Diddy anyimwa dhamana na Mahakama, alitoa ofa ya bilioni 135

Diddy anyimwa dhamana na Mahakama, alitoa ofa ya bilioni 135

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Rapa na mfanyabiashara ‘Diddy’ ameripotiwa kunyimwa dhamana baada ya kudai kuwa Hana hatia katika mashtaka ya kingono yanayomkabili na hivyo ataendelea kubaki rumande hadi pale kesi yake itakapoanza kusikilizwa.
1726641176631.png

Imeelezwa kuwa Diddy alitoa ofa ya dola milioni 50 (Tsh bilioni 136+) na kuisalimisha passport yake ili atolewe kwa dhamana lakini ombi hilo lilipigwa chini Jaji wa Mahakama ya Manhattan ‘Robyn F. Tarnofsky’.

Kwenye ofa ya dhamana hiyo Diddy aliweka nyumba yake ya Miami yenye thamani ya dola mililioni 48 pamoja na mjengo wa Mama yake wenye thamani ya dola milioni 2 ili kukamilisha kiasi alichotaja kukitoa.

Pia waendesha mashtaka waligoma kuachiwa kwa Diddy wakidai kuwa ni hatari kwa jamii.

Kumbuka jana Rapa huyu aliripotiwa kukamatwa na Maafisa Usalama wa New York kama sehemu ya Uchunguzi wa Kesi zilizofunguliwa dhidi yake kama vile kuwatumikisha mabinti wadogo kingono, udhalilishaji n.k

Pia, Soma:

==> Waendesha Mashtaka wadai nyumba ya Diddy ilikutwa na Vilainishi, Silaha, Dawa za Kulevya, Mafuta ya Watoto Chupa zaidi ya 1000
==> Diddy aomba radhi baada ya video akimpiga Cassie kusambaa
==> Mahakama yamuamuru Sean ‘Diddy’ Combs kulipa Dola Milioni 100 kwa mwanaume aliyemshtaki kwa kumnyanyasa kingono
 
Back
Top Bottom