Digrii, Masters na PhD zote zifutwe tuanzishe mfumo wa elimu unaoendana mazingira yetu

Wanaosoma Tz wengi ni kipato cha chini au cha kati wasio na hela ya kutafuta elimu bora nje.

Hakuna elimu Tz ni kupoteza tu mda.
Wanasiasa wanasemaga tu mfumo tutaubadilisha halafu inakua imeusha hivo.

Upuuzi mtupu.
 
Kama mawazo haya yataungwa mkono na wengi basi ni bora tuifute kabisa nchi tuanze moja, mikoa mingine ikajiunge Uganda, Kenya, Burundi, Rwanda, Msumbiji, Malawi na Congo
 
Ukiugua huwa unatibiwa na nani?
 
Ukitoa degree, Masters na PhD tutakuwa na nini mbadala?
Tanzania si kisiwa, baadhi ya mambo ni ya kidunia.

Cha kufanya ni kuboresha sera na mitaala yetu ili mtanzania anapokuwa na degree, aweze kutenda na kuwaza globally kama degree holders wa nchi zingine zilizo advanced kuliko sisi.

Mfano:
1. Lugha ya kifundishia iwe English mwanzo mwisho.

2. Contents za mitaala zibadilike, tuache zisizoakisi mahitaji ya dunia ya leo na kuongeza zinazofit.

3. Mtindo wa ufundishaji ubadilike kabisa. Madarasa yajae models za kujifunzia. Kwanza tuwe na practical lesson plans za kitaifa. Walimu waandae resources na kufuata plans hizo tu.

4. Assessment za kumtoa mtu level Moja kwenda nyingine ibadilike kabisa.
Tunahitaji system ya kuhifadhi continuous assessment za kazi za watoto huko mashuleni badala ya kungoja 'national exam'.

Mambo ni mengi.
 
Hapana mkuu, hizo ngazi za elimu ziendelee kuwepo, humohumo tutapata wataalamu wa ukweli. Hata ukipanda mbegu shambani, usitegemee mazao yote yatakuwa na ubora ulio sawa; lazima yatatofautiana. Mbona tumeona wataalamu waliobuni (design) mambio makubwa katika taifa letu? Angalia daraja la juu la Mfugale! Wapo kweli baadhi wanakariri, lakini hiyo isiwe kigezo cha kusitisha ngazi hizo za elimu ulizotaja. Lichukulie hili kama katika msafara wa mamba na kenge nao wamo!
 

Una maana hata PhD ya madam nayo ikwende na maji?
 
Tukiacha mtaala wa kikoloni sasa hivi tutarudi karne ya 18. Unajua tulipaswa kuwaacha wazungu watawale hadi 2050 huku tukijichanganya nao na kijifunza kwao kila jambo jema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…