Dietrich Bonhoeffer: Mchungaji Aliyemsumbua Hitler kwa Neno la Biblia

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Nilikuwa katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), maarufu kama Archbishop Mgulunde Learning Resource Center, mwanzoni mwa Novemba, nilipokutana na kitabu cha zamani kilichofichwa kimya kimya kwenye moja rafu ya maktaba: The Plot to Kill Hitler: Dietrich Bonhoeffer – Pastor, Spy, Unlikely Hero cha mwanamama Patricia McCormick. Nilipoomba kukiazima, niliambiwa kuwa “kimehifadhiwa maalum kwa ajili ya mapadri wa katoliki na wakufunzi wa masomo ya dini pekee waliopo chuoni hapo.”
images - 2025-12-19T195102.448.jpeg

Kauli hiyo haikunishawishi kwani nilihitaji kukiazima kwa siku kadhaa. Nilipiga picha ya jalada, nikaandika pembeni jina la kitabu, kisha nikaenda Amazon Kindle kujipatia uhondo.
51XnHJr39OL._AC_UF1000,1000_QL80_FMwebp_.webp

Kama haujashiba vizuri au ni jamii ya wafuasi wa Mbogamboga basi simulizi hii tamu itakuboa mapema sana, historia ya giza na hofu ya utawala wa chama cha Nazi ilipatiwa dibaji iliyoshiba kisha baadaye kupewa nafasi ya kuangaziwa kwa lugha nyepesi kabsa: Ujerumani kwa wakati huo ilikuwa ni kama mbwa aliyelowana maji na mwenye hofu, kanisa liligawanyika kati ya usaliti na ujasiri, wapo wachugaji waliofyata mkia na kuwa vibaraka wa Hitler.
0798f2eb-6f1a-4d94-ac4f-41ddd40c92c9.jpeg

Watu kama Ludwig Muller, Paul Schmidt, Martin Niemoller, pamoja na Alois Hudal walijizima data kabsa na kuunga mkono pamoja na kutoa baraka kwa unyama ambao Hitler alikuwa akifanya.
Ila katika purukushani na fujo zote kuna mchungaji mmoja aliyethubutu kusema “hapana” kwa Hitler na kutumia utimamu wake kuonesha kuwa hakuna sehemu yoyote ya neno takatifu la Biblia linalounga mkono ujinga na ushenzi wa chama cha Nazi wala mipango ya Hitler.
images - 2025-12-19T193729.514.jpeg

Alikuwa ni mchungaji ambaye hakutaka kuwa kama Mchugaji Richard Hananja, hakuwa mchungaji wa kusifu na kuimba mapambio kwenye madhabahuni; aliingia kwenye mtandao wa siri wa upinzani, akawa mchungaji, jasusi, na shahidi wa kanisa la Kilutheri.
images - 2025-12-19T193657.183.jpeg

Kitabu hiki usisome ukiwa na njaa! Usisome ukiwa unaamini kuwa kesi ya Simba kutafuna watoto wa Swala itapata suluhu na maamuzi bora mbele ya Chui kama Hakimu wa Mahakama.
images - 2025-12-19T193650.241.jpeg

Ni kitabu ambacho kilichoandikwa kwa mtindo wa kukuonesha matukio kwa ukaribu, kinaonyesha wazi jinsi baadhi ya makanisa yalivyogeuka vyombo vya propaganda, wachungaji walivyobadilika na kuwa makasuku.
hqdefault.jpg

Achana na lile kundi la kina Alois Hudal, kuna kina Jozef Tiso huku wachungaji wachache sana wakisimamia imani zao na kuzifanya kuwa silaha ya kupinga uovu, mbaya ni kuwa hata Kanisa Katoliki nao walifyata mkia na kuingia baridi ile mbaya.
images - 2025-12-19T220924.427.jpeg

Watu kama Abbot Alban Schachleiter walitia aibu sana kanisa Katoliki, huyu mwamba alikuwa akitumia salamu ya kinazi waziwazi, mpaka madhabauni na mbele ya Altare, huku pia akitumia ibada kama uwanja wa kuhalalisha ujinga wa Hitler.
5314116.jpg

Kadinali Michael von Faulhaber aliona huyu mpuuzi analeta mazoea na Altare takatifu kwa kuhubiri upuuzi wake na uchawa, hivyo akamchoma kwa Boss Kubwa, Papa Pius XI, Abbot Alban Schachleiter aliondolewa na Vatican hawakuwa na jambo jingine bali kurudi maneno yake, “ROMA LOCUTA EST; CAUSA FINITA EST”. Kisa cha Abbot Alban Schachleiter nitakileta hivi karibuni!
images - 2025-12-19T193622.854.jpeg

February 4 mwaka 1906 ikiwa ni Jumapili moja tulivu kabsa ndani ya Mji wa Breslau Ujerumani ambapo kwa sasa panatambulika kama Wroclaw, Poland alizaliwa dogo mmoja, shahidi wa imani na kanisa, wazazi wake wakiwa ni Karl Bonhoeffer na aliyeteremsha chuma duniani ni Mwanamama Paula von Hase. picha linaanza wazazi wakaona itapendeza sana kama dunia itamfahamu mtoto wao kwa majina ya Dietrich Theodor Ludwig Bonhoeffer.
51XnHJr39OL._AC_UF1000,1000_QL80_.jpg

Mwamba Bonhoeffer alikuwa mchungaji wa Kanisa la Kilutheri, mwanatheolojia mashuhuri wa mwelekeo wa neo-orthodoxy, na mpinzani shupavu wa utawala wa Adolf Hitler. Maisha yake, harakati zake pamoja na huduma yake kwa kanisa la Kilutheri yamefanya jina lake lihesabiwe leo kama la shahidi (martyr) katika baadhi ya madhehebu ya Kikristo.
images - 2025-12-19T193517.136.jpeg

Mara baada ya kupanda kwa chama cha Nazi na kuingia madarakani mwaka 1933 hali hii ilimkuta Bonhoeffer akiwa kijana mwenye kipaji kikubwa cha kitaaluma na kiroho.
images - 2025-12-19T193650.241.jpeg

Ajabu ni kwamba mwamba alikuwa hana mbili kwenye moja, alihubiri na kutafsiri andiko bila kupindisha hata silabi moja, kariba yake ilimtofautisha sana na viongozi wengine wa dini ambao walikuwa aidha ni wanafiki au makasuku.
images - 2025-12-19T193504.802.jpeg

Ukiachana na bwana mdogo, ndani ya Ujerumani pamoja na Austria kulikuwa na idadi kubwa sana ya viongozi wa dini mandazi sana waliokaa kimya na wengine kuamua kuwaunga mkono wanachama wa Nazi katika utawala mpya, tofauti kabsa na Bonhoeffer ambaye alichagua njia hatari ya kuwa mpinzani, alikuwa anajua kupiga spana haswa.
images - 2025-12-19T193753.194.jpeg

Siku mbili tu baada ya Hitler kuteuliwa kuwa Kansela, Bonhoeffer aliandaa mahubiri yake na kumuomba Roho Mtakatifu nguvu kisha alikwenda kutoa hotuba redioni akiionya Ujerumani dhidi ya kumwabudu Führer kama sanamu ya kisiasa.
images - 2025-12-19T193846.626.jpeg

Hotuba hiyo ilikatizwa ghafla – ishara ya kwanza ya chuki ambayo utawala wa Nazi ungeelekeza kwake. Ila kabla hawakazima hotuba yake mwamba akawahasa watu wakasome 2 Wafalme 17:38, huku akiwadokezea na andiko jingine takatifu kutoka Kutoka 20:3-17.
images - 2025-12-19T193622.854.jpeg

Kwa mujibu wa Ferdinand Schlingensiepen katika kitabu chake cha Dietrich Bonhoeffer: Martyr, Thinker, Man of Resistance cha mwaka 2012, Bonhoeffer aliona mapema kuwa Nazism haikuwa tu mfumo wa kisiasa wa ovyo na dhalimu bali pia uzushi wa kidini ndani ya Ujerumani.
images - 2025-12-19T193657.183.jpeg

Wanachama wa Nazi, kupitia vuguvugu la Deutsche Christen, walijaribu kuoanisha pamoja na kufungamanisha dini ya Ukristo na utaifa na ukabila, hata kufikia hatua ya kutaka kuondoa kabsa Agano la Kale kwa sababu tu ya asili yake ya Kiyahudi. Kwa Bonhoeffer, hili lilikuwa shambulio la moja kwa moja dhidi ya Injili yenyewe. Mwamba akaona hawa wameingia choo cha kike, acha awanyooshe barabara.
images - 2025-12-19T193517.136.jpeg

Ndani ya Kanisa la Kiprotestanti la Ujerumani, Bonhoeffer alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa Bekennende Kirche (Kanisa la Kukiri), lililokataa utiifu wa aina yoyote kwa serikali ya Hitler katika masuala ya imani pamoja na uongozi. Ngoma ikazidi kuwa ngumu, dakika ya 30 bado ubao unasoma bila bila.
images - 2025-12-19T193504.802.jpeg

Wazee wa kanisa wakaweka kikao chao na kuja na Azimio la Barmen la mwaka 1934, lililoandikwa na Karl Barth na kuungwa mkono kwa 100% na Bonhoeffer, lilisisitiza kwamba Kristo – si Führer – na Kristo ndiye kichwa pekee cha Kanisa mwisho wa nukuu.
images - 2025-12-19T193729.514.jpeg

Bonhoeffer akaamua kukazia maumivu kwa chawa na vibaraka wa Hitler akawapiga na neno kutoka 1 Wakorintho 8:6 pamoja na Waefeso 4:6-8. Acha kabsa moto uliwaka vifuani vya maafisa wa Nazi waliokuwa ndani ya Wolfsschanze pamoja na Adlerhorst. Maneno na msimamo huu ulimfanya Bonhoeffer awe adui wa wazi wa dola ya Nazi.
images-53.jpeg

Chuki ya wanachama wa Nazi dhidi Bonhoeffer haikubaki kwenye kejeli za maneno pekee. Kwanza kabsa alipigwa marufuku kufundisha, kuchapisha, na hatimaye kusafiri kwa uhuru kutoka eneo moja ndani ya Ujerumani. Mwamba akaona hawezi kutuia kizembe namna hiyo, akafungua Seminari ya siri na kuipatia jina la Finkenwalde, aliyokuwa akiiongoza kwa ajili ya kuwafundisha wachungaji wa Kanisa la Kukiri, ilivamiwa na Gestapo na kufungwa.
5314116.jpg

Hapo ndipo Bonhoeffer aliandika kitabu chake maarufu The Cost of Discipleship cha mwaka 1937, ambacho mwaka 1989 Edwin Robertson alikitaja kama wito wa Ukristo wa “neema ya gharama” (costly grace)—imani inayodai utii halisi hata kama gharama yake ni mateso au kifo.
images - 2025-12-19T193622.854.jpeg

Kadiri vita vya pili vya dunia vilivyozidi, Bonhoeffer alikabiliwa na mgogoro mkubwa: je, Mkristo anaweza kushiriki katika njama ya kumuua dikteta? Kupitia shemeji yake Hans von Dohnányi, mzee baba Bonhoeffer aliingia katika mtandao wa upinzani ndani ya Abwehr (majasusi wa kijeshi ndani ya Ujerumani).
images - 2025-12-19T193504.802.jpeg

Alitumia nafasi hiyo kusaidia Wayahudi kutoroka na pia kuwasiliana na maafisa wa Uingereza, akiwemo Askofu George Bell wa Chichester, kama alivyoeleza Kenneth Slack mwaka 1971. Wanahistoria wa Ujerumani kama vile; Fritz Fischer hudai kuwa mzee baba Bonhoeffer alikuwa agent wa Abwehr.
images - 2025-12-19T193729.514.jpeg

Ingawa alikuwa mpinzani wa vurugu kwa misingi ya imani, Bonhoeffer alikiri kuwa wakati mwingine “mtu anayewajibika” analazimika kuchukua hatia juu yake mwenyewe kwa ajili ya kizazi kijacho.
images - 2025-12-19T193753.194.jpeg

Mwanzoni lengo la msingi la Bonhoeffer lilikuwa ni kuzuia Nazi wasiharibu kanisa ila taratibu aliona kuna haja kubwa ya kulinda kila pembe kwani kila sehemu Nazi walitaka kupeleka nadhari ya kipuuzi ambazo hazikuwa na msingi wowote. Mwaka jana mwandishi wa kitabu cha The Sovereign Human Being, Prof Valentin Jeutner alieleza kinaganga jinsi Bonhoeffer alivyovuka mipaka ya nadharia na kuingia kwenye maamuzi halisi ya kimaisha. Ni kama Bonhoeffer aliona jamaa hawahitaji mahubiri pekee pia na mapigo kama Farao.
images - 2025-12-19T193846.626.jpeg

Kukamatwa kwake mwaka 1943 ulikuwa mwanzo wa safari yake ya mwisho, maana aliwatoa jasho vya kutosha Nazi. Akiwa gerezani huko Tegel, Bonhoeffer alitumia nafasi hiyo kuandika barua na tafakari zilizojaa matumaini, mashaka, na imani, zilizokusanywa baadaye katika Letters and Papers from Prison.
229234fa7584fe498e96d32cd830879b.jpg

Humo, alizungumza juu ya “Ukristo usio wa kidini,” akitafakari mustakabali wa imani katika dunia ya kisekula, mahala ambapo serikali haifungamani na dini yoyote.
images - 2025-12-19T193657.183.jpeg

Baada ya kugunduliwa kwa nyaraka za Abwehr mwaka 1945, Hitler alipandwa na hasira kwa kiwango cha 5G, na ili kukomesha kabsa roho hii ya ajabu ya mtu kama Bonhoeffer aliamuru kunyongwa kwa washiriki wote wenye mahusihano na Abwehr. Bonhoeffer alinyongwa akiwa uchi alfajiri ya tarehe 9 Aprili 1945.
images - 2025-12-19T193504.802.jpeg

Leo, Bonhoeffer anatambuliwa na makanisa mengi kama shahidi. Kanisa la Anglikana, Kanisa la Kilutheri Marekani (ELCA), na Kanisa la Methodisti linampa heshima na kumkumbuka rasmi kama mtu aliyekufa kwa ushuhuda wa imani. Sababu si tu kifo chake, bali maisha yake yote: aliishi kile alichohubiri, aliishi na roho mtakatifu ambaye alimuongoza kusema ukweli bila kupindisha maneno.
images - 2025-12-19T193517.136.jpeg

Katika kitabu cha Bonhoeffer’s Black Jesus kilichoandikwa na Reggie L. Williams mwaka 2014 kinasimulia ujasiri wa ajabu wa Bonhoeffer ambaye aliutazama Ukristo kama tumaini na nguvu kubwa sana ambayo haitoki kwenye chama cha siasa wala kwenye mikono ya serikali.
images - 2025-12-19T193622.854.jpeg

Kwa kifupi, Dietrich Bonhoeffer hakuuawa kwa bahati mbaya ya vita, bali alikufa kwa sababu alikataa kuisaliti Injili, hakukubali kubadilisha maandiko ili baadhi ya watu wafurahie na kucheka mpaka MOLARS NA PREMOLARS zionekane. Katika dunia ambayo mara nyingi imani hutumiwa kuhalalisha nguvu na ukatili, Bonhoeffer anabaki kuwa kumbukumbu hai kwamba Ukristo wa kweli unaweza – na wakati mwingine lazima – kusimama dhidi ya dola, hata kama gharama yake ni maisha yenyewe.
images-53.jpeg

Alikuwa tofauti kabsa na wapuuzi kama, Alois Hudal, Jozef Tiso, Abbot Alban Schachleiter, Gerhard Kittel ambapo walikubali kulamba nyayo za Hitler na kuhubiri vitu vice versa, huku wakiwa mstari wa mbele kueneza chuki na propaganda za kijinga ndani ya makanisa.
images - 2025-12-19T193622.854.jpeg

Pumzika kwa amani mwamba, Dunia itaendelea kuenzi kazi yako tukufu, jina lako Dietrich Theodor Ludwig Bonhoeffer limeandikwa kwa wino wa dhahabu katika historia ya kanisa la Kilutheri. Kwa hakika wito wako uliutendea haki kwa 100%, ulisema na kuhubiri ukweli kama ambayo ulifundishwa na Frank Fisher kwenye mitaa ya Harlem pale katika kanisa la Abyssinian Baptist Church.
 
Nilikuwa katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), maarufu kama Archbishop Mgulunde Learning Resource Center, mwanzoni mwa Novemba, nilipokutana na kitabu cha zamani kilichofichwa kimya kimya kwenye moja rafu ya maktaba: The Plot to Kill Hitler: Dietrich Bonhoeffer – Pastor, Spy, Unlikely Hero cha mwanamama Patricia McCormick. Nilipoomba kukiazima, niliambiwa kuwa “kimehifadhiwa maalum kwa ajili ya mapadri wa katoliki na wakufunzi wa masomo ya dini pekee waliopo chuoni hapo.”
View attachment 3517914
Kauli hiyo haikunishawishi kwani nilihitaji kukiazima kwa siku kadhaa. Nilipiga picha ya jalada, nikaandika pembeni jina la kitabu, kisha nikaenda Amazon Kindle kujipatia uhondo.
View attachment 3517916
Kama haujashiba vizuri au ni jamii ya wafuasi wa Mbogamboga basi simulizi hii tamu itakuboa mapema sana, historia ya giza na hofu ya utawala wa chama cha Nazi ilipatiwa dibaji iliyoshiba kisha baadaye kupewa nafasi ya kuangaziwa kwa lugha nyepesi kabsa: Ujerumani kwa wakati huo ilikuwa ni kama mbwa aliyelowana maji na mwenye hofu, kanisa liligawanyika kati ya usaliti na ujasiri, wapo wachugaji waliofyata mkia na kuwa vibaraka wa Hitler.
View attachment 3517915
Watu kama Ludwig Muller, Paul Schmidt, Martin Niemoller, pamoja na Alois Hudal walijizima data kabsa na kuunga mkono pamoja na kutoa baraka kwa unyama ambao Hitler alikuwa akifanya.
Ila katika purukushani na fujo zote kuna mchungaji mmoja aliyethubutu kusema “hapana” kwa Hitler na kutumia utimamu wake kuonesha kuwa hakuna sehemu yoyote ya neno takatifu la Biblia linalounga mkono ujinga na ushenzi wa chama cha Nazi wala mipango ya Hitler.
View attachment 3517924
Alikuwa ni mchungaji ambaye hakutaka kuwa kama Mchugaji Richard Hananja, hakuwa mchungaji wa kusifu na kuimba mapambio kwenye madhabahuni; aliingia kwenye mtandao wa siri wa upinzani, akawa mchungaji, jasusi, na shahidi wa kanisa la Kilutheri.
View attachment 3517925
Kitabu hiki usisome ukiwa na njaa! Usisome ukiwa unaamini kuwa kesi ya Simba kutafuna watoto wa Swala itapata suluhu na maamuzi bora mbele ya Chui kama Hakimu wa Mahakama.
View attachment 3517926
Ni kitabu ambacho kilichoandikwa kwa mtindo wa kukuonesha matukio kwa ukaribu, kinaonyesha wazi jinsi baadhi ya makanisa yalivyogeuka vyombo vya propaganda, wachungaji walivyobadilika na kuwa makasuku.
View attachment 3517922
Achana na lile kundi la kina Alois Hudal, kuna kina Jozef Tiso huku wachungaji wachache sana wakisimamia imani zao na kuzifanya kuwa silaha ya kupinga uovu, mbaya ni kuwa hata Kanisa Katoliki nao walifyata mkia na kuingia baridi ile mbaya.
View attachment 3517918
Watu kama Abbot Alban Schachleiter walitia aibu sana kanisa Katoliki, huyu mwamba alikuwa akitumia salamu ya kinazi waziwazi, mpaka madhabauni na mbele ya Altare, huku pia akitumia ibada kama uwanja wa kuhalalisha ujinga wa Hitler.
View attachment 3517917
Kadinali Michael von Faulhaber aliona huyu mpuuzi analeta mazoea na Altare takatifu kwa kuhubiri upuuzi wake na uchawa, hivyo akamchoma kwa Boss Kubwa, Papa Pius XI, Abbot Alban Schachleiter aliondolewa na Vatican hawakuwa na jambo jingine bali kurudi maneno yake, “ROMA LOCUTA EST; CAUSA FINITA EST”. Kisa cha Abbot Alban Schachleiter nitakileta hivi karibuni!
View attachment 3517927
February 4 mwaka 1906 ikiwa ni Jumapili moja tulivu kabsa ndani ya Mji wa Breslau Ujerumani ambapo kwa sasa panatambulika kama Wroclaw, Poland alizaliwa dogo mmoja, shahidi wa imani na kanisa, wazazi wake wakiwa ni Karl Bonhoeffer na aliyeteremsha chuma duniani ni Mwanamama Paula von Hase. picha linaanza wazazi wakaona itapendeza sana kama dunia itamfahamu mtoto wao kwa majina ya Dietrich Theodor Ludwig Bonhoeffer.
View attachment 3517928
Mwamba Bonhoeffer alikuwa mchungaji wa Kanisa la Kilutheri, mwanatheolojia mashuhuri wa mwelekeo wa neo-orthodoxy, na mpinzani shupavu wa utawala wa Adolf Hitler. Maisha yake, harakati zake pamoja na huduma yake kwa kanisa la Kilutheri yamefanya jina lake lihesabiwe leo kama la shahidi (martyr) katika baadhi ya madhehebu ya Kikristo.
View attachment 3517929
Mara baada ya kupanda kwa chama cha Nazi na kuingia madarakani mwaka 1933 hali hii ilimkuta Bonhoeffer akiwa kijana mwenye kipaji kikubwa cha kitaaluma na kiroho.
View attachment 3517926
Ajabu ni kwamba mwamba alikuwa hana mbili kwenye moja, alihubiri na kutafsiri andiko bila kupindisha hata silabi moja, kariba yake ilimtofautisha sana na viongozi wengine wa dini ambao walikuwa aidha ni wanafiki au makasuku.
View attachment 3517930
Ukiachana na bwana mdogo, ndani ya Ujerumani pamoja na Austria kulikuwa na idadi kubwa sana ya viongozi wa dini mandazi sana waliokaa kimya na wengine kuamua kuwaunga mkono wanachama wa Nazi katika utawala mpya, tofauti kabsa na Bonhoeffer ambaye alichagua njia hatari ya kuwa mpinzani, alikuwa anajua kupiga spana haswa.
View attachment 3517923
Siku mbili tu baada ya Hitler kuteuliwa kuwa Kansela, Bonhoeffer aliandaa mahubiri yake na kumuomba Roho Mtakatifu nguvu kisha alikwenda kutoa hotuba redioni akiionya Ujerumani dhidi ya kumwabudu Führer kama sanamu ya kisiasa.
View attachment 3517920
Hotuba hiyo ilikatizwa ghafla – ishara ya kwanza ya chuki ambayo utawala wa Nazi ungeelekeza kwake. Ila kabla hawakazima hotuba yake mwamba akawahasa watu wakasome 2 Wafalme 17:38, huku akiwadokezea na andiko jingine takatifu kutoka Kutoka 20:3-17.
View attachment 3517927
Kwa mujibu wa Ferdinand Schlingensiepen katika kitabu chake cha Dietrich Bonhoeffer: Martyr, Thinker, Man of Resistance cha mwaka 2012, Bonhoeffer aliona mapema kuwa Nazism haikuwa tu mfumo wa kisiasa wa ovyo na dhalimu bali pia uzushi wa kidini ndani ya Ujerumani.
View attachment 3517925
Wanachama wa Nazi, kupitia vuguvugu la Deutsche Christen, walijaribu kuoanisha pamoja na kufungamanisha dini ya Ukristo na utaifa na ukabila, hata kufikia hatua ya kutaka kuondoa kabsa Agano la Kale kwa sababu tu ya asili yake ya Kiyahudi. Kwa Bonhoeffer, hili lilikuwa shambulio la moja kwa moja dhidi ya Injili yenyewe. Mwamba akaona hawa wameingia choo cha kike, acha awanyooshe barabara.
View attachment 3517929
Ndani ya Kanisa la Kiprotestanti la Ujerumani, Bonhoeffer alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa Bekennende Kirche (Kanisa la Kukiri), lililokataa utiifu wa aina yoyote kwa serikali ya Hitler katika masuala ya imani pamoja na uongozi. Ngoma ikazidi kuwa ngumu, dakika ya 30 bado ubao unasoma bila bila.
View attachment 3517930
Wazee wa kanisa wakaweka kikao chao na kuja na Azimio la Barmen la mwaka 1934, lililoandikwa na Karl Barth na kuungwa mkono kwa 100% na Bonhoeffer, lilisisitiza kwamba Kristo – si Führer – na Kristo ndiye kichwa pekee cha Kanisa mwisho wa nukuu.
View attachment 3517924
Bonhoeffer akaamua kukazia maumivu kwa chawa na vibaraka wa Hitler akawapiga na neno kutoka 1 Wakorintho 8:6 pamoja na Waefeso 4:6-8. Acha kabsa moto uliwaka vifuani vya maafisa wa Nazi waliokuwa ndani ya Wolfsschanze pamoja na Adlerhorst. Maneno na msimamo huu ulimfanya Bonhoeffer awe adui wa wazi wa dola ya Nazi.
View attachment 3517921
Chuki ya wanachama wa Nazi dhidi Bonhoeffer haikubaki kwenye kejeli za maneno pekee. Kwanza kabsa alipigwa marufuku kufundisha, kuchapisha, na hatimaye kusafiri kwa uhuru kutoka eneo moja ndani ya Ujerumani. Mwamba akaona hawezi kutuia kizembe namna hiyo, akafungua Seminari ya siri na kuipatia jina la Finkenwalde, aliyokuwa akiiongoza kwa ajili ya kuwafundisha wachungaji wa Kanisa la Kukiri, ilivamiwa na Gestapo na kufungwa.
View attachment 3517917
Hapo ndipo Bonhoeffer aliandika kitabu chake maarufu The Cost of Discipleship cha mwaka 1937, ambacho mwaka 1989 Edwin Robertson alikitaja kama wito wa Ukristo wa “neema ya gharama” (costly grace)—imani inayodai utii halisi hata kama gharama yake ni mateso au kifo.
View attachment 3517927
Kadiri vita vya pili vya dunia vilivyozidi, Bonhoeffer alikabiliwa na mgogoro mkubwa: je, Mkristo anaweza kushiriki katika njama ya kumuua dikteta? Kupitia shemeji yake Hans von Dohnányi, mzee baba Bonhoeffer aliingia katika mtandao wa upinzani ndani ya Abwehr (majasusi wa kijeshi ndani ya Ujerumani).
View attachment 3517930
Alitumia nafasi hiyo kusaidia Wayahudi kutoroka na pia kuwasiliana na maafisa wa Uingereza, akiwemo Askofu George Bell wa Chichester, kama alivyoeleza Kenneth Slack mwaka 1971. Wanahistoria wa Ujerumani kama vile; Fritz Fischer hudai kuwa mzee baba Bonhoeffer alikuwa agent wa Abwehr.
View attachment 3517924
Ingawa alikuwa mpinzani wa vurugu kwa misingi ya imani, Bonhoeffer alikiri kuwa wakati mwingine “mtu anayewajibika” analazimika kuchukua hatia juu yake mwenyewe kwa ajili ya kizazi kijacho.
View attachment 3517923
Mwanzoni lengo la msingi la Bonhoeffer lilikuwa ni kuzuia Nazi wasiharibu kanisa ila taratibu aliona kuna haja kubwa ya kulinda kila pembe kwani kila sehemu Nazi walitaka kupeleka nadhari ya kipuuzi ambazo hazikuwa na msingi wowote. Mwaka jana mwandishi wa kitabu cha The Sovereign Human Being, Prof Valentin Jeutner alieleza kinaganga jinsi Bonhoeffer alivyovuka mipaka ya nadharia na kuingia kwenye maamuzi halisi ya kimaisha. Ni kama Bonhoeffer aliona jamaa hawahitaji mahubiri pekee pia na mapigo kama Farao.
View attachment 3517920
Kukamatwa kwake mwaka 1943 ulikuwa mwanzo wa safari yake ya mwisho, maana aliwatoa jasho vya kutosha Nazi. Akiwa gerezani huko Tegel, Bonhoeffer alitumia nafasi hiyo kuandika barua na tafakari zilizojaa matumaini, mashaka, na imani, zilizokusanywa baadaye katika Letters and Papers from Prison.
View attachment 3517919
Humo, alizungumza juu ya “Ukristo usio wa kidini,” akitafakari mustakabali wa imani katika dunia ya kisekula, mahala ambapo serikali haifungamani na dini yoyote.
View attachment 3517925
Baada ya kugunduliwa kwa nyaraka za Abwehr mwaka 1945, Hitler alipandwa na hasira kwa kiwango cha 5G, na ili kukomesha kabsa roho hii ya ajabu ya mtu kama Bonhoeffer aliamuru kunyongwa kwa washiriki wote wenye mahusihano na Abwehr. Bonhoeffer alinyongwa akiwa uchi alfajiri ya tarehe 9 Aprili 1945.
View attachment 3517930
Leo, Bonhoeffer anatambuliwa na makanisa mengi kama shahidi. Kanisa la Anglikana, Kanisa la Kilutheri Marekani (ELCA), na Kanisa la Methodisti linampa heshima na kumkumbuka rasmi kama mtu aliyekufa kwa ushuhuda wa imani. Sababu si tu kifo chake, bali maisha yake yote: aliishi kile alichohubiri, aliishi na roho mtakatifu ambaye alimuongoza kusema ukweli bila kupindisha maneno.
View attachment 3517929
Katika kitabu cha Bonhoeffer’s Black Jesus kilichoandikwa na Reggie L. Williams mwaka 2014 kinasimulia ujasiri wa ajabu wa Bonhoeffer ambaye aliutazama Ukristo kama tumaini na nguvu kubwa sana ambayo haitoki kwenye chama cha siasa wala kwenye mikono ya serikali.
View attachment 3517927
Kwa kifupi, Dietrich Bonhoeffer hakuuawa kwa bahati mbaya ya vita, bali alikufa kwa sababu alikataa kuisaliti Injili, hakukubali kubadilisha maandiko ili baadhi ya watu wafurahie na kucheka mpaka MOLARS NA PREMOLARS zionekane. Katika dunia ambayo mara nyingi imani hutumiwa kuhalalisha nguvu na ukatili, Bonhoeffer anabaki kuwa kumbukumbu hai kwamba Ukristo wa kweli unaweza – na wakati mwingine lazima – kusimama dhidi ya dola, hata kama gharama yake ni maisha yenyewe.
View attachment 3517921
Alikuwa tofauti kabsa na wapuuzi kama, Alois Hudal, Jozef Tiso, Abbot Alban Schachleiter, Gerhard Kittel ambapo walikubali kulamba nyayo za Hitler na kuhubiri vitu vice versa, huku wakiwa mstari wa mbele kueneza chuki na propaganda za kijinga ndani ya makanisa.
View attachment 3517927
Pumzika kwa amani mwamba, Dunia itaendelea kuenzi kazi yako tukufu, jina lako Dietrich Theodor Ludwig Bonhoeffer limeandikwa kwa wino wa dhahabu katika historia ya kanisa la Kilutheri. Kwa hakika wito wako uliutendea haki kwa 100%, ulisema na kuhubiri ukweli kama ambayo ulifundishwa na Frank Fisher kwenye mitaa ya Harlem pale katika kanisa la Abyssinian Baptist Church.
Mkuu Simulizi Tam Sana shusha nondo tuondoke, usisahau kunitag siku nyingine inshaallah 🙏🏿
 
Mwamba kabisa yaani hapo juu umenichekesha na kunirudisha zamani kidogo nikiwa nasoma seminary mojawapo jijini Dar es salaam nikiwa chini ya chaplain RICHARD HANANJA kipindi HANANJA bado ni HANANJA kabla ya kupitiwa na pepo la uchawa .

Hakika nimeipenda hii simulizi ,inavikumbusha vizazi na wazee wa makanisani kuacha uchawa na kusimamia kweli iliyo kweli .

Ni jana tu kijana wa bwana Hananja Airwaye OT hananja ,alumni wa Chuo kikuuu cha Dar es salaam, katika mambo ya mziki alinipigia akasema kaka pole na udhalimu wote ulioigusa familia yako nikasema ahsante sana ila mwambie mzee kapatwa nini ? Alicheka sana akasema mzee simsomi pia ila zaidi hata mama anahisi mzee labda amekuwa croned 😀😀 inachekesha sana enhe ? Ila ni maumivu sana tena sana .

Tanzania government free hamphrey polepole
 
Yes jamaa anatuletea Comedy wakati kumbe mtoto wake naye ilikuwa ½ wampe ulemavu
 
Mpango wa kumuua Hitler ulisukwa na watu wengi sana .. sikujua na huyu bwana alikwepo kwenye list
Yes! Jamaa aliona wanachafua kanisa ikabidi ajiunge na Abwehr kumnyoosha Hitler
 
Amani ni tunu yetu basi tuilinde kwa wivu mkubwa sana

epuka maandamano Linda uhai wako
 
Jukwaa la historia linazidi kunoga.

Kutoka historia tunajifunza mengi sana.

2021 15 October

Nadharia ya Upumbavu

Dietrich Bonhoeffer alisema kwamba watu wajinga ni hatari zaidi kuliko waovu. Hii ni kwa sababu ingawa tunaweza kupinga au kupigana na watu waovu, dhidi ya wajinga hatuna ulinzi — sababu hazipatikani. Maandishi maarufu ya Bonhoeffer, ambayo tuliyahariri kidogo kwa video hii, yanatumika kama onyo kwa jamii yoyote huru kuhusu kile kinachoweza kutokea wakati watu fulani wanapata nguvu za kiutawala iwe ktk serikali au dini

Si UPUMBAVU tu kwa English inaitwa ni “CULTURAL APPROPRIATION” ili kujipatia umaarufu.
fatma karume aka Shangazi
@fatma_karume
Si UPUMBAVU tu kwa English inaitwa ni “CULTURAL APPROPRIATION” ili kujipatia umaarufu.
Ndio maana I ❤️ English. Ina msamiati for everything
maana I English. Ina msamiati for everything.
Bonhoeffer argued that stupid people are more dangerous than evil people. This is because we can protest or fight evil people, but against stupid people we are defenseless. Reason falls on deaf ears. This is his theory of stupidity.

Dietrich Bonhoeffer argued that stupid people are more dangerous than evil ones.

View: https://m.youtube.com/watch?v=ww47bR86wSc
This is because while we can protest against or fight evil people, against stupid ones we are defenseless — reasons fall on dead ears.

Bonhoeffer's famous text, which we slightly edited for this video, serves any free society as a warning of what can happen when certain people gain too much power.
 
Jukwaa la historia linazidi kunoga.

Kutoka historia tunajifunza mengi sana.

2021 15 October

Nadharia ya Upumbavu

Dietrich Bonhoeffer alisema kwamba watu wajinga ni hatari zaidi kuliko waovu. Hii ni kwa sababu ingawa tunaweza kupinga au kupigana na watu waovu, dhidi ya wajinga hatuna ulinzi — sababu hazipatikani. Maandishi maarufu ya Bonhoeffer, ambayo tuliyahariri kidogo kwa video hii, yanatumika kama onyo kwa jamii yoyote huru kuhusu kile kinachoweza kutokea wakati watu fulani wanapata nguvu za kiutawala iwe ktk serikali au dini

Dietrich Bonhoeffer argued that stupid people are more dangerous than evil ones.

View: https://m.youtube.com/watch?v=ww47bR86wSc
This is because while we can protest against or fight evil people, against stupid ones we are defenseless — reasons fall on dead ears.

Bonhoeffer's famous text, which we slightly edited for this video, serves any free society as a warning of what can happen when certain people gain too much power.

Bonhoeffer alikuwa anajua kupiga spana hata kama wakuu walikuwa hawapendi
 
Back
Top Bottom