kutoka Bongo5
Diamond Platnumz amesema Zari hajawahi
kuolewa na kwamba hadi sasa hajapokea baruajn
yoyote kutoka mahakamani ikimtaka kuchukua
vipimo vya DNA vya mtoto wake, Tiffah.
Kwa mujibu wa Diamond, barua iliyowekwa
kwenye akaunti ya King Lawrenc ni moja ya njia
ya swahiba hiyo wa ex wa Zari, Ivan ya kujipatiaj
umaarufu.
Sijapokea barua yoyote, Diamond ameiambia
255 ya XXL kupitia Clouds FM leo.
Unajua lazima tujue kila mtu anatumia mitandao
kwa njia zake. Wengine wanatumia kutafutia
umaarufu kama hivyo which is not bad but
kupata umaarufu ni kazi sio, mtu anatafuta njia
yoyote kutafuta umaarufu na watu wakamsikiliza
na kupata pongezi kwa sababu amekaa amebuni
kitu mpaka watu wakamsikiliza, amesema
Diamond.
Zari hajawahi kuolewa kwanza, ni story tu hizo,
lakini hajawahi kuolewa, ukimuuliza mwenyewe
anasema hajawahi kuolewa kabisa, amesisitiza
staa huyo.
Unapokuwa na mahusiano na mtu huwezi
kufuatilia vitu vyake vya nyuma. Tumeanza
maisha yangu mimi na yeye sidhani kama
umeshaona post yangu yoyote ya kumzungumzia
vibaya ndio maana nikiona vitu ambavyo navisikia
naona ni uongo, mimi sifuatilii maisha ya mtu.