Diaspora tukutane hapa: Tupeane ushauri wa kuanza maisha mapya Tanzania

Hapo utafurahia maisha bongo, ila kama wewe ni ras kama I'd yako mm
Hapo uta
Hapo bongo utapafurahia, wewe ni Ra's kama I'd yako ilivyo? Yaan sijui ma rasi nawachukuliaje? Any way nawaza tuu, maana juzi town nimekutana na ras ana dem mzungu, inasemekana ni gf wake ila alivyo kuwa dah suliluali kama linataka kudondoka, sigara yaan nashindwa kumdefine.

Kama nimekukwaza nisamehe
 
Mkuu mm hilo ni jina tuu sina uhusiano na u ras

sivuti bangi wala sina dread
 
Wapi nimekwambia unaringa? Dogo I've been there done that.....anytime nikitaka kuingia US au UK au nchi yoyote ya aina hio naingia. Sioni cha ajabu, ndio maana nakushangaa kuja kuponda watu kisa $150,000! Sio hela kidogo ila sio tiketi ya kuja kuponda watu humu.

Yaani unaongea vitu vya kawaida....sasa unafikiri nani anataka kujua kuwa huwa unarudishiwa hela ya kodi? Hicho nacho ni kitu cha kuja kututangazia humu?! Ndio maana kuna watu wakiona thread ya Diaspora wanakuja kuwatukana tu kwasababu ya watu kama wewe!
 

Been there done that! halafu ukaamua kuwa bilionea wa Kariakoo. huh!
Kwani wewe nani alikwambia watu wanataka kujua kuwa ulifika US na UK? Kunya anye kuku akinya bata kaharisha!

Unakataa hujasema naringa, brag maana yake nini au hukutumia hilo neno kwangu?

Sijaponda watu kwa hela nimeponda watu kwa uzembe. Halafu wewe pia una usongo na diaspora. Kuna mada huwa naposti kuwafunua macho watanzania yaliyoko nje unakuja juu kwani kila kitu lazima tuige Marekani.

Wewe unaona naringa wengine wanajifunza hapa. Na hakuna njia nzuri ya kufundisha zaidi ya kutumia mifano hai.

Kumbuka nilisema sina umeneja wala ukurugenzi. Elimu ya kufukuzia position hizo ninayo. Ila nimeona nichukue position ya chini yenye majukumu madogo ili nipate muda wa kuingia viwanjani nifukuzie shughuli zangu nyingine.

Eti ndio maana kuna watu wakiona mada za diaspora wanakuja kututukana. Hujagundua kuwa chupi zimewabana wameukimbia huu uzi?

Bila ya kujiongopea mwenyewe ulipokuwa Marekani ulitengeneza dola zaidi ya laki na sabini kwa mwaka mmoja?

Huo ni mshahara wa mwaka wa mbunge wa Marekani. Kudaaaaadeki!

Don’t hate the player, hate the game!
 
I wish akili zingekuwa zinachangiwa kama damu waliopungukiwa na akili wangechangiwa!
 
I wish akili zingekuwa zinachangiwa kama damu waliopungukiwa na akili wangechangiwa!

Unajua Mkuu kuna watu humu wanaongea as if wengine tumezaliwa sayari ya Marsi au kwamba bongo hatuijui. Hivi huyu mtu anayekunja $150K a year kwa bongo...ni nani? na kama wapo wako wangapi? Hii ni hela ndefu no matter how we look at it.

Wengi walikuwa wanazipata serikalini kwa figisu (remember CEOs wa Mashirika ya umma na 40M zao ambazo baada ya Magu kuingia zimewatokea puani..). In all, while in US and other western countries it is possible kutengeneza hiyo hela hapa kwetu...bado sana. Yes, wapo wanaozipata hizo...... Lakini ni very few and indeed very notable.
 

Kabisa.

Mimi nimesema watu wapatayo hiyo hela kwa mwaka tena kihalali kabisa wanaweza wasizidi hata asilimia 2 ya population nzima. Si ajabu hata asilimia 1 hawafiki.

Hivi GDP per capita ya Tanzania ni kiasi gani vile?
 
Kabisa.

Mimi nimesema watu wapatayo hiyo hela kwa mwaka tena kihalali kabisa wanaweza wasizidi hata asilimia 2 ya population nzima. Si ajabu hata asilimia 1 hawafiki.

Hivi GDP per capita ya Tanzania ni kiasi gani vile?

Kabisa. Ni very few kama wapo. Hata hiyo one percent sijui kwa kweli.....(kwa private sector ipi? kwa public sector ipi?)

Just thinking eti Mengi au Bakhresa anamlipa CEO wa makampuni yake 300M kwa mwaka...hahahahahaah...

Vingine humu wengine tunaandika kuchangamsha baraza Lakini tunajua kabisa uhalisia ni mdogo mno in TZ context.
 
Msameheni bure jamaa pamoja na usomi wake kachanganya mzunguko wa mtaji wa dola laki na hamsini na kipato cha dola laki na hamsini. Hajui kuwa wakifika China wakishanunua mzigo wanabakia na bukta tu halafu wanaomba Mungu biashara iende salama.
Na hiyo ni kwa wachache wenye mtaji huo. Wengi wao wanazungusha mtaji wa dola elfu hamsini mpaka mia.
 
Mkuu inaonyesha hiki kibano kilikukuta. Hebu tuambie ni nchi gani ulikokuwa na mambo gani yalikukuta ukarudi hapa nyumbani? Sababu unaongea kwa uzoefu wa maisha hayo.
 
Ha ha ha wapinzani wa diaspora wamezima sigara. Hii ndio ile Umsolopagas alisema “wako wapi waliopanda ngazi kuu”

Mwanadiaspora ukiamua kurudi nyumbani rudi tu kwa mapenzi ya nyumbani usirudi kwa kushindwa maisha nje. Labda kama umeshakipaka sana nje hutamaniki huchukuliki.

Sio siri kuishi kwenye mazingira haya unaweza kuona ni afadhali matope ya Bongo. Inapendeza kuchungulia ila kama uko kituo cha basi. We acha tu.
 

Mtoa mada kuna kitu muhimu kwenye uzi wako hakikujadiliwa. Hao rafiki zako watatu waliokufa ni mazingira gani walikufa. Ni ugonjwa, ajali au waliuliwa. Unaweza ukatufundisha kitu.

Ninaowajua mimi wamerudi Bongo wengine wana hali nzuri kiuchumi. Wengine hawafi cha moto wanakiona. Tena hawa niliwaambia wasirudi. Wengine walirudi wakageuza wamerudi nje.

Kuna mtangazaji mmoja wa muda mrefu wa redio Marekani ilitokea figisu kazini kwake akaacha kazi. Ila alisema atatafuta ishu ya kufanya. Kwa sababu anawajua rafiki waliostaafu pesa wanayo lakini walikufa chapu chapu kwa kukaa tu nyumbani.

Labda niseme kabla ya kurudi nyumbani jipime afya. Wakikuambia una makolestro na presha pima ukirudi nyumbani yatazidi au yatapungua. Inaweza kuwa heri kwa sababu nyumbani tunatembea sana na hatuli sana mafuta.
 
Wacha niendelee kujisifia atakaechafuka roho alambe ndimu ili asitapike.

Mwishoni mwa 2008 Bush alipokipaka uchumi ukadorora wamarekani walipoteza kazi maelfu kwa maelfu kila siku. Nilikuwa mmoja waliokumbwa na dhoruba ile.

Ila sikuterereka kwa sababu nilikuwa na kazi mbili za part time zaidi ya hiyo niliyoachishwa ambayo nilikuwa nafanya full time.

Kilichoendelea niliomba full time moja ya kazi zile mbile. Nikawa na kazi moja na nusu. Raha zaidi waliponipa full time kwa kuwa ilikuwa kazi ya serikali wakanipa mshahara sawa na wa ile kazi niliyoachishwa. Walimechisha mshahara wangu.

Sasa basi kule nikoachishwa kazi kulikuwa na mafao. Na jamaa hawakutoa kwa mpigo. Wakaendelea kunilipa mshahara karibu mwaka mzima.

Ina maana mwaka 2009 wakati watu wengi hawakuwa na mishahara walitegemea mishara ya serikali kwa wasio na kazi ambayo ni kama nusu mshahara, mimi nilikuwa nachukua mishahara mitatu kama mfanyakazi hewa wa Bongo[emoji23][emoji23][emoji23]

Bongo kuna utaratibu huo wa kulinda maslahi ya wafanyakazi?

Diaspora 3 Bongo 0
 

 
Hii topic tamu sana mi nimewai kwenda nje ila sijawai kuishi sana zaidi ya mwezi sema maisha niliyokuta ndugu zangu waafrica wanaishi kule ni tofauti na jinsi tunavyowachukulia uku yani ukisikia mtu anasema "Ana watoto watatu wanaishi nje" Ile prestige ni tofauti na furaha waliyonayo wakiwa kule .
Bongo kutamu sana
 
Kwani baridi unashinda nje? Huna heater nyumbani? Kwenye gari je? Baridi mwaka mzima?

Waulize watu Omaha[emoji23][emoji23][emoji23]

Halafu kuna wanaopanda matreni hasa Ulaya. Kwa mfano wanaofanya kazi Washington DC kuna shida ya parking.Wengi wanapaki magari vituo vya treni wanaingia DC kwa treni. Wengine huona udhia wanapanda basi na treni.

Fikiria watu wa Canada. Ndio maana hakuna watu kule. Linchi kubwa vile lakini lina watu wachache kuliko Tanzania.
 

Maisha hayafanani kuna wengine hao watoto ndio wanaowapa pesa ya kula na kuishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…