Aisee kwa anae nyanyua kinywa na kutukana hawa wazee asamehewe, kuna toleo la plato "allegory of the cave" akielezea effects za education aisee ukiweza kunyambua na ukapata maana basi mjadala utakuwa umeisha ,kwa upande wangu mwalimu na plato wanatofautiana sana japo kama ulivyoeleza tofauti zao pia ni chache kwakuwa mwalimu alipita katika maandishi yake na akaamua kufanya kwa aina yake yeye mwenyewe kwa umahiri mkubwa nikiri tuu kuwa mwalimu alikuwa na uwezo mkubwa na kumtukana ni kumvunjia heshima maana hakuna aliyeweza kufanya kama yeye hadi sasa nikiongea hivi lazma tuangalie majira na wakati wa utawala wa mwalimu alifanya kazi kubwa katika elimu kuhakikisha mwanafunzi haishii kusoma tuu lakini afanye kwa vitendo pia hapo pia naona ni idea ya bwana john Dewey ambae anasimamia falsafa ya learn by doing hivyo mwalimu anaonekana kusoma watangulizi ili nae aje na utaratibu wake hivyo sioni kosa lake na ndivyo hata na fidel castro akiwa gerezani alipenda kusoma vitabu kuelewa siri za utawala hivyo ndio maana na sisi tunawasoma hadi leo na ukisikiliza maneno ya mwalimu nyerere anaonekana kama mtabiri wa haya ya leo,waheshimiwe hawa wazee