Simba wamefanya jaribio zito la kutaka kumng’oa juu kwa juu kiungo wa Yanga Mkongomani, Maxi Nzengeli ambaye alipiga mabao mawili dhidi ya Simba kwenye ushindi wa mabao 5-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara hivi karibuni.
Simba wamepiga simu kwa klabu ya zamani ya Nzengeli ya Union Maniema ya DR Congo na kumwaga ofa nzito wakijua kwamba huenda kiungo huyo yuko jangwani kwa mkopo kama ilivyowahi kuzushwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya wachambuzi.
Hata hivyo, Mwanaspoti linajua Simba wamejibiwa kwamba Nzengeli ni mali halali ya Yanga na kwamba kama kuna hatua za kumuuza licha ya Maniema watapata mgao wao lakini watu wa kwanza watakaosimamia biashara hiyo ni watani Jangwani ambapo hawakuridhika wakaingia mfukoni na kutoa ahadi nzito kwamba mabosi hao wa Maniema basi walianzishe kwa kutaka kumchomoa kisha wao watamwaga fedha za kufuru mara mbili ya zile ambazo Yanga walilipa.
View attachment 2822835