Diaspora Wetu Wanafanya Nini cha Kuonekanika Huko Ughaibuni?. Diaspora Mliofanikiwa, Onekanikeni Kupitia TAK na Rudisheni Tanzania Japo Kidogo!

Mkuu, Nimefurahi kuona type 1 unawaheshimu pia.
Unajua nini, maisha Yana mambo mengi sana. Sometimes people decice to be how they are because of what happened to them. People around you can influence you to choose how to be.

Mapitio yangu ndio sababu ya kuona niishi maisha yangu tu. Unaweza kuwa unateseka kwenye jamii ambayo watu wanaishia kukusimanga na kukunyanyapaa ingali kuwa unajua wanaweza kabusa kukusaidia kulinusuru na hali Yako lakini haiwi hivyo.

Unaamua kuondoka au kupambana kwa nguvu zako, juhudi na maarifa Yako, unapata bahati ya kufanikiwa then from nowhere mtesi wangu ajitie kunifahamu. Never, can't do so. Kusaidia ni willing yangu na kuchagua namna ya kuishi pia ni juu yangu, iweje mtu awe na malalamiko eti nimefanikiwa na sisaidii au awe shocked na mfumo wangu wa maisha?

That's all
I Feel it ....uncle
Myself ni muhanga wa hili suala though bado sijavuka boundaries as you, Pasco mayalla na wengine
 
Ni ziara binafsi kwasababu mimi ni an African man, nina miji miwili, first family iko hapa US, second family iko Bongo
au ndio kwenye harakati za ppr kufungua ofisi USA?
Kufuatia hussles za a working viza za production team yangu kuja US, nimeamua kuisajili PPR US narudi Bongo kumtafuta mtu competent kuwa bureau chief wangu wa US, TAK itaanzia US.
Huenda ukawa na lengo zuri lakini namna ulivyolileta inatupa ukakasi.
Mimi ni Mbongo, na wabongo nawajua, especially when it comes to sharing success stories, hivyo sishangai. Kuna watu wanafanya makubwa mazuri lakini wako low profile, mfano mzuri ni S.S. Bakheresa, japo ana TV na redio, huwezi kuona akionyeshwa anatoa msaada popote, lakini anasaidia sana. Na kuna wengine wakisaidia lazima wajionyeshe. Lengo la TAK ni kuimulika Tanzania Africa na Kimataifa kwa Watanzania.
Shida kubwa mara zote imekua upande wa serikali yetu, wao ndio wanatakiwa watoe boriti Kisha mambo ya kibanzi yatafuatia kwenye hili la Diaspora wa Tanzania waishio Marekani.
It's true
Hao jirani zetu unaowatolea mfano wamefika hapo kwa vile serikali Yao ipo bega Kwa bega na wao.
Hiki ndicho tunachotaka Diaspora wetu wafanye waseme wangependa serikali yao iwafanyie nini?. Kila mtu wa East Africa akifika DC, ukiulizia African foods unapelekwa pale. Viongozi wa Kenya wanakutana na Wakenya hapo, sisi viongozi wetu ni kukutania kwa balozi au hotelini!. Visibility ya diaspora wa India, Ghana, Nigeria, Kenya etc ni kubwa hadi data za remittances ni very transparent, kwa Tanzania...
P
 
Mkuu, Nimefurahi kuona type 1 unawaheshimu pia.
Unajua nini, maisha Yana mambo mengi sana. Sometimes people decice to be how they are because of what happened to them. People around you can influence you to choose how to be.

Mapitio yangu ndio sababu ya kuona niishi maisha yangu tu. Unaweza kuwa unateseka kwenye jamii ambayo watu wanaishia kukusimanga na kukunyanyapaa ingali kuwa unajua wanaweza kabusa kukusaidia kulinusuru na hali Yako lakini haiwi hivyo.

Unaamua kuondoka au kupambana kwa nguvu zako, juhudi na maarifa Yako, unapata bahati ya kufanikiwa then from nowhere mtesi wangu ajitie kunifahamu. Never, can't do so. Kusaidia ni willing yangu na kuchagua namna ya kuishi pia ni juu yangu, iweje mtu awe na malalamiko eti nimefanikiwa na sisaidii au awe shocked na mfumo wangu wa maisha?

That's all
Mimi naheshimu sana the right to privacy, ila napenda holistic lifestyle, live for others.
P
 
Ni ziara binafsi kwasababu mimi ni an African man, nina miji miwili, first family iko hapa US, second family iko Bongo

Kufuatia hussles za a working viza za production team yangu kuja US, nimeamua kuisajili PPR US narudi Bongo kumtafuta mtu competent kuwa bureau chief wangu wa US, TAK itaanzia US.

Mimi ni Mbongo, na wabongo nawajua, especially when it comes to sharing success stories, hivyo sishangai. Kuna watu wanafanya makubwa mazuri lakini wako low profile, mfano mzuri ni S.S. Bakheresa, japo ana TV na redio, huwezi kuona akionyeshwa anatoa msaada popote, lakini anasaidia sana. Na kuna wengine wakisaidia lazima wajionyeshe. Lengo la TAK ni kuimulika Tanzania Africa na Kimataifa kwa Watanzania.

It's true

Hiki ndicho tunachotaka Diaspora wetu wafanye waseme wangependa serikali yao iwafanyie nini?. Kila mtu wa East Africa akifika DC, ukiulizia African foods unapelekwa pale. Viongozi wa Kenya wanakutana na Wakenya hapo, sisi viongozi wetu ni kukutania kwa balozi au hotelini!. Visibility ya diaspora wa India, Ghana, Nigeria, Kenya etc ni kubwa hadi data za remittances ni very transparent, kwa Tanzania...
P

Ahsante sana Kwa majibu yaliyoenda mbali zaidi ya matarajio yangu Kaka.

Kama mtizamo wa serikali hautabadiliia inavyowachukulia diaspora, sitegemei wao watahangaika au kujishughulisha Kwa chochote kinachowahusisha wao na serikali.

Ni kama tayari serikali yetu ilishaweka wazi kwamba haiwakumbatii wala kuwathamini hawa watu, ndio maana wengi wamehanfaika wanavyojua wao hadi kufikia hapo walipo. Huenda hizi juhudi zako zikabadili upepo siku za usoni, lakini Kwa Sasa, hili ni jambo gumu sana kutekelezeka.

Aidha nikupongeze Kwa hatua uliyopiga kwenye eneo lako la kazi, kupanua wigo na kuwa na malengo makubwa African man, hongera sana.
 
I Feel it ....uncle
Myself ni muhanga wa hili suala though bado sijavuka boundaries as you, Pasco mayalla na wengine
What matters ni kufanikiwa kwa kuyawezea maisha, kuna watu wako hapa hapa Bongo na maisha wameyapatia, na kuna watu wako ughaibuni, bado wanajitafuta. Mimi target yangu kwenye TAK ni only the success stories.

It's true uncle...hiyo burning desire uko nayo ni absolutely impressive...hope one day at a time stories will change in a blink of an eye
 
Sij
Wanabodi,

Bado niko hapa nchini Marekani kwa ziara binafsi, nimejitahidi kujichanganya na baadhi ya wana diaspora wa Tanzania walioko nchini Marekani, na kujiuliza jee wana Dispora wetu, wanafanya nini cha kueleweka na cha kuonekanika?.

Nimejitahidi kuwasiliana na kile chama cha DICOTA, sikubahatika kupata ushirikiano mzuri, ila nitaendelea kuwatafuta Diaspora wetu waliofanikiwa Marekani, wanafanya nini, na hayo mafanikio yao, yanaifaidia vipi nchi yao ya Tanzania?.

Kwa kupitia juhudi binafsi, nimefanikiwa kumuona dada mmoja wa Kitanzania, aliyehamia Marekani, mwaka 1999, na yuko kule mpaka leo. Huyu dada, naomba nisimtaje jina kwasababu sikumwambia kuwa nitaandika. Nime note Diaspora wa Tanzania waliofanikiwa hapa nchini Marekani, hawapendi kutajwa au kuandikwa wanafanya nini Marekani.

Huyu Dada ni mmiliki wa kampuni inayo fanya biashara ya huduma, services industry, ameajiri watu zaidi ya 50, kila mwezi anawalipa mishahara ya zaidi ya milioni 500.

Dada kanikaribisha kwake, ana kaa mtaa wa kitajiri, anamiliki nyumba, kubwa ya ghorofa tatu na ana magari 5 ya kifahari, ikiwemo Benzi ya G Wagon na gari ya Kimarekani ya Tesla inayotumia umeme. Hesabu ya haraka haraka ya thamani ya magari ni zaidi ya Shilingi Bilioni 1 ya Kitanzania.

Huu ni mfano mmoja tuu wa Mtanzania aliyefanikiwa Marekani, ametoa ajira kwa watu, na kutengeneza faida kubwa. Nilipomuuliza kwanini asiwekeze Tanzania, alinijibu anasubiria uraia pacha, ndipo aje kuwekeza Tanzania.

Imetokea tuu mimi ninamfahamu huyu Dada, mpaka kule kijijini kwao, Sanya Juu Moshi, ambako mimi nimefika, na kabla sijakwenda Marekani, nilipita hapo kwao Sanya, sasa hali niliyoiona ya umasikini wa hapo kijijini kwao, nikilinganisha na maisha ya kitajiri na kifahari anayoishi Marekani, ni mbingu na nchi!.

Hivyo huu ni wito kwa serikali yetu kuharakisha mkakati wa uraia pacha, ili Diaspora wa Tanzania waliofanikiwa ughaibuni, waje kuwekeza nyumbani Tanzania na kurudisha shukrani nyumbani Tanzania na sio kupiga tuu mapicha kurungishia mandinga yao makali ya ma G-Wagon na ma Tesla!.

Mtu Mtanzania ana magari matano ya kifahari, nchini Marekani, anaendesha kwa kubadilisha tuu magari, halafu ile hospitali ya Kibon’goto pale Sanya, kuna wamama wajawazito, wanajifungulia chini kwa kukosa, kitanda, ile G-Wagon moja tuu, ingejaza vitanda hospitali nzima, au ma deski shule nzima!.

Nimetembelea maeneo mbalimbali ya Marekani labda nitaona mafanikio ya kuonekanika ya Diaspora wa Tanzania, zaidi ya huyu dada kunikaribisha kwake, sikufanikiwa kuona kitega uchumi chochote cha Mtanzania nchini Marekani, kila rais wetu akija Marekani ni kukutana na Watanzania waishio Marekani, na kubadilisha mawazo tuu, Rais wa Kenya akija Marekani ni anafungua miradi ya Diaspora wa Kenya.

Muda aliokuja Marekani, huyu mdada wa Tanzania, ule mwaka 1999, ni muda huo Mkenya Kevin Onyona, alihamia Marekani, na kuajiriwa na Home Depot, kampuni ya kimataifa ya uboreshaji wa nyumba ya Marekani. Sasa hivi Kevin ni mmiliki ya migahawa ya Swahili Village ambayo ni mojawapo ya mikahawa bora zaidi ya vyakula vya Kiafrika nchini Marekani.

Kevin Onyona alianzisha mlolongo huo mwaka wa 2016, na leo inajivunia migahawa mitatu. Miaka sita baadaye, ametumia migahawa yake kujenga uhusiano halisi kati ya utamaduni wa Kiafrika na dunia nzima. Mkahawa mkuu wa Swahili Village oko Rhode Island Ave, Beltsville. Migahawa mingine miwili iko Washington DC na New Jersey. Mgahawa wa Washington DC ulifunguliwa na aliyekuwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kiongozi gani wa Kitanzania aliwahi kufungua mradi wowote wa Diaspora wa Tanzania nje ya Nchi?

Wito kwa Diaspora wetu, najua kuna uwezekano kuna mambo makubwa mazuri ya kuonekanika Diaspora wa Tanzania wanafanya, lakini hatuyaoni na hatuyajuo, hivyo natoa wito kwa Diaspora wetu, anekanikeni basi, inaumiza kila siku unaona diaspora wa wenzetu, na kujiuliza diaspora wetu wako wapi na wanafanya nini?.

Sasa mimi mwandishi wakp wa habari na mtangazaji wa kujitegemea, Pascal Mayalla, , anayeandaa vipindi vya TV, Redio, makala magazetini na kwenye mitandao ya kijamii, nikifanya kazi kupitia kampuni ya PPR, www.ppr.co.tz, ambayo sasa imetua rasmi nchini Marekani kwa kufungua ofisi, nimejotolea kuandaa vipindi vya mchango wa diaspora wa Tanzania kwa maendeleo ya taifa.

Kipindi Kipya cha TAK
TAK ni kipindi kipya cha TV chenye lengo la kuiangazia Tanzania Kitaifa, Kikanda na Kimataifa kuhusu mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, ambayo yanaihusu Tanzania kwenye medani za kimataifa, kama issues za Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola, issues za kikanda na kimataifa, AU, SADC, AfCFTA, Bunge la Afrika, Bunge la EAC, Jumuiya ya Africa Mashariki, EAC na mambo mengine ya kimataifa. Kipindi hiki kitaimulika Tanzania kwenye mikutano ya kimataifa, ukiwemo mchango wa Diaspora wa Tanzania, na wakati huo huo kuangazia fursa mbalimbali za kimataifa kwa Watanzania kuzichangamkia.

Kipindi hiki kitarushwa kwenye local channels za TV za Tanzania, DSTV, Star Times na kwenye online media.

Mimi kama Mtanzania Mzalendo, ninaumia sana kila ninapoona diaspora wa wenzetu wanafanya mambo makubwa ya kuonekanika, na kujiuliza Diaspora wetu wanafanya nini?, mbona hatuwaoni?, hivyo napenda kuona Tanzania tunafaidika na mchango wa wana diaspora wetu wenye exposure kubwa huko walipo, kuitumia kulisaidia taifa letu kisiasa, kiuchumi cha kijamii.

Paskali
Rejea za Mwandishi Kuhusu Diaspora
Sijalisoma andiko lote lakini kwa ufupi, sidhani kama kuna diaspora ambae ana akili za kujionesha Tanzania, ili iweje?

Sifahamu kama kuna diaspora ambae anaishi vizuri kisheria hajafanya kitu nyumbani.

Kuna diaspora wengi sana, tena sana, ambao wamejiamulia huko nje walipo ndiyo kwao. Tanzania patabaki kuwa asili yake.

Sheria za Tanzania za kuzuwia uraia pacha zimewafanya diaspora wengi wadhulumiwe na ndugu, jamaa na marafiki mpaka ikawakatisha tamaa kufanya lolote la maana Tanzania.

Kwa wengi, sisemi wote, kama mwenyewe haupo Tanzania, kuwekeza Tanzania imefikia kuwa kama mtu kuchukuwa pesa kuzimwaga shimo la choo.
 
Kitendo cha serikali kuzuia uraia pacha ni kama kuwafungia milango raia wa kitanzania waliochukua uraia wa nchi nyingine.
 
Wanabodi,

Bado niko hapa nchini Marekani kwa ziara binafsi, nimejitahidi kujichanganya na baadhi ya wana diaspora wa Tanzania walioko nchini Marekani, na kujiuliza jee wana Dispora wetu, wanafanya nini cha kueleweka na cha kuonekanika?.

Nimejitahidi kuwasiliana na kile chama cha DICOTA, sikubahatika kupata ushirikiano mzuri, ila nitaendelea kuwatafuta Diaspora wetu waliofanikiwa Marekani, wanafanya nini, na hayo mafanikio yao, yanaifaidia vipi nchi yao ya Tanzania?.

Kwa kupitia juhudi binafsi, nimefanikiwa kumuona dada mmoja wa Kitanzania, aliyehamia Marekani, mwaka 1999, na yuko kule mpaka leo. Huyu dada, naomba nisimtaje jina kwasababu sikumwambia kuwa nitaandika. Nime note Diaspora wa Tanzania waliofanikiwa hapa nchini Marekani, hawapendi kutajwa au kuandikwa wanafanya nini Marekani.

Huyu Dada ni mmiliki wa kampuni inayo fanya biashara ya huduma, services industry, ameajiri watu zaidi ya 50, kila mwezi anawalipa mishahara ya zaidi ya milioni 500.

Dada kanikaribisha kwake, ana kaa mtaa wa kitajiri, anamiliki nyumba, kubwa ya ghorofa tatu na ana magari 5 ya kifahari, ikiwemo Benzi ya G Wagon na gari ya Kimarekani ya Tesla inayotumia umeme. Hesabu ya haraka haraka ya thamani ya magari ni zaidi ya Shilingi Bilioni 1 ya Kitanzania.

Huu ni mfano mmoja tuu wa Mtanzania aliyefanikiwa Marekani, ametoa ajira kwa watu, na kutengeneza faida kubwa. Nilipomuuliza kwanini asiwekeze Tanzania, alinijibu anasubiria uraia pacha, ndipo aje kuwekeza Tanzania.

Imetokea tuu mimi ninamfahamu huyu Dada, mpaka kule kijijini kwao, Sanya Juu Moshi, ambako mimi nimefika, na kabla sijakwenda Marekani, nilipita hapo kwao Sanya, sasa hali niliyoiona ya umasikini wa hapo kijijini kwao, nikilinganisha na maisha ya kitajiri na kifahari anayoishi Marekani, ni mbingu na nchi!.

Hivyo huu ni wito kwa serikali yetu kuharakisha mkakati wa uraia pacha, ili Diaspora wa Tanzania waliofanikiwa ughaibuni, waje kuwekeza nyumbani Tanzania na kurudisha shukrani nyumbani Tanzania na sio kupiga tuu mapicha kurungishia mandinga yao makali ya ma G-Wagon na ma Tesla!.

Mtu Mtanzania ana magari matano ya kifahari, nchini Marekani, anaendesha kwa kubadilisha tuu magari, halafu ile hospitali ya Kibon’goto pale Sanya, kuna wamama wajawazito, wanajifungulia chini kwa kukosa, kitanda, ile G-Wagon moja tuu, ingejaza vitanda hospitali nzima, au ma deski shule nzima!.

Nimetembelea maeneo mbalimbali ya Marekani labda nitaona mafanikio ya kuonekanika ya Diaspora wa Tanzania, zaidi ya huyu dada kunikaribisha kwake, sikufanikiwa kuona kitega uchumi chochote cha Mtanzania nchini Marekani, kila rais wetu akija Marekani ni kukutana na Watanzania waishio Marekani, na kubadilisha mawazo tuu, Rais wa Kenya akija Marekani ni anafungua miradi ya Diaspora wa Kenya.

Muda aliokuja Marekani, huyu mdada wa Tanzania, ule mwaka 1999, ni muda huo Mkenya Kevin Onyona, alihamia Marekani, na kuajiriwa na Home Depot, kampuni ya kimataifa ya uboreshaji wa nyumba ya Marekani. Sasa hivi Kevin ni mmiliki ya migahawa ya Swahili Village ambayo ni mojawapo ya mikahawa bora zaidi ya vyakula vya Kiafrika nchini Marekani.

Kevin Onyona alianzisha mlolongo huo mwaka wa 2016, na leo inajivunia migahawa mitatu. Miaka sita baadaye, ametumia migahawa yake kujenga uhusiano halisi kati ya utamaduni wa Kiafrika na dunia nzima. Mkahawa mkuu wa Swahili Village oko Rhode Island Ave, Beltsville. Migahawa mingine miwili iko Washington DC na New Jersey. Mgahawa wa Washington DC ulifunguliwa na aliyekuwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kiongozi gani wa Kitanzania aliwahi kufungua mradi wowote wa Diaspora wa Tanzania nje ya Nchi?

Wito kwa Diaspora wetu, najua kuna uwezekano kuna mambo makubwa mazuri ya kuonekanika Diaspora wa Tanzania wanafanya, lakini hatuyaoni na hatuyajuo, hivyo natoa wito kwa Diaspora wetu, anekanikeni basi, inaumiza kila siku unaona diaspora wa wenzetu, na kujiuliza diaspora wetu wako wapi na wanafanya nini?.

Sasa mimi mwandishi wakp wa habari na mtangazaji wa kujitegemea, Pascal Mayalla, , anayeandaa vipindi vya TV, Redio, makala magazetini na kwenye mitandao ya kijamii, nikifanya kazi kupitia kampuni ya PPR, www.ppr.co.tz, ambayo sasa imetua rasmi nchini Marekani kwa kufungua ofisi, nimejotolea kuandaa vipindi vya mchango wa diaspora wa Tanzania kwa maendeleo ya taifa.

Kipindi Kipya cha TAK
TAK ni kipindi kipya cha TV chenye lengo la kuiangazia Tanzania Kitaifa, Kikanda na Kimataifa kuhusu mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, ambayo yanaihusu Tanzania kwenye medani za kimataifa, kama issues za Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola, issues za kikanda na kimataifa, AU, SADC, AfCFTA, Bunge la Afrika, Bunge la EAC, Jumuiya ya Africa Mashariki, EAC na mambo mengine ya kimataifa. Kipindi hiki kitaimulika Tanzania kwenye mikutano ya kimataifa, ukiwemo mchango wa Diaspora wa Tanzania, na wakati huo huo kuangazia fursa mbalimbali za kimataifa kwa Watanzania kuzichangamkia.

Kipindi hiki kitarushwa kwenye local channels za TV za Tanzania, DSTV, Star Times na kwenye online media.

Mimi kama Mtanzania Mzalendo, ninaumia sana kila ninapoona diaspora wa wenzetu wanafanya mambo makubwa ya kuonekanika, na kujiuliza Diaspora wetu wanafanya nini?, mbona hatuwaoni?, hivyo napenda kuona Tanzania tunafaidika na mchango wa wana diaspora wetu wenye exposure kubwa huko walipo, kuitumia kulisaidia taifa letu kisiasa, kiuchumi cha kijamii.

Paskali
Rejea za Mwandishi Kuhusu Diaspora
Mambo ya kufuatiliana muangamize familia za walio nje ndio kikwazo. Nchi yetu ni ya kidwanzi sana.
Mikoani kuna Maendeleo ya kimyakimya Mkuu sio lazima wajiunge na hizo jumuiya fake za kuchunguza watu.
Wewe Fanya lililokupeleka mengine waachie wenyewe kha! Tuache kuchunguzana tuta Barikiwa ni hivyo tu!
 
Ahsante sana Kwa majibu yaliyoenda mbali zaidi ya matarajio yangu Kaka.
Asante
Kama mtizamo wa serikali hautabadiliia inavyowachukulia diaspora, sitegemei wao watahangaika au kujishughulisha Kwa chochote kinachowahusisha wao na serikali.
Serikali ni yetu tuieleze tunataka nini
Ni kama tayari serikali yetu ilishaweka wazi kwamba haiwakumbatii wala kuwathamini hawa watu, ndio maana wengi wamehanfaika wanavyojua wao hadi kufikia hapo walipo.
Serikali sasa inajali
Huenda hizi juhudi zako zikabadili upepo siku za usoni,
Tuombe uzima
lakini Kwa Sasa, hili ni jambo gumu sana kutekelezeka.
Ni kweli, tena MFA na balozi zetu, unatuma barua, haujibiwi, nitawabasa huko mbele ya safari, ngoja nikiisha vuka mto!. Wanajisahau sana hawajui hiyo mishahara yao, tunawalipa sisi ni fedha zetu, tumewaajiri watutumikie.
Aidha nikupongeze Kwa hatua uliyopiga kwenye eneo lako la kazi, kupanua wigo na kuwa na malengo makubwa
Asante
African man, hongera sana.
Hii African man bado tunasumbuana na kanisa langu Katoliki, hakuna popote kwenye Bible Mungu kakataza wake wengi, hiyo ya mke mmoja, kwa vile wenzetu wazungu uwezo wao ndio huo, sasa wanalazimisha wote tuwe hivyo!, "Pongezi Rais Magufuli Kuwa Mkweli Daima. Tuanzishe Church of Africa, Tuoe Wake Wengi, Tuzae Watoto Wengi?"
P
 
Mambo ya kufuatiliana muangamize familia za walio nje ndio kikwazo. Nchi yetu ni ya kidwanzi sana.
Mikoani kuna Maendeleo ya kimyakimya Mkuu sio lazima wajiunge na hizo jumuiya fake za kuchunguza watu.
Wewe Fanya lililokupeleka mengine waachie wenyewe kha! Tuache kuchunguzana tuta Barikiwa ni hivyo tu!
Duh...!, vipi majirani zetu hawa Diaspora wa Kenya wafanya makubwa Marekani. Sisi Diaspora Wetu wanafanya nini cha kuonekana huko walipo? kuuliza diaspora wetu wanafanya nini ni kuwachunguza?.

P
 
Ukimya wa watu una sababu
Elewa hivyo!
Hilo nalielewa sana na kuliheshimu sana hili jambo la the right to privacy
Wewe endelea kupigania mkate wako na familia yako ya wenyewe hayakuhusu Mkuu
Mkate wangu ni kuonyeshea wengine wanafanya nini, niko hapa wiki ya pili sasa, my time yangu hapa is up, natakiwa kupeleka program hewani ili mkate wangu uje mezani, mpaka leo hakuna cha kuonyesha!, au kuna ukweli diaspora wetu hawana cha kuonekanika?.
P
 
Hilo nalielewa sana na kuliheshimu sana hili jambo la the right to privacy

Mkate wangu ni kuonyeshea wengine wanafanya nini, niko hapa wiki ya pili sasa, my time yangu hapa is up, natakiwa kupeleka program hewani ili mkate wangu uje mezani, mpaka leo hakuna cha kuonyesha!, au kuna ukweli diaspora wetu hawana cha kuonekanika?.
P
Watu wameendeleza vijijini kwao
Watu wamejenga shule vitu o vya Afya barabara hawahitaji kujitangaza Mkuu.
Tusiwapangie watu maisha

Mtafute pesa ni mkimya mhongwa pesa kelele nyiiiingi..
 
Back
Top Bottom