Dini Dini Dini Dini.....Sasa miye nimeanza kuboreka na hizi threads za dini, Je wewe?

Je, Sehemu ya Dini/Imani Ifungwe au Isifungwe hapa JF?!

  • Isifungwe

    Votes: 14 43.8%
  • Ifungwe

    Votes: 8 25.0%
  • Irekebishwe

    Votes: 10 31.3%

  • Total voters
    32
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Mimi nashauri ukumbi wa Siasa ufungwe maana matusi na kashfa zimezidi

Masatu, asante kwa kuweka maoni yako hapa, ila nadhani ingekuwa madhubuti zaidi kama ungelianzisha thread ya maoni inayohusiana na swala hilo katika siasa kuliko kuweka hapa, maana hii ni ya maoni yahusianayo na dini. Uhuru wa kusema upendalo hata hivyo nina uheshimu. Baadae.

SteveD.
 
Kwa wote mliochangia mpaka hivi sasa;
Nashukuru sana kwa maoni yenu. Mwangaza nilioupata ni mkubwa kuhusiana na jinsi tunavyo ona majadiliano yahusuyo imani/dini yanavyo jiendesha hapa jamvini.

Kutokana na yale niliyoyasoma, miye pia naona ni bora jamvi la dini/imani libakie. Ila kimoja ni kuwa labda ni kumshauri ndugu Admin aongeze sana moderation/uhakiki katika hili jamvi bila kukwaza maoni ya watu. Ila nasi kama wachangiaji ni muhimu kuzingatia yale mengi wengi wetu tumeyasema kwenye thread hii, ya kuwa; Imani/dini ni kitu sensitive sana, na kwa wengine imani/dini inashika umbele kuliko hata wazazi, hivyo tupunguze maoni yanayoonekana ni kashfa zidi ya wengine katika hili. Pia kama tuna kitu tunakiona ni cha kukosoa/kuuliza kihusinacho na imani ya mwingine, basi tukiulizie/tukijadili katika hali ya ustaarab. Ni hayo tu kwasasa. Ahsanteni.

SteveD.
 
Niliomba kupewa tafsiri ya "kashfa", lilikuwa ni direct swali kwa SteveD, lkn haikuwa na maana kuwa wengine wasingeweza kuchangia! Vinginevyo tutakuwa tukijadili kitu tusichokijua.

Tanzania 1,
Samahani sikuweza kukujibu swali lako hapo awali. Kwa vile umetuuliza swali hapa lihusianalo na tafsiri ya neno, nitajitahidi tu kulijibu kwa uharaka haraka kama jinsi nionavyo miye. Naona kama ni kupata tafsiri fasaha kisheria kama ulivyo uliza, labda bora kulipeleka swali lako kwenye forum ya lugha, naamini kuna wataalam huko wanaweza lichambua ipasavyo..

'Kashfa' kama nilivyo iongelea mimi ni ile hali ya kuongelea kitu 'imani/dini' ya mwenzako kwa lengo mahiri kuwa unataka kumkosoa yeye, yakuwa anacho amini si halali na hakifai mbele ya macho yake na ya wengine, na jinsi unavyo ongelea swala hilo ni katika hali ya kudharau wala si kujenga hoja (logical reasoning) bali unafanya hivyo kwa msukumo wa imani yako, kitu ambacho nacho ni cha kuaminika tu pia.

Na imani kuwa kuna wengine wanaweza kulifafanua hili kwa undani na kwa kiswahili fasaha zaidi. Ahsante.


OOh, out of topic: Tanzania 1, avatar yako kiboko ndugu yangu.. nimeipenda sana tu..lol.


SteveD.
 

SteveD,

Thanks for "your defn". Naona nisiendelee na hili maana umeshatoa decision, ambayo hata nami ninaiunga mkono. Asante kwa jitihada zako za kutuweka sawa!

Ooh, asante, ndugu yangu! Nimeitengeneza hii avatar kimchezo-mchezo tu! K/hiyo unanishauri nifungue kampuni ya graphics designing? Mmmh, kichwa kinanielemea; kimekuwa kikubwaa!
 

Kashfa maana yake ni ukweli uliofichwa, ukweli ambao ukitoka adharani utaondoa reputation ya mtu au jambo husika. Kasshfa ni sawasawa na neno la kiingrerza Scandal.

Mfano: Kama ueandika kitabu na watu wakagunduwa kuwa vile vilivyomo ndani ya kitabu hicho ni uwongo, that's Kashfa, kwa sababu watu wamegunduwa kuwa ulicho andika ni uwongo na hali ya kwamba wewe mwandishi au publisher umekusudia watu waamini kuwa kilichomo ndani ya kitabu chako ni kweli.

Kama mwandishi ameelezea jambo fulani ndani ya kitabu chake au amezungumzia machafu ya mtu fulani, na jambo hilo likaja kuonekana kuwa ni uwongo, hii Pia ni kashfa kwa mwandishi kwa mwandishi aliye andika na inapelekea kazi yake kuwa kwenye kundi la Libel. Yaani umesingizia.

Kwa upande wa dini kama jambo linaongelewa ni logical Reasoning, na likaonekana kuwa ni kweli, basi hiyo ni Kashfa kwa sababu umetoa kweli iliyofichwa dhidi ya kundi fulani.

Lakini maandishi yako na reasons zako zikithibitika kuwa ni uwongo tha's Libel dhidi ya mandishi yako.

Kwa ufupi neno KASHFA ni neno la kiarabu na maana yake ni kuelezea jambo la ukweli ambalo likitoka hadharani litaondoa reputation yako au kile unacho kiamini.
 

Mimi ninajua kwamba Kashfa maana yake ni matamshi au mchoro au kitendo fulani chenye lengo la kupotosha maana halisi ya kitu fula jinsi kilivyo.

Tuwe FAIR tunapotaka kuweka mambo fulani wazi tusipeleke jazba hata pale mtu anapotaka kufahamu mambo fulani ya msingi.

Mfano
 
Dini muhimu ndugu zangu, lakini mbaya kukashifu madhehebu ya watu. Kwani dini nini? Wengi tunadhani dini ni madhehebu ya kiislamu, kikristo, kibudha nk. Dini kwa maoni yangu ni ile hisia ya kimaadili iliyoumbwa katika nyoyo za binadamu. Pahala fulani katika historia wakazuka watu au vikundi vya watu wakaamua kurasmisha mienendo ya watu wengine kufuata hayo maadili. Lakini wengi wa hawa watu walidandia migongoni mwa mawazo au mifano ya maisha ya watu wachache walioishi maisha ya mifano bora kimaadili kama kina Manueli au Yesu au Issa; au kina Muddy, samahani Muhammadi na wengineo. Kinachogomba sasa ni ushabiki wa wafuasi wa haya makundi, yaani madhehebu, SI DINI KWA MAANA YA DINI!
Kwa hiyo dini kwa maana ya masuala ya maadili ya kijamii, kiroho nk ni muhimu kujadiliwa kwa minajili ya kuongozana au hata kuongoana; tuachie tufwaidi hizo nondo kama kweli nondo zenyewe zina uzito na dawa mujarab kwa maisha yetu!
 
tupo hapa kutafuta solution ya ukumbi wa dini na wengine wameona huku huku walete hayo mambo yao ya kitoto.hivi unatuonesha nini? kwamba huwezi kujirekebisha au?.waswahili tuna tabu kweli kweli. haya lete kejeli nyengine.
 

SteveD,
Wewe ndiye uliyeanzisha thread hii, kwa dhamira njema tu, na ukafikia kwenye uamuzi:
Huyo niliyemnukuu hapo juu nadhani ni mtu mzima, ila sidhani km anaelewe kinachojadiliwa hapa, and his mental health is questionable. Kutokana na hilo, naomba admin. im-ban at least ktk mjadala huu, o/wise hakukuwa na haja ya kuuanzisha mjadala huu, na k/hiyo hakuna haja ya kuuendeleza. THIS IS RIDICULOUS!!
 
Tanzania 1 na under age, nashukuru kwa hekima zenu katika kuliona hilo. Kwa kweli hizo ndiyo kejeli, kashfa na kufuru tunazotaka tuziondoe katika forum ya dini/imani.

Nitawakilisha malalamiko yenu kwa Admin. Ahsanteni.

SteveD.
 
Kwa kweli bias ni mbaya! Nilipotumia majina ya aina zote kwa Issa haikuonekana mbaya, lakini kwa Muhammad ikawa noma!!! Poleni, nimeshakujueni. Kama admini watanifungia safi tu!!! Kwani wataninyima ugali??Tuvumiliane.
 
Kwa kweli bias ni mbaya! Nilipotumia majina ya aina zote kwa Issa haikuonekana mbaya, lakini kwa Muhammad ikawa noma!!! Poleni, nimeshakujueni. Kama admini watanifungia safi tu!!! Kwani wataninyima ugali??Tuvumiliane.

Ngao,
Samahani ndugu, naomba kupingana nawe kidogo hapo juu kwenye wekundu. Kunradhi naomba kutumia lugha ya wenzetu hapa kidogo inayosema kuwa 'two wrongs don't make a right', basi na kwenye hilo swala la kutumia mifano miwili ya majina haimaanishi kuwa kwa vile upande mmoja hawajaudhika au kukerwa na yale uliyoyasema hilo halimaanishi kuwa kile ulichokisema ni cha kuhalalisha kwa wale wengine.

Ngao, kwenye post yako awali nilipenda jinsi ulivyo anza kuelezea dini na kutoa maoni yako kuhusu hilo. Lakini ghafla ukajikwaza kwa kuita majina Mitume wa Waumini, majina ambayo Waumini wengine hawakubaliani nayo. Jambo ambalo linaenda kinyume kabisa na yale tuliyokuwa tunayajadili katika thread hii. Ya kuwa, kuna wenzetu jambo la dini/imani linashika mstari wa mbele katika maisha yao kabla ya chochote. Hivyo basi kulitamka jina la Mtume wao kikejeli au kinamna ambayo hawataridhia si jambo la busara. Na katika hii thread, mimi ndiyo ninachotaka kuwaambia wote kuwa ili basi tuendelee kuwa tunachangia mawazo kwenye hii forum ya dini/imani, haina budi wote waumini na wasio waumini kujirudi na matamshi yote ambayo yanaweza kuchukuliwa kama kashfa kwa wengine. Na katika kufanya hivyo ushauri wangu mkubwa kwa wengi katika forum ya dini ni kuwa, ili kuondoa utata na kujikwaza, ni bora member wa forum hii aongelee dini/imani yake na siyo ya mwingine. Maana huwezi jua yale utakayosema kama yatakuwa ni kashfa kwangu mimi au laa, isitoshe dini ni imani, na kiwango cha imani kwa mtu hakina kipimo na hakipimiki kwenye mizani, bali ni cha kuaminika tu.

Ngao, kama ndugu Admin anakufungia, basi kubali kutumikia kifungo maana utakuwa umeonekana unakosa, kama vile wenginewo wanaofungiwa kisha kufunguliwa baada ya muda katika kutumikia adhabu yao, kama unasamehewa basi nalo ni jukumu watakalo chukua. Ndiyo hali yenyewe tena, maana kila jambo lina consequences yake na majuto ni mjukuu.

Ila kwa vile umesema 'tuvumiliane' hapo mwishoni, hii inaonesha kupevuka kwako na kinamna fulani kujirudi kutokana na yale uliyosema. Ahsante na siku njema ndugu.

SteveD.
 
Kwa kweli bias ni mbaya! Nilipotumia majina ya aina zote kwa Issa haikuonekana mbaya, lakini kwa Muhammad ikawa noma!!! Poleni, nimeshakujueni. Kama admini watanifungia safi tu!!! Kwani wataninyima ugali??Tuvumiliane.

Ndugu, you have to lie in the bed you have made. Issa/Yesu anakubalika ktk dini zote mbili, Uislam na Ukristo. Na anajulikana kwa majina km ulivyoyataja. Lkn, ulikuwa na maana gani kusema?:

kina Muddy, samahani Muhammadi

AU KEYBOARD YAKO HAIWEZI KUFUTA UNAPOKOSEA?! ANY FOOL COULD SAY WHAT YOU SAID. Hakuna aliyefuata ugali hapa JF.
 
Steve D
Suala la dini ni suala la ajabu sana, watu hawawezi kufanya discussion kuhusu mambo ya dini objectively. Kila mtu anakuwa subjective, na mara nyingi watu wanaishia kurushiana maneno ya kashfa, kuna haja ya kurekebisha thread hii au kuifuta. Dini maa nyingi ni jambo la mtu binafsi na anachokiabudu, kwa hiyo wangeachiwa wenyewe na roho na akili zao, sio ku-share.
 
Thread za dini zimeanza kuwa na matatizo mengi tena, tena sana tu... sidhani kama kuna mamoderator wa kutosha kuratibu au kukemea yale yasiyofaa kimaadili ya Kitanzania na kwa kisheria za ukumbi huu. Members wameongezeka na michango yenye kukebehiana inazidi kushamiri. Nimekaa kimya kwa muda kuhusu hili lakini imefika wakati nashindwa kuvumilia kwa yale yanayozidi kuandikwa na baadhi ya WanaJF.

Kutegemea moderators ambao wala hawalipwi sioni kama kutafua dafu kwa wingi wa threads za dini, na kuongezea mamods nako pia kunaweza kuleta matatizo yake yasiyotabirika. Nina imani kubwa kuwa moderator hao hao wanakodolea macho zaidi threads za siasa na mambo ya kiuchumi Tanzania kuliko hizi za dini, sijui sababu, lakini nadhani ni labda kwa kuamini kuwa, watu wanaochangia kwenye dini ni Wacha Mungu hivyo wanajikimu na kuzingatia maadili mema kidini. Hata hivyo yanayozidi kujitokeza huko ni kinyume kabisa.

Sasa ndugu, nashindwa cha kufikiri isipokuwa kuwa kuleta hoja ya kwamba, labda michango ya kwenye dini ipunguzwe, sema watu waweze kupost kwenye dini siku ya Ijumaa au Jumapili au Jumamosi tu. Ili kupunguzia mzigo waratibu wa ukumbi. Au basi, mtu aweze kupost mara moja tu katika dini kwa siku kama hilo linawezekana, maana kufunga ukumbi tuliafikiana hakutafaa kama sisi wenyewe tunaweza kujimudu... jambo ambalo naona polepole linashindikana.

Sababu mojawapo ya mimi kusema hivi ni kuwa, hata katika jamii zetu, kuna siku maalum za kusujudu miungu wetu tulizowekewa au kujiwekea. Najua watu wako huru kufanya swala zao siku yoyote na wakati wowote, ila katika hili siyo jambo la swala tena, bali limekuwa jambo la kuporomosheana kashfa zidi ya wenzetu wenye imani tofauti. Kujiheshimu na kuheshimu dini/imani za wenzetu kunazidi kushuka kimaadili na kimisingi ya kimaoni haswa katika mwongozo na kanuni za JF. Na ninavyoona kuratibu mambo yote hayo nadhani inawawia vigumu sana ma mods hapa JF. Tusitahamaki na kukuta kuwa, tumekuwa na ukumbi wa vita vya kidini JF kimaandishi na kusahahu kabisa mustakabali wa Taifa letu kama jambo hili linatuwia vigumu kulitatua.

JF inakua na itazidi kukua, najua kwa wengine ni ukumbi tu, lakini kwa yale niliyojifunza toka nijiunge nayo- kwa kweli naiheshimu nakuta kushiriki kila nipatapo muda kuiendeleza. Naomba ndugu zangu tuchangie jinsi ya kuiendeleza. Ni rahisi sana mtu kupost vitu ambavyo vinaweza kuangusha ukumbi huu. Tusipojali kulinda ukumbi wetu, sijui tutakuwa tunajali kitu gani.... sijui kwa kweli, sasa hivi nina imani wengi wetu tunaijua mifumo mingi ya nchi yetu kutokana na ukumbi huu, basi na tuilinde ngome yetu hata katika mambo ya imani/dini.

Naomba kutoa hoja. Ahsanteni.


SteveD.
 
Steve D,

Mimi ukiniuliza nasema ifungwe tu.. maana ni kutukanana kila kukicha unajua watu wanaochangia kule wanatetea Imani zao zaidi ya kujibu hoja!

Ndo maana neno kama Mpumbavu!!!! kutumiwa na watu huona ni poa...sasa watu wengine wanaokuja hapa jamvini wanajifunza nini?

Ifungwe kwa say 2 weeks hadi wachangiaji wajirekebishe kwanza!
 
Mkuu nakuunga mkono kabisa.Suala la imani ni la ajabu sana,wapo wachangiaji hapa JF katika mada zingine utasema hivi ni vichwa kwelikweli lakini akija huku kwenye imani utashangaa jinsi munkari unavyompanda hata anapoteza staha yake ile tunayoifahamu.
Imani iachwe kujadiliwa maana ni swala la moyoni na jinsi lilivyoingia huko kila mtu anafahamu kwa nafsi yake binafsi.
 
Kama ingekuwa watu wanatoa hoja kwa manufaa ya kujenga au kufunza kwa lugha au kauli njema, forum ya dini ilikuwa sehemu njema tu.

Tatizo watu wanatumia ukumbi kukashifu imani tofauti na zao,au lengo la kufanya imani yao ionekane bora zaidi au labda pia kutafuta wafuasi.

Labda tuangalie jinsi ya kuirekebisha badala ya kuifunga kabisa.
 
Tatizo kubwa liko katika hizi dini zenye asili na hapo mashariki ya kati tuu.Kelele na ugomvi utadhani hizo ndio dini pekee hapa Duniani. Mbona wapo Mabudha,Wahindu na nyingine nyingi lakini hawapigiani kelele wala kuuana? Hapa lazima kuna tatizo lililojificha ndani yake.
 
Kikatiba sote tuna haki y kuabudu na kuamini, Ila nadhani kuna mahala tunaelekea na hii mijadala ya DINI.
Kumbukeni kuwa ushabiki usio na mipaka hatima yake inaishia kutafutana na kutafunana. Kama mijadala itaenda kistaarab hapo ninaunga mkono ila mijadala ya humu ndani kuhusu dini inavuka mipaka. Wana imani kummbukeni kuwa hakuna mwenye haki zaidi ya mwenzake hivyo sote tunalindwa na katiba moja ndani ya nchi yetu.
Najua wengu humu wameishiwa na sera ndiyo maana wanachagua kuwa radical wa kidini.

Nashauri Mods labda kuiondoa hiki kipengele cha dini ktk JF au kuweka maadili mapya ya wanathreads wa dini.

Kumbukeni kuwa wenzetu (magharibi) wanafanya tafiti ktk mars lakini sisi tunashindana ktk kuamini. Naamini hata huyo Mungu anashangaa kuona hatutumii akili alizotupa kwa hekima....
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…