Kaka hayo mamlaka hatukupewa bure bure yanakuja na majukumu juu ya wanawake wanaume tuna majukumu makubwa juu ya wanawake yaani ili wawe chini yetu tunatakiwa kuwatimizia mahitaji yao yote kiuchumi sasa siku hizi dunia imebadilika wanaume wengi hawafanyi hivyo wanataka wake zao nao watafute pesa na wawasaidie katika maendeleo na kuhudumia familia kiuchumi kitu ambacho kinapoteza mamlaka tuliyonayo wanaume
Kwahiyo sidhani kama hiyo kauli yako bado ni applicable kwenye dunia ya sasa ambayo wanaume wengi wanakimbia majukumu yao juu ya wake zao halafu bado wanataka kuwa na mamlaka juu ya wanawake never ndo maana wanawake nao siku hizi wamekengeuka hawana tena nidhamu kwa wanaume na hatuwezi kuwalaumu kwa hilo Mungu siyo mjinga eti amwambie mwanamke amtii mwanaume hivi hivi tu wakati hatujawaumba wala hatujawazaa hiyo heshima ina gharama yake
Najua nimetoka kidogo nje ya mada maana mimi sipo kwenye huo umbea ila nilikuwa najaribu kukurekebisha hapo uliposema kuwa wanaume ndo wenye mamlaka hapa duniani huo umebaki tu ni siku hizi msemo ila kiuhalisia dunia ya leo hiyo mamlaka haipo tena tumeshaipoteza na hatuna wa kumlaumu zaidi ya sisi wenyewe