Red black
JF-Expert Member
- Nov 29, 2019
- 5,962
- 17,648
DahWow!
Alikuwa anapenda sana kuolewa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
DahWow!
Alikuwa anapenda sana kuolewa.
Sisi binadamu ni wenye kusahau hivyo ni wajibu wetu kukumbushana......
Aliyewahi kufa akaja kuhadithia kuhusu hiyo adhabu ya kaburi ni Nani? Na MTU akishakufa maumivu anayasikia kwenye nini maana MWILI tayari unaoza!Ukifa utajua tu
salum?Huyu ndio aliolewa na yule shehe njaa wakaachana?
KUNA LA KUJIFUNZA KWA MAISHA YA MWANADAMU HAPA DUNIANI KWAMBA NI UBATILI MTUPU !
Hekima ya mfalme Selemani kutoka kitabu cha MHUBIRI sura ya 2
1 Nikauambia moyo wangu, Haya, nitakujaribu kwa njia ya furaha basi ujifurahishe kwa anasa. Na tazama, hayo nayo yakawa ubatili.
2 Nikasema juu ya kicheko, Ni wazimu; na juu ya furaha, Yafaa nini?
3 Moyoni mwangu nikapeleleza jinsi ya kuuburudisha mwili kwa mvinyo, na (moyo wangu ukali ukiniongoza kwa hekima) jinsi ya kushikana na upumbavu, hata niyaone yaliyo mema ya kuwafaa wanadamu, ili wayafanye hayo chini ya mbingu siku zote za maisha yao.
4 Nikajifanyizia kazi zilizo kubwa; nikajijengea nyumba; nikajipandia mashamba ya mizabibu;
5 nikajifanyizia bustani na viunga, na kuipanda humo miti yenye matunda ya kila namna;
6 nikajifanyizia birika za maji, ya kuunyweshea mwitu mlimopandwa miti michanga.
7 Nami nikanunua watumwa na wajakazi, nikawa na wazalia nyumbani mwangu; tena nikawa na mali nyingi za ng'ombe na kondoo, kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu;
8 tena nikajikusanyia fedha na dhahabu, na tunu za kifalme na za kutoka katika majimbo. Nikajipatia waimbaji, waume kwa wake, nao wale ambao wanadamu wanawatunuka, masuria wengi sana.
9 Basi nikawa mkuu, nikaongezeka kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; pia hekima yangu nikakaa nayo.
10 Wala sikuyanyima macho yangu cho chote yalichokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yo yote; maana moyo wangu ulifurahi kwa sababu ya kazi yangu yote, na hii ilikuwa sehemu yangu katika kazi yangu yote.
11 Kisha nikaziangalia kazi zote zilizofanywa kwa mikono yangu, na taabu yote niliyotaabika katika kuzitenda; na tazama, yote ni ubatili na kujilisha upepo, wala faida hakuna chini ya jua.
12 Nikageuka ili kuipambanua hekima, na wazimu na upumbavu. Kwa maana mtu amfuataye mfalme afanye nini? Lilo hilo tu lililokwisha kufanywa.
13 Ndipo nilipoona ya kuwa kweli hekima hupita upumbavu, kwa kadiri nuru ipitavyo giza;
14 macho yake mwenye hekima yamo kichwani mwake, lakini mpumbavu huenda gizani; ila hata hivyo nikatambua ya kwamba ni tukio moja la mwisho liwapatalo wote sawasawa.
15 Nikasema moyoni mwangu, Kama limpatavyo mpumbavu, ndivyo litakavyonipata mimi nami; basi, kwa nini nikawa na hekima zaidi? Nikasema moyoni mwangu ya kuwa hayo nayo ni ubatili.
16 Maana hakuna kumbukumbu la milele la mwenye hekima, wala la mpumbavu; kwa sababu siku zijazo wote pia watakuwa wamekwisha kusahauliwa. Na mwenye hekima, jinsi gani anavyokufa sawasawa na mpumbavu!
17 Basi, nikauchukia uhai; kwa sababu kazi inayotendeka chini ya jua ilikuwa mbaya kwangu; yaani, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo.
18 Nami nikaichukia kazi yangu yote niliyojishughulisha nayo chini ya jua; maana sina budi kumwachia yeye atakayenifuata.
19 Naye ni nani ajuaye kama huyo atakuwa mwenye hekima au mpumbavu? Hata hivyo atatawala juu ya kazi yangu yote niliyojishughulisha nayo, ambamo ndani yake mimi nimeonyesha hekima chini ya jua. Hayo nayo ni ubatili.
20 Kwa hiyo nikageuka kukata tamaa moyoni mwangu juu ya kazi yangu yote niliyojishughulisha nayo chini ya jua.
21 Maana kuna mtu ambaye kazi yake ni kwa hekima, na kwa maarifa, na kwa ustadi; naye atamwachia mtu asiyeshughulika nayo kuwa sehemu yake. Hayo tena ni ubatili, nayo ni baa kuu.
22 Kwa maana mtu hupata nini kwa kazi yake yote, na kwa juhudi ya moyo wake alivyojitahidi chini ya jua?
23 Kwa kuwa siku zake zote ni masikitiko, na kazi yake ni huzuni; naam, hata usiku moyoni mwake hamna raha. Hayo nayo ni ubatili.
24 Mwanadamu hapati jema kupita kula na kunywa, na kuiburudisha roho yake kwa mema katika kazi yake. Hayo nayo naliona ya kwamba hutoka mkononi mwa Mungu.
25 Kwa maana ni nani awezaye kula au kujiburudisha kuliko mimi?
26 Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo.
Inadaiwa alikuwa amelazwa kwa Matibabu Muhimbili.
Amefariki usiku wa leo.
---
TANZIA: Aliyekuwa Mtangazaji wa Kipindi cha Mashamsham cha Wasafi FM, Khadija 'Dida' Shaibu, amefariki dunia usiku wa leo Oktoba 4, 2024 wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Muhimbili
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mtangazaji mwenzake, Maulid Kitenge, kupitia mtandao wa X, Dida alikuwa amelazwa Hospitalini hapo baada ya kuugua.
Mmmh maneno gan hayo Kwa marehem si Bora yeye alkua anaolewa kuliko kuziniMwendo kaumaliza na uke wake kautendea haki kwa ndoa za kutosha.
Apumzike kwa amani.
Mambo ya MOFVifo vya ghafla hivi?
We bwana tuache Sisi, tusianze kutishana.ndio yule aliyekuwa anapenda dogodogo? au mwingine. si ndio yule alikuwa anadai ana pesa nyingi? Pole sana kwa wafiwa, ila wanadamu jueni maisha yanapita, ngono zinapita, pesa zinapita, kila kitu unachokiona kinapita, everything in this world shall fade away, cha muhimu unachotakiwa kujiuliza ni, utakapokufa utaenda wapi? motoni au uzimani? where will you spend your eternity? hilo ndio liwe swali la kujiuliza kila utakapoamka, kwasababu hujui utakufa lini. Nina uhakika, as long as alikuwa Mtanzania, alishasikia injili ya Yesu Kristo, na ninyi nyote mnaosoma hapa hakuna siku ile atasema mbele za kiti cha hukumu kwamba hakusikia habari za Yesu Kristo, wote mmeshasikia hivyo ni hiari yenu kuamua hatima ya maisha yenu ya baadaye.
Mungu awasaidie
Adhabu ya kaburi ni katika mambo ya ghaibu na Waislam tunayaamini. Sisi Waislam tunaamini kuwa kuna adhabu na neema za kaburi kwa sababu tumeambiwa hilo katika Qur'an na Mtume Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake) katuambia hilo.Aliyewahi kufa akaja kuhadithia kuhusu hiyo adhabu ya kaburi ni Nani? Na MTU akishakufa maumivu anayasikia kwenye nini maana MWILI tayari unaoza!
Mimi mwenyewe nakutegemea wewe ulete finding report kutoka eneo la tukio...Nilikuwa najua unakuja na file lake kutoka muhimbili kwa chanzo chako cha uhakika,sasa kumbe na wewe ndio unastuka!nimenyong'onyea
Au sio.Mmmh maneno gan hayo Kwa marehem si Bora yeye alkua anaolewa kuliko kuzini
Kwanini?Wow!
Alikuwa anapenda sana kuolewa.
Picha yako ukilia?Nimeliaa sanaa, baada ya kupata taarifa hii saa 1 iliyopita.
Didaa ameniumaa mnooo. [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Kabisa amepambana akaishi maisha mazuri.....na alikua anajua kujipenda, anajipeleka kutalii sehemu mbalimbali.Alikuwa ni mwanamke mpambanaji, mtu wa watu na mcheshi kupitiliza....
Alikua anapambania nini?Alikuwa ni mwanamke mpambanaji, mtu wa watu na mcheshi kupitiliza....
Ndo Dunia yetu hii.. naimani wapo ndugu na jamaa watamlea Binti yetu .Kabisa amepambana akaishi maisha mazuri.....na alikua anajua kujipenda, anajipeleka kutalii sehemu mbalimbali.
Apumzike kwa amani, namuonea huruma binti yake 🥹
Anapambana na maisha yake ili apate chochote kitu kama wewe unavyopambana kuhudumia familiar yako.Alikua anapambania nini?