Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Mchezaji wa mpira wa miguu, gwiji Dimitri Payet anaripotiwa kuchunguzwa na polisi nchini Brazil baada ya kushutumiwa kwa 'unyanyasaji wa kimwili na kisaikolojia' dhidi ya aliyekuwa mpenzi wake mwanadada Larissa Ferrari wakati wa mapenzi yao ya miezi saba.
Nyota huyo wa zamani wa klabu ya West Ham anadaiwa kumlazimisha Larissa Ferrari mwenye umri wa miaka 28, kunywa mkojo wake na kulamba sakafu pamoja na kumsukuma na kumkanyaga sehemu kadhaa za mwili wake.
Nyota huyo wa zamani wa West Ham na kiungo wa kikosi cha Vasco da Gama, anaripotiwa kuwa chini ya uchunguzi wa polisi mjini Rio de Janeiro kutokana na changamoto hiyo.
Kwa mujibu wa AFP ripoti ya polisi ya Machi 29, mwanamke huyo alisema "Nilishambuliwa na kuachiwa alama kwenye mwili wangu kwa kupigwa na kusukumwa kisha kudhulumiwa kimwili, kimaadili, kisaikolojia na kingono.
Mwezi Desemba, tuligombana akaniomba uthibitisho wa mapenzi, ambao ulikuwa na udhalilishaji. Nilirekodi video nikinywa mkojo wangu, kunywa maji kwenye bakuli la choo na kulamba sakafu".
Huu unakuwa ni muendelezo wa visa na mikasa ambayo nyota wengi duniani wamekutana navyo, sio Neymar sio nani, ila namba inaendelea kuwa kubwa. Wanawake wamepata kuzitumia vibaya sheria ambazo zipo kwa ajili ya kuwalinda. Katika hili kama Payet hakuchukua matukio kwa njia ya video basi anakwenda kuisha.