Hatimaye Dickson Maimu ambaye alikuwa CEO wa RITA na ambaye kwa muda wote yeye na Jack Gotham walikuwa wanajiandaa na mradi huu mkubwa amepewa tender yeye baada ya kupelekwa kwenye mradi huo toka RITA.Kumbukumbu zaonyesha kwamba Maimu na Jack ni wale wale na kwa tabia na uzoefu wa Maimu kuna kila aina ya uozo kwenye hili .Maimu ambaye alikuwa pale RITA alifanikiwa kuweka ukoo mzima katika ofisi za RITA na hata wamejazana hapo leo ameshinda kinyemela tender ikiwa inasemekana kwamba bado ni Jack Gotham behind baada ya kuondolewa kwa magazeti kulia lia lakini JK ame kubali tena tender iende kwa akina Jack kupitia Maimu ambaye sasa inaonyesha kashinda tender .Habari hizi nimezipata muda huu ila naomba mwenye nazo kwa undani na tujue who is behind the whole move on this movie.
Dickson Maimu alikuwa Mkurugenzi wa moja za Idara za Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Nafasi
Ya CEO wa RITA ilitangazwa magazetini, wenye sifa waliomba akiwemo huyo Maimu. Vetting kubwa ilifanyika na Maimu akashinda tatizo liko wapi?.
Mradi wa National ID ulipoiva ikaonekana anahitajika mtu mwenye sifa na uwezo wa kusimamia. Mr. Maimu ikaonekana anafaa akaondolewa RITA, akapewa mradi.
Tenda ya National ID ilitangazwa magazetini, makampuni yenye sifa yakaomba akiwemo huyo Gotham. Kwa vile National ID ni mradi nyeti unaogharimu mabilioni ya fedha, lazima mchakato ulikuwa makini. Sasa kama Gotham kashinda kihalali, what is a problem?.
Kama Maimu kapewa ulaji na hana uwezo, hiyo ni issue valid au kama Gotham hana uwezo, yeye ni middle men tuu kama mradi wa Rada na Gulf Stream.
Rada serikali iliambiwa na kelele zimepigwa sana hatimaye Radar imenunuliwa, hata kama saa hizi haifanyi kazi, biashara 'safi' ilifanyika na malipo 'halali' yameshalipwa, tatizo nini?,
Ndege ya rais ni vivyo hivyo, kelele zimepigwa, ndege imenunuliwa, hata kama hairuki, malipo 'halali' yameshalipwa, what is the problem?.
Ndivyo itakavyokuwa kwa mradi wa Vitambulisho vya kitaifa, vitatengenezwa na waTanzania watapata National ID. Malipo 'halali' yatalipwa, where is the problem?,