Dili la Simba kumng'oa Max Nzengeli lagonga mwamba

Simba wamefanya jaribio zito la kutaka kumng’oa juu kwa juu kiungo wa Yanga Mkongomani, Maxi Nzengeli ambaye alipiga mabao mawili dhidi ya Simba kwenye ushindi wa mabao 5-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara hivi karibuni.

Simba wamepiga simu kwa klabu ya zamani ya Nzengeli ya Union Maniema ya DR Congo na kumwaga ofa nzito wakijua kwamba huenda kiungo huyo yuko jangwani kwa mkopo kama ilivyowahi kuzushwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya wachambuzi.

Hata hivyo, Mwanaspoti linajua Simba wamejibiwa kwamba Nzengeli ni mali halali ya Yanga na kwamba kama kuna hatua za kumuuza licha ya Maniema watapata mgao wao lakini watu wa kwanza watakaosimamia biashara hiyo ni watani Jangwani ambapo hawakuridhika wakaingia mfukoni na kutoa ahadi nzito kwamba mabosi hao wa Maniema basi walianzishe kwa kutaka kumchomoa kisha wao watamwaga fedha za kufuru mara mbili ya zile ambazo Yanga walilipa.

View attachment 2822835
Simba ii ya kumsajili Max? Simba ya MO sasa hivi lengo lao kubwa ni kumng'oa Mangungu kwenye uongozi. Wako tayari Simba ifungwe goli 10 watafurahi ikia ndiyo suluhisho la kumwondoa Mangungu. Hawana uchungu walaa huzuni kufungwa magoli mengi. Ndio maana makocha wote Simba walioo ngea nao MO alikataa kujifunga kuwa atawalipa mshahara. Halafu leo wanaokuja hao hao kusema eti Simba inataka kumsajili Max. Kina MO wafahamu wanaweza kuwadanganya wanasimba wote kwa kipindi kidogo tu lakini itafika muda wanasimba watamshtukia na watafanya ya kwao
 
Hatari sana
 
Wale wachezaji wa yanga wapo pale Kama familia na hapo apongezwe Injinia jinsi alivyotengeneza huo muunganiko .
Kuna maelewano makubwa kati ya wachezaji, viongozi , mfadhili na zaidi Mpaka familia za wachezaji na timu walikotoka kuna mawasiliano na Viongozi .
 
Kuna watu walisema ...Yanga wameleta wacongo kwaajili ya dance[emoji23]
 
Matokeo ya kejeli ni kilio .
Nimeipata hii habari Kwenye mtandao .

Maxi anataka kuwa kama mayele au Nonda .

Back
Top Bottom