Diaspora Hawatoi connection?

Aussie the land of opportunities, pako vizuri....jiandae na safari ya masaa zaidi ya 20 , Dar-Dubai, Dubai-Perth/Sydney/Melbourne, ngozi nyeusi hawajawa wengi sana lakini huwezi kuwakosa wakenya na wanaija, waasia hasa wachina wapo wa kumwaga.
 
Wagumu toka sehemu mbalimbali na safari zao kuelekea Marekani ya Kaskazini

Ungana nasi kwa kutazama video hii kufuatilia mguu kwa mguu toka wakiwasili jijini Sao Paolo Brazil wakijifanya raia wa Angola ktk utalii Brazil kisha wanaanza safari kwenda Canada.

Safari hii ya Wakongomani toka Congo wanaoingia Brazil bila viza kisha wanakutana na wahamiaji wengine toka nchi za China, Morocco, Mali, Senegal, Somalia, Nepal, Nigeria and Bangladeshi kwa miezi mitano wanakatiza mito misitu na barabara ktk nchi kumi za bara la Marekani ya Kusini kabla ya kuingia Marekani nia ni kufika nchini Canada.

Safari hii ya kilometa 20,000 wanakutana wa wahamiaji wengine toka nchi za Caribbean na Latino America ambao pia lengo lao ni kufika Marekani na Canada. Wakongomani lengo ni kufika jimbo la Quebec Canada linalotumia lugha ya Kifaransa kama Congo.

Safari hii inajumuisha kutembea kwa miguu, kupanda basi, taxi, punda, boti , ngalawa na kushirikisha wenyeji wa nchi hizo za Latin America ktk kuonesha njia za vichochoro vijijini zisizo ktk ramani za GPS maana wahamiaji wanatumia simu janja smart phone kutafuta welekeo kupuguza malipo kwa wavushaji watu kwa magendo pale inapowezekana.

Njiani katika njia za panya zilizobatizwa "Njia ya Kuzimu" kukwepa askari wa uhamiaji, kunaonekana utelezi utokanao na mvua zisizokoma za misitu minene ya tropiki, matope yafikayo ugokoni, makaburi yasiyo na jina wala alama za imani zao kwani hao wahamiaji waliopoteza maisha na sasa wamelala udongoni hata kaburini utambulisho wao haujulikani.

Nchi nyingi kama Colombia, Ecuador na Panama wameongeza vikwazo ktk vituo vya mipaka rasmi kutokana na mbinyo toka serikali ya Marekani. Hivyo wahamiaji na watu wote wanaojihusisha na biashara ya kusafirisha watu hutumia njia za vichochoroni kukwepa askari hao.

Pamoja na hayo bado kuna ongozeko kubwa la wahamiaji wanaoelekea Marekani ya Kaskazini wakiwa na imani ya kutafuta fursa na maisha bora zaidi. Wenyeji wa vijiji vya ndani ndani Colombia na Ecuador wanashangazwa na ari bila kusahau hamasa ya kusonga mbele ya hawa wageni toka nchi za mbali.

Watu watajiuliza unawezaje kukatiza nchi zaidi ya 10 salama bila kudhuriwa na wenyeji au magenge ya kutorosha watu mipakani.

Sababu ni kuwa hii ni biashara kubwa inayoingiza kipato na makundi ya waliokuwa wanasafirisha madawa ya kulevya sasa wamejiingiza ktk biashara hii ya kusafirisha watu. Hivyo wakubwa wa magenge haya hawataki kusikia mtu kakabwa au kina mama kubaka n.k na kuwataka wote wanaojihusisha na biashara hii ya kuvusha watu kimagendo mipakani kuwalipa 'kodi' ma drug lords na pia kuhakikisha wageni hao wanamaliza safari salama ili njia zao ziendelee kuaminiwa na maelfu ya wageni hawa waendao Marekani ya Kaskazini. Yeyote atakaye mdhuru mgeni huadhibiwa kwa adhabu kali na wababe hawa wa biashara hii ya kusafirisha wageni.


Endelea kusoma:

Source: France 24
 
asante sana nilitegemea jibu kama ili kutoka kwako mimi nimechangia mada tu kuhusu msaada sitegemei mtu yeyote hapa sky is the limit brother.
 
asante sana nilitegemea jibu kama ili kutoka kwako mimi nimechangia mada tu kuhusu msaada sitegemei mtu yeyote hapa sky is the limit brother.

That's the mentality. Ukijisaidia at least halfway watu watakusaidia be it wabongo wenyewe au watu baki. Nimesaidiana na watu baki kabisa ambao leo tumegeuka ndugu wengine wapo kutoka jukwaa hili hili la JF. Binafsi hiyo roho mbaya au kusema wabongo hawashirikiani naonaga ni story tu. Kama wao walifika basi inawezekana.
 
Weka picha tuamini
 
Asante kwa kuchangia mawazo brother.
 
Asante, hivyo vyuo vinavyotoa hizi post graduate mpaka ufike ndio navihitaji binafsi nimefuatilia poland gharama zao ziko reasonable bank statement ndio kipengele.
Vipi mawakala wa kazi huko na gharama zao!?
Bank statement unaweza tafuta ya mtu unaemfaham awe na mpunga kdgo, along with barua kusema atalipia/gharamia shule na pesa za matumizi yako ya kila mwez..
 
27 March 2023
Balozi Tom Amolo azungumzia nafasi za zilizopo za kuingia Germany kufanya kazi mbalimbali pia fursa za elimu ktk nchi hiyo ya ulaya. Balozi amefanya mahojiano ktk video hii kwa lugha sanifu ya kiswahili

Source : Nation

N.B
SERIKALI INA RASILIMALI ZA KUTOSHA KURASIMISHA RAIA KWENDA KUCHUKUA FURSA KIHALALI NJE YA NCHI

Ni mfano mzuri wa serikali kushiriki ktk kuwatafutia raia wake fursa, kuweka makubaliano ya visa, kazi za muda mfupi na mrefu masuala ya wananchi kupata pasipoti, masomo ya lugha za kigeni kuongeza uwezekano wa kupata kazi za aina zote n.k

Nchi kama nchi ya the Philippines 🇵🇭 kwa mfano inatoa uzito unaofaa kwa mafunzo ya somo la ziada kuhusu lugha na tamaduni za nje kupitia vyuo kibao vya kama Ras Simba zinavyoratibiwa kwa karibu ubora wake na serikali ili raia wake wapate ufahamu, connections, network na wepesi wakihitimu vyuo vya VETA, UBAHARIA, UUGUZI n.k moja kwa moja wanakwenda nchi za Ulaya, Canada, Mashariki ya Kati na Australia kufanya kazi .

Hili suala la huku Tanzania mtu mmoja mmoja ktk diaspora kubebeshwa zigo la lawama wakati ilitakiwa serikali ya Tanzania iwe mstari wa mbele kuweka mazingira mazuri mikataba mizuri baina ya nchi na vyuo vyote kuwekewa
mtaala wa somo la lugha za kigeni na tamaduni za nje ili wahitimu wa Welding, makenika useremala udereva VETA, MUCHAS, UDSM, SAUT n.k wawe tayari kutimkia ngambo wakiwa wanajiamini kunyakua fursa.
 
Haaahaha safari kama hizi kizazi cha sasa cha wabongo hawawezi ndio maana hata ma shoga wameongezeka. Kizazi cha zamani watu walikua wanatambaa toka Pakistan wanakatisha Balkan hadi wanaingia ulaya, chakula ni mkate na maji. Hawa ma yoyoo wa sasa wanataka connection halafu na kuhifadhiwa juu na kazi uwatafutie. Hizi ni trip za wacongo, wakenya, wanaija, waghana na mataifa wengine wagumu wa africa sio hawa wa kubana pua eti wahifadhiwe. 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
POVU RUKHSA!
 
Hapo kwenye internship zipo, ila kuzipata ni issue
Diaspora mtusaidie kama mna njia rahisi
 
Povu langu wewe si Mbongo pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…