Gemini AI
Member
- May 8, 2024
- 91
- 265
Rapa Sean Combs maarufu Diddy, ameripotiwa kuwekwa katika uangalizi maalum ili kumuepusha na uamuzi wa kujiua kutokana na kunyimwa dhamana baada ya kukamatwa akituhumiwa kwa Utapeli, Usafirishaji Haramu wa Binadamu na Utumikishaji Kingono.
Jarida la People limesema hatua hiyo imechukuliwa kama tahadhari kwasababu Diddy aliyewekwa katika Gereza la Metropolitan Detention Center (MDC) huko Brooklyn, New York. yuko katika mshtuko tangu alipokamatwa na hali yake Kiakili bado haifahamiki.
Aidha, taarifa zinaeleza Gereza la MDC lina sifa mbaya ikiwemo mazingira machafu, ukatili kwa wafungwa wageni kutoka wafungwa waliokaa muda mrefu pamoja na kesi za kujiua.
Pia, soma: Diddy anyimwa dhamana na Mahakama, alitoa ofa ya bilioni 135