawaomba wasanii wajitokeze kujaza fomu za ushiriki jamaa akachomoa. Na siyo kuchomoa tu akatoa maneno ya dharau eti ohoo siwezi kujaza fomu mimi ili niwekwe kwenye tuzo ni kama naapply. Hili ndilo lililofanya mpaka kesho EA media wasipige nyimbo za WCB.

Mashabiki wa Diamond mnalaumu bure tu lakini tambueni kuwa hakuna mtu kichaa ambaye anaweza akaacha kucheza nyimbo nzuri za WCB akacheza vinyimbo vya kina Mario bila sababu ya msingi, ukiona mtu amefikia hatua hiyo jua kuwa imemlazimu. Redio stations ni makampuni lakini zinaongozwa na watu ambao wanastahili heshima na kuwa recognized mchango wao na wakidharauliwa wanaumia siyo wamiliki tu staff wote wanajisikia vibaya maana ofisi ni kama familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naungana na wote waliotoa maoni tena ni mazuri na yana afya masikioni mwetu.

Kwaupande wangu (ni maoni tu) sio kama kuna ugomvi na kati ya redio na redio lah, sina neno moja la kitaalamu ambalo linatumika kwa nitakachokisema.

Kundi linaitwa Wasafi, Rekodi Lebo, inaitwa Wasafi, Redio inaitwa Wasafi, Televisheni inaitwa Wasafi. Nini maana yake? Jibu ni Wasafi ni Brand (bidhaa) Nijuavyo itakuwa nivigumu hilo neno Wasafi kutajwa kwenye redio stesheni nyingine hasa zilizosajiliwa kutoa burudani, wanaita muingiliano wa maslahi, nisawasawa wanaifanyia promosheni bidhaa ya Wasafi.

Mo Dewji akianzisha kituo cha redio, kwenye mazungumzo ya watangazaji wake hawawezi kutamka neno Mo Faya (hichi kinywaji cha Ali Kiba) au uvae T- shirt ya Vodacom uwe unafanyakazi Zantel. Au kipindi kilichodhaminiwa na Airtel kikiwahewani halafu kuna tangazo linalosomwa mwisho wa tangazo kuna namba za simu (0625 ******) hauwezi kusikia mtangazaji akitamka " wapigie kwenye Halotel.... atakuwa amefanya promosheni.
[emoji120][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Au tujiulize wote, kwanini michuano ya Ndondo Cup haipati kurushwa hewani na redio zote?
 
kwa East Africa media wao tofauti yao na wasafi imeanza mwishoni mwa mwaka 2016 wao waliandaa tuzo na walitangaza kila msanii alete nyimbo zake katika idara ya muziki ili waweze kupanga kategori lakini wasafi walipuuzia ilo na iyo ndo sababu ya EATV na EA radio hawapigi nyimbo za wasafi kwani wao hawakuonyesha ushirikiano walipoandaa tuzo iweje wao wasapoti nyimbo zao...
kama ni kweli basi hao Wasafi walionyesha dharau
 
Diamond Platnumz tusimtetee sana jamaa anadharau imagine alichowafanyia East Africa Media. East Africa media waliandaa tuzo wakawaomba wasanii wajitokeze kujaza fomu za ushiriki jamaa akachomoa. Na siyo kuchomoa tu akatoa maneno ya dharau eti ohoo siwezi kujaza fomu mimi ili niwekwe kwenye tuzo ni kama naapply. Hili ndilo lililofanya mpaka kesho EA media wasipige nyimbo za WCB.

Mashabiki wa Diamond mnalaumu bure tu lakini tambueni kuwa hakuna mtu kichaa ambaye anaweza akaacha kucheza nyimbo nzuri za WCB akacheza vinyimbo vya kina Mario bila sababu ya msingi, ukiona mtu amefikia hatua hiyo jua kuwa imemlazimu. Redio stations ni makampuni lakini zinaongozwa na watu ambao wanastahili heshima na kuwa recognized mchango wao na wakidharauliwa wanaumia siyo wamiliki tu staff wote wanajisikia vibaya maana ofisi ni kama familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
vinyimbo vya Mario hapo ndio ulipoharibu mkuu japo ulikua na hoja nzuri. Jaribu kuonyesha heshima kwa wasanii wengine Marioo ni msanii mzuri pia
 
Back
Top Bottom