Diaspora Hawatoi connection?

Ndugu usijichoshe sana kujibishana na mtu jibu tayari linajulikana wabongo wazinguaji kwenye kutoa connection za majuu kama siyo uchoyo basi tunaogopana labda.
 
Wabongo wanaponda wabeba box kumbe behind the scene wanatamani kwenda kiwanja.

BTW; naomba connection ya kwenda kwenda Russia kupiga box
Wabongo wanachotaka kinachoitwa connection, umuandikie jinsi ya kuapply college, eeh akikubaliwa jinsi ya kupata visa, eeh akiipata umpokee airport, eeehh umchukue uende nae kwako aoge halafu ale bure.. eeh kesho uache shughuli zako umpeleke sehemu za kazi umuoneshe na umsaidie kuaplly kazi. yaani umraisishie kila kitu kama mtoto mdogo vile, hajui kuna watu wanakata mbuga wanaruka ukuta tokea Mexico na wengine wana cross boarder kwenye snow ya Canada. Nachoona ni kuwaacha wapambane na tozo huko na sie tuendelee kubeba mabox yetu teehteehteeh.
 
Na mkikaribishwa amchelewi kuharibu.Mfano ukienda sauzi hata ukisikia mbongo anagonga kiswahili,weka headphones kabisa.
 
Bongo watu wanakula bata tu sio
Bongo kutamu mzee baada ya Bi mkubwa kuchukua kitengo magogoni😂🤣🤣🤣🤣 kidogo kuna ahueni.Nilikua na mpango wa kwenda Chicago kule southside Parkway gardens 6400 blocks (WIIIC City)kwenye zile project now days wanaziita O block nikaanzie aharakati huko ila mwenyeji wangu ambae ni raia wa marekani kanitisha kwa kuniambia ukweli kuhusu gang,s violence eneo analoishi ambalo mimi nitafikia kwake kukaa nikaghairi kwa mda mipango yote mkuu.
 
kaka komaa mwenyewe ukitegemea mtu muda utakuacha bure hakuna atayekupa msaada hapa.
Labda nitoe sources zangu haswa kwa agricultural stream
  1. Kuna CAEP
  2. Kuna waTz wanajiita Universal Career Development Pivot
  3. Kuna Bixter.Training
  4. WISE foundation
Hao ni kama madalali, makampuni, recruiters, nk ama vyovyote unavyoweza kuwaita.... Wanaotafuta kampuni zinazokuwa na nafasi kwa ajili ya kwenda kupata training/internship. Kikawaida utaenda kwa ajili ya hizo internship kupitia J-1 Visa. Nina marafiki walioenda kupitia kampuni zote hapo, binafsi nipo kwny process ila mambo ni kupambana. Kama kuna fursa tushirikishane.
 
Mdau huyo mwana wa kuitwa @ Bufa alikuambia uwe shoga ndio uende marekani🤣🤣🤣🤣😂😂😂??????Yeye anakaa state ipi??????? Nitafute nikupe connection za wana wapo Chicago na Huston city Texas wanaweza kukupa maelezo yaliyonyooka mkuu.Usikate tamaa kama ipo basi ipo tu.
 
Safi sana kwa mzalendo Putin wewe kweli mbeba box halisi Ndugu yangu
Putin ni mzalendo hasa na anawajali watu weusi,
Pia Russia ilitusaidia kipindi kile cha kupambana na wakoloni. Ni wakati sasa Watanzania twende kwa mzee Putin kupiga box tuachane na hawa wazungu wa magharibi maana wanalazimisha ushoga
 
Ukishinda dv lottery unateleza kama upepo. Hela yako tu ya nauli tena uzuri hii Hamna kukata ticket ya go and return.
Ukiwa na m5 tu unachokomoka kirahisi kabisa.
Kuhusu SSN na green card wanakutumia kwenye address utapofikia ndani ya week mbili tu.
Uzuri wa dv lottery mambo yote unamaliza ubalozini hapo dsm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…