Dini kama janga linalofukarisha wasiotaka kushtuka, kujifunza, kubadilika, kubuni , na kuchapa kazi

Dini kama janga linalofukarisha wasiotaka kushtuka, kujifunza, kubadilika, kubuni , na kuchapa kazi

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Japo dini ni hazina tofauti na uganga wa kienyeji, upiga ramli, na utapeli, ni wachache wanaoelewa hivi.

Hebu angalia namna dini zinavyotufanya waswahili tuwe maskini tukitajirisha wale waliozileta.

Mosi, zina mfumo wa kuwatoa waumini kodi kwa njia haramu kama vile fungu la kumi, michango, sadaka, na zaka.

Pili, dini kama Roman Catholic, zilinyakua ardhi kubwa katika bara la Afrika. Kwa taarifa yenu, Kwa mujibu wa Madison Trust Company, Kanisa la Roma linashikilia nafasi ya kwanza kuwa na ardhi kuliko taasisi yeyote duniani.

Lina heka zipatazo 177,000,000. Kwa kulinganisha, ukubwa wa ardhi inayomilkiwa na Vatican, ni kubwa kuliko taifa la Ufaransa ambalo lina ukubwa wa heka 166, 757,337.

Ni zaidi ya nusu ya eneo la Tanzania yenye ukubwa wa heka 234,108,380. Kuonyesha mnyororo na ukoloni, familia ya kifalme ya Uingereza nayo inaongoza kwa kuwa na hekali 6,600,000,000.

Tatu, dini zinawajaza watu wetu ujinga na uvivu kwa kuwapa neno wakati zikichukua fedha toka kwao.

Nne, dini zinaua ubunifu na uwezo wa kufikiri. Kwanini kuishia pepo wakati maisha yako hapa duniani na jehanam? Unakuja jitu maskini wa kutupwa llinakataa kufanya kazi na kuwa bunifu llikingojea miujiza uchwa wakati miujiza yenyewe ni namna lilivyopumbazwa na kuibiwa mchana kweupe. Mijitu inauziwa kila upuuzi eti ibarikiwe. Baraka ni ardhi na utajiri uliomo unaotaka utumie japo common sense kuufaidi na siyo maombi wala miujiza.

Tano, dini zinasababisha chuki, chochoko, na mifarakano. Rejea tunavyoitana makafiri, wasiozaliwa upya, wenye dhambi na upuuzi mwingine.

Rejea baadhi ya nchi kama vile Afrika ya Kati waafrika wanavyouana tokana na kuwa dini tofauti.

Sita, dini zinachochea ukichaa na ugaidi miongoni mwa watu waliozoea kuishi kama ndugu. Rejea mauaji ya kimbari ya Rwanda na kwingineko.

Saba, dini zinajenga unafiki na fitina. Rejea kesi nyingi za ubakaji na uzinzi ima zinazokabili baadhi ya dini au vinavyoendelea kwa kisingizio cha dini.

Nane, dini zinatumiwa na serikali fisadi kuwapumbaza watu wake kwa kuwaaminisha kuwa masahibu na umaskini wao ni mpango wa Mungu.
Madhara ni mengi.

Ongeza uyajuayo.
KARIBUNI TUJADILI JANGA HILI KWA BARA LA AFRIKA
 
Unakufuru habari njema za wokovu uletao uzima. Labda kama unazungumzia dini za kishenzi, hizo zinajulikana sana tu, hata maeneo zilikoenea dini hizo kuna umasikini mkubwa sana. Haipaswi kuichukulia dini kwa mtazamo hasi na mtazamo mgando
 
Dini ni mfumo wa kitapeli.
Wanakuuzia matumaini hewa, wanakujaza hofu ili utawalike kisha unawalipa kwa sadaka, shukrani, zaka, matokeo, n.k

Greatest scam ever.
 
Unakufuru habari njema za wokovu uletao uzima. Labda kama unazungumzia dini za kishenzi, hizo zinajulikana sana tu, hata maeneo zilikoenea dini hizo kuna umasikini mkubwa sana. Haipaswi kuichukulia dini kwa mtazamo hasi na mtazamo mgando
Nawe unakufuru kwa kushindwa kutumia akili na kujua kuwa dini ni kiini macho cha kawaida.
 
Nawe unakufuru kwa kushindwa kutumia akili na kujua kuwa dini ni kiini macho cha kawaida.
kiini macho gani wakati dini imem maintain binadamu awe na mentality ya kiutu, namkufuru nani? Dini ndiyo ina regulate tabia za binadamu kuwa na adabu, heshima, hekima, busara na ustaarabu. Kufanya kazi kwa bidii na kupata maendeleo ni takwa la dini
 
Sadaka,zaka, mavuno ya parokia na Jimbo Bado harambee.
 
Unakufuru habari njema za wokovu uletao uzima. Labda kama unazungumzia dini za kishenzi, hizo zinajulikana sana tu, hata maeneo zilikoenea dini hizo kuna umasikini mkubwa sana. Haipaswi kuichukulia dini kwa mtazamo hasi na mtazamo mgando
Dini gani za kishenzi zaidi ya ulokole unao uamini ww?
Kuna dhehebu linalo tumika kutapeli watu na kuwafanya masikini na wapumbavu kama ulokole hapa duniani?
Hivi dini inayo muaminisha mtu eti anaweza kutajirika kwa maombi na si kwa kufanya kazi alafu utegemee mfuasi wake awe na akili?
 
kwanza elewa dhana ya ulokole ni nini ndio uje ujumuishi jadidi. Ulokole ni dhana potofu na si imani kama unavyofikiri na kusikia. Walokole ndio hao wanaotangatanga huku na kule wakitafuta miujiza na ishara, hawana imani na hawana msimamo. Naona hujui dhana ya ulokole na walokole, hata uislam na waislam hujui, unafuata mkumbo tu
 
Back
Top Bottom