Dinasours special thead: unajua lolote kuhusu wanyama kale? Tupeane ujuzi.

Ungekuwa unawatolea maelezo japo kidogo
 
Najua tu kutoweka kwao haikuwa process ya siku moja kama wengi wanavyo amini kuwa kile kimondo kiliua wote baada ya kupiga eneo la huko Mexico, hapana. Dinosaurs walitoweka kutokana na vumbi jingi lililoikumba dunia baada ya kupigwa na kimondo kikubwa. Vumbi hilo lilifanya mimea ishindwe kutengeneza chakula chake.
 
Duh!
Kivipi?
Kulingana na utafiti wa wanasayansi wa vitu vya kale wanaelezea baadhi ya wanyama kadhaa na ndege tulionao sasa ni kati tu ya sehemu ya uthibitisho wa mabadiliko haya ya kibiolojia toka wanyama na ndege wale wakubwa wa zamani kabisa mpaka hawa tunaoishi nao leo hii.


Mfano halisi ni ule wa jamii ya ndege wa zamani. Hawa ndege wanafananishwa sana na ndege wa leo kama kuku kwa vielelezo mbalimbali hasa kwa upande wa mifumo ya mifupa yao. Tumshukuru mungu sana kuku hana meno.

Pia kuna wanyama zaidi wameweza kuonyesha mfanano mkubwa na wanyama wa kale kama ;

ndege huyu anaepatikana kisiwa kimoja huko australia anaitwa CASSOWARY

anafananishwa na ndege huyu wa zamani aitwaye VELOCIRAPTOR

Golilla wa leo anafananishwa na GIGANTOPITHECUS


Rhino wa leo anafananishwa na PARACETHERIUM


Mamba wa leo anafananishwa na SARCOSUCHUS ambae kwa ukubwa kwenda juu ni sawa na mbwa aliyekuwa mpaka mwisho


Elephant wa leo anafananishwa sana na MAMMOTH


Hiyo ni baadhi ya mifano hai waliyotoa watafiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…