Nilikuwa katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), maarufu kama
Archbishop Mgulunde Learning Resource Center, mwanzoni mwa Novemba, nilipokutana na kitabu cha zamani kilichofichwa kimya kimya kwenye moja rafu ya maktaba:
The Plot to Kill Hitler: Dietrich Bonhoeffer – Pastor, Spy, Unlikely Hero cha mwanamama
Patricia McCormick. Nilipoomba kukiazima, niliambiwa kuwa “kimehifadhiwa maalum kwa ajili ya mapadri wa katoliki na wakufunzi wa masomo ya dini pekee waliopo chuoni hapo.”
View attachment 3517914
Kauli hiyo haikunishawishi kwani nilihitaji kukiazima kwa siku kadhaa. Nilipiga picha ya jalada, nikaandika pembeni jina la kitabu, kisha nikaenda
Amazon Kindle kujipatia uhondo.
View attachment 3517916
Kama haujashiba vizuri au ni jamii ya wafuasi wa Mbogamboga basi simulizi hii tamu itakuboa mapema sana, historia ya giza na hofu ya utawala wa chama cha Nazi ilipatiwa dibaji iliyoshiba kisha baadaye kupewa nafasi ya kuangaziwa kwa lugha nyepesi kabsa: Ujerumani kwa wakati huo ilikuwa ni kama mbwa aliyelowana maji na mwenye hofu, kanisa liligawanyika kati ya usaliti na ujasiri, wapo wachugaji waliofyata mkia na kuwa vibaraka wa Hitler.
View attachment 3517915
Watu kama
Ludwig Muller, Paul Schmidt, Martin Niemoller, pamoja na
Alois Hudal walijizima data kabsa na kuunga mkono pamoja na kutoa baraka kwa unyama ambao
Hitler alikuwa akifanya.
Ila katika purukushani na fujo zote kuna mchungaji mmoja aliyethubutu kusema “hapana” kwa Hitler na kutumia utimamu wake kuonesha kuwa hakuna sehemu yoyote ya neno takatifu la Biblia linalounga mkono ujinga na ushenzi wa chama cha Nazi wala mipango ya
Hitler.
View attachment 3517924
Alikuwa ni mchungaji ambaye hakutaka kuwa kama
Mchugaji Richard Hananja, hakuwa mchungaji wa kusifu na kuimba mapambio kwenye madhabahuni; aliingia kwenye mtandao wa siri wa upinzani, akawa mchungaji, jasusi, na shahidi wa kanisa la Kilutheri.
View attachment 3517925
Kitabu hiki usisome ukiwa na njaa! Usisome ukiwa unaamini kuwa kesi ya
Simba kutafuna watoto wa Swala itapata suluhu na maamuzi bora mbele ya Chui kama Hakimu wa Mahakama.
View attachment 3517926
Ni kitabu ambacho kilichoandikwa kwa mtindo wa kukuonesha matukio kwa ukaribu, kinaonyesha wazi jinsi baadhi ya makanisa yalivyogeuka vyombo vya propaganda, wachungaji walivyobadilika na kuwa makasuku.
View attachment 3517922
Achana na lile kundi la kina
Alois Hudal, kuna kina
Jozef Tiso huku wachungaji wachache sana wakisimamia imani zao na kuzifanya kuwa silaha ya kupinga uovu, mbaya ni kuwa hata Kanisa Katoliki nao walifyata mkia na kuingia baridi ile mbaya.
View attachment 3517918
Watu kama
Abbot Alban Schachleiter walitia aibu sana kanisa Katoliki, huyu mwamba alikuwa akitumia salamu ya kinazi waziwazi, mpaka madhabauni na mbele ya Altare, huku pia akitumia ibada kama uwanja wa kuhalalisha ujinga wa Hitler.
View attachment 3517917
Kadinali Michael von Faulhaber aliona huyu mpuuzi analeta mazoea na Altare takatifu kwa kuhubiri upuuzi wake na uchawa, hivyo akamchoma kwa Boss Kubwa,
Papa Pius XI,
Abbot Alban Schachleiter aliondolewa na Vatican hawakuwa na jambo jingine bali kurudi maneno yake,
“ROMA LOCUTA EST; CAUSA FINITA EST”. Kisa cha Abbot Alban Schachleiter nitakileta hivi karibuni!
View attachment 3517927
February 4 mwaka 1906 ikiwa ni Jumapili moja tulivu kabsa ndani ya Mji wa Breslau Ujerumani ambapo kwa sasa panatambulika kama
Wroclaw, Poland alizaliwa dogo mmoja, shahidi wa imani na kanisa, wazazi wake wakiwa ni
Karl Bonhoeffer na aliyeteremsha chuma duniani ni Mwanamama
Paula von Hase. picha linaanza wazazi wakaona itapendeza sana kama dunia itamfahamu mtoto wao kwa majina ya
Dietrich Theodor Ludwig Bonhoeffer.
View attachment 3517928
Mwamba
Bonhoeffer alikuwa mchungaji wa Kanisa la Kilutheri, mwanatheolojia mashuhuri wa mwelekeo wa
neo-orthodoxy, na mpinzani shupavu wa utawala wa
Adolf Hitler. Maisha yake, harakati zake pamoja na huduma yake kwa kanisa la Kilutheri yamefanya jina lake lihesabiwe leo kama la shahidi
(martyr) katika baadhi ya madhehebu ya Kikristo.
View attachment 3517929
Mara baada ya kupanda kwa chama cha Nazi na kuingia madarakani mwaka 1933 hali hii ilimkuta
Bonhoeffer akiwa kijana mwenye kipaji kikubwa cha kitaaluma na kiroho.
View attachment 3517926
Ajabu ni kwamba mwamba alikuwa hana mbili kwenye moja, alihubiri na kutafsiri andiko bila kupindisha hata silabi moja, kariba yake ilimtofautisha sana na viongozi wengine wa dini ambao walikuwa aidha ni wanafiki au makasuku.
View attachment 3517930
Ukiachana na bwana mdogo, ndani ya Ujerumani pamoja na Austria kulikuwa na idadi kubwa sana ya viongozi wa dini mandazi sana waliokaa kimya na wengine kuamua kuwaunga mkono wanachama wa Nazi katika utawala mpya, tofauti kabsa na
Bonhoeffer ambaye alichagua njia hatari ya kuwa mpinzani, alikuwa anajua kupiga spana haswa.
View attachment 3517923
Siku mbili tu baada ya Hitler kuteuliwa kuwa Kansela,
Bonhoeffer aliandaa mahubiri yake na kumuomba Roho Mtakatifu nguvu kisha alikwenda kutoa hotuba redioni akiionya Ujerumani dhidi ya kumwabudu
Führer kama sanamu ya kisiasa.
View attachment 3517920
Hotuba hiyo ilikatizwa ghafla – ishara ya kwanza ya chuki ambayo utawala wa Nazi ungeelekeza kwake. Ila kabla hawakazima hotuba yake mwamba akawahasa watu wakasome
2 Wafalme 17:38, huku akiwadokezea na andiko jingine takatifu kutoka
Kutoka 20:3-17.
View attachment 3517927
Kwa mujibu wa
Ferdinand Schlingensiepen katika kitabu chake cha
Dietrich Bonhoeffer: Martyr, Thinker, Man of Resistance cha mwaka 2012, Bonhoeffer aliona mapema kuwa Nazism haikuwa tu mfumo wa kisiasa wa ovyo na dhalimu bali pia uzushi wa kidini ndani ya Ujerumani.
View attachment 3517925
Wanachama wa Nazi, kupitia vuguvugu la
Deutsche Christen, walijaribu kuoanisha pamoja na kufungamanisha dini ya Ukristo na utaifa na ukabila, hata kufikia hatua ya kutaka kuondoa kabsa
Agano la Kale kwa sababu tu ya asili yake ya Kiyahudi. Kwa Bonhoeffer, hili lilikuwa shambulio la moja kwa moja dhidi ya Injili yenyewe. Mwamba akaona hawa wameingia choo cha kike, acha awanyooshe
barabara.
View attachment 3517929
Ndani ya Kanisa la Kiprotestanti la Ujerumani, Bonhoeffer alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa
Bekennende Kirche (Kanisa la Kukiri), lililokataa utiifu wa aina yoyote kwa serikali ya
Hitler katika masuala ya imani pamoja na uongozi. Ngoma ikazidi kuwa ngumu, dakika ya 30 bado ubao unasoma bila bila.
View attachment 3517930
Wazee wa kanisa wakaweka kikao chao na kuja na
Azimio la Barmen la mwaka 1934, lililoandikwa na
Karl Barth na kuungwa mkono kwa 100% na
Bonhoeffer, lilisisitiza kwamba
Kristo – si Führer – na Kristo ndiye kichwa pekee cha Kanisa mwisho wa nukuu.
View attachment 3517924
Bonhoeffer akaamua kukazia maumivu kwa chawa na vibaraka wa
Hitler akawapiga na neno kutoka
1 Wakorintho 8:6 pamoja na
Waefeso 4:6-8. Acha kabsa moto uliwaka vifuani vya maafisa wa Nazi waliokuwa ndani ya
Wolfsschanze pamoja na
Adlerhorst. Maneno na msimamo huu ulimfanya
Bonhoeffer awe adui wa wazi wa dola ya Nazi.
View attachment 3517921
Chuki ya wanachama wa Nazi dhidi
Bonhoeffer haikubaki kwenye kejeli za maneno pekee. Kwanza kabsa alipigwa marufuku kufundisha, kuchapisha, na hatimaye kusafiri kwa uhuru kutoka eneo moja ndani ya Ujerumani. Mwamba akaona hawezi kutuia kizembe namna hiyo, akafungua Seminari ya siri na kuipatia jina la
Finkenwalde, aliyokuwa akiiongoza kwa ajili ya kuwafundisha wachungaji wa Kanisa la Kukiri, ilivamiwa na
Gestapo na kufungwa.
View attachment 3517917
Hapo ndipo
Bonhoeffer aliandika kitabu chake maarufu
The Cost of Discipleship cha mwaka 1937, ambacho mwaka 1989 Edwin Robertson alikitaja kama wito wa Ukristo wa “neema ya gharama” (
costly grace)—imani inayodai utii halisi hata kama gharama yake ni mateso au kifo.
View attachment 3517927
Kadiri vita vya pili vya dunia vilivyozidi,
Bonhoeffer alikabiliwa na mgogoro mkubwa: je, Mkristo anaweza kushiriki katika njama ya kumuua dikteta? Kupitia shemeji yake
Hans von Dohnányi, mzee baba
Bonhoeffer aliingia katika mtandao wa upinzani ndani ya
Abwehr (majasusi wa kijeshi ndani ya Ujerumani).
View attachment 3517930
Alitumia nafasi hiyo kusaidia Wayahudi kutoroka na pia kuwasiliana na maafisa wa Uingereza, akiwemo
Askofu George Bell wa Chichester, kama alivyoeleza Kenneth Slack mwaka 1971. Wanahistoria wa Ujerumani kama vile;
Fritz Fischer hudai kuwa mzee baba
Bonhoeffer alikuwa agent wa
Abwehr.
View attachment 3517924
Ingawa alikuwa mpinzani wa vurugu kwa misingi ya imani, Bonhoeffer alikiri kuwa wakati mwingine “mtu anayewajibika” analazimika kuchukua hatia juu yake mwenyewe kwa ajili ya kizazi kijacho.
View attachment 3517923
Mwanzoni lengo la msingi la
Bonhoeffer lilikuwa ni kuzuia Nazi wasiharibu kanisa ila taratibu aliona kuna haja kubwa ya kulinda kila pembe kwani kila sehemu Nazi walitaka kupeleka nadhari ya kipuuzi ambazo hazikuwa na msingi wowote. Mwaka jana mwandishi wa kitabu cha
The Sovereign Human Being,
Prof Valentin Jeutner alieleza kinaganga jinsi
Bonhoeffer alivyovuka mipaka ya nadharia na kuingia kwenye maamuzi halisi ya kimaisha. Ni kama
Bonhoeffer aliona jamaa hawahitaji mahubiri pekee pia na mapigo kama Farao.
View attachment 3517920
Kukamatwa kwake mwaka 1943 ulikuwa mwanzo wa safari yake ya mwisho, maana aliwatoa jasho vya kutosha Nazi. Akiwa gerezani huko
Tegel,
Bonhoeffer alitumia nafasi hiyo kuandika barua na tafakari zilizojaa matumaini, mashaka, na imani, zilizokusanywa baadaye katika
Letters and Papers from Prison.
View attachment 3517919
Humo, alizungumza juu ya “Ukristo usio wa kidini,” akitafakari mustakabali wa imani katika dunia ya kisekula, mahala ambapo serikali haifungamani na dini yoyote.
View attachment 3517925
Baada ya kugunduliwa kwa nyaraka za
Abwehr mwaka 1945, Hitler alipandwa na hasira kwa kiwango cha 5G, na ili kukomesha kabsa roho hii ya ajabu ya mtu kama
Bonhoeffer aliamuru kunyongwa kwa washiriki wote wenye mahusihano na
Abwehr.
Bonhoeffer alinyongwa akiwa uchi alfajiri ya tarehe 9 Aprili 1945.
View attachment 3517930
Leo,
Bonhoeffer anatambuliwa na makanisa mengi kama shahidi. Kanisa la Anglikana, Kanisa la Kilutheri Marekani (ELCA), na Kanisa la Methodisti linampa heshima na kumkumbuka rasmi kama mtu aliyekufa kwa ushuhuda wa imani. Sababu si tu kifo chake, bali maisha yake yote: aliishi kile alichohubiri, aliishi na roho mtakatifu ambaye alimuongoza kusema ukweli bila kupindisha maneno.
View attachment 3517929
Katika kitabu cha
Bonhoeffer’s Black Jesus kilichoandikwa na
Reggie L. Williams mwaka 2014 kinasimulia ujasiri wa ajabu wa
Bonhoeffer ambaye aliutazama Ukristo kama tumaini na nguvu kubwa sana ambayo haitoki kwenye chama cha siasa wala kwenye mikono ya serikali.
View attachment 3517927
Kwa kifupi,
Dietrich Bonhoeffer hakuuawa kwa bahati mbaya ya vita, bali alikufa kwa sababu alikataa kuisaliti Injili, hakukubali kubadilisha maandiko ili baadhi ya watu wafurahie na kucheka mpaka
MOLARS NA PREMOLARS zionekane. Katika dunia ambayo mara nyingi imani hutumiwa kuhalalisha nguvu na ukatili,
Bonhoeffer anabaki kuwa kumbukumbu hai kwamba Ukristo wa kweli unaweza – na wakati mwingine lazima – kusimama dhidi ya dola, hata kama gharama yake ni maisha yenyewe.
View attachment 3517921
Alikuwa tofauti kabsa na wapuuzi kama,
Alois Hudal, Jozef Tiso, Abbot Alban Schachleiter, Gerhard Kittel ambapo walikubali kulamba nyayo za
Hitler na kuhubiri vitu vice versa, huku wakiwa mstari wa mbele kueneza chuki na propaganda za kijinga ndani ya makanisa.
View attachment 3517927
Pumzika kwa amani mwamba, Dunia itaendelea kuenzi kazi yako tukufu, jina lako
Dietrich Theodor Ludwig Bonhoeffer limeandikwa kwa wino wa dhahabu katika historia ya kanisa la Kilutheri. Kwa hakika wito wako uliutendea haki kwa 100%, ulisema na kuhubiri ukweli kama ambayo ulifundishwa na
Frank Fisher kwenye mitaa ya Harlem pale katika kanisa la
Abyssinian Baptist Church.